Wazo: Eneo la Makaburi ya Viongozi na Mashujaa ya Kitaifa Haliko Tayari Dodoma?

Wazo: Eneo la Makaburi ya Viongozi na Mashujaa ya Kitaifa Haliko Tayari Dodoma?

Watanzania wenzangu poleni kwa msiba wa Mzee Mkapa. Tunapoendelea kuijenga Dodoma Kama Makao Makuu, ule mpango wa kuwa na eneo la Makaburi ya viongozi na Mashujaa wa Kitaifa ulifikia wapi? Sidhani Kama mfumo wa kuwazika Viongozi/Mashujaa kila mtu kijijini ni endelevu kwani watasahaulika na kukumbukwa na watu wa kwao.

Mfano Edward M. Sokoine wengi hawajapata na hawatopata nafasi ya kutembelea Monduli. Hilo ni kweli hata kwa Mwalimu Butiama au kwa Dr. Omar Ali Juma na Mzee Marine, Kawawa, n.k. Tunawazika ili kuwasahau!?

Kwanini tusianzie na Mzee Mkapa na baadaye kuhamisha Mikki ha Viongozi na Mashujaa huko Dodoma? Huko mbeleni watu wakienda Dodoma wanaweza kuzuru Makaburi ya viongozi wetu na hata Mashujaa wa kale ( tukihamishia makaburi huko)...tujenge na Maktaba Kubwa itakayotunza historia ya Marais (presidential library) katika eneo Hilo.

Tuanze na Marehemu Mzee Mkapa....RIP
Siku hizi unaingia jf kwa kunyata, utumwa mbaya sana
 
Wanapendelea wakawazike makwao sababu ndipo miungu yao ilipo.

Waliofika butiama wanajua naongea nini, kuanzia ardhi ya pale, milima, anga, hali ya hewa n.k

Wazikwe tu makwao, hakuna la maana ccm walotenda ktk hii nchi mpaka ifike hatua ya kukumbukwa. Hata uyo sokoine walimuondoa haohao.
Tukichukua nchi tunakwenda kufuta historia na uchafu walouacha maccm, hivi ccm watakumbikwa kwa lipi?
 
Back
Top Bottom