Wazo: Eneo la Makaburi ya Viongozi na Mashujaa ya Kitaifa Haliko Tayari Dodoma?

Wazo: Eneo la Makaburi ya Viongozi na Mashujaa ya Kitaifa Haliko Tayari Dodoma?

Maktaba hizo huwa chini ya Ungalizi wa Makumbusho ya Taifa ( National Arc hives)
Makumbusho ya Taifa ( National Museums) sio National Archives. Hawa wanazungumzia Presidential Libraries kama ile anayojengewa Obama Chicago. Ni taratibu ya Kimarekani.

Amandla...
 
Mashujaa wenyewe wako wapi?
Au unamuwaza JPM aje azikwe Dom?
Naamini huyu ndo shujaa wako namba moja
Mpaka Sasa sijaona shujaa

Shujaa katika lipi ?

Aliyoyafanya yangeweza fanywa na mwingine yeyote Kama wangepata hizo nafasi

Nataka kujua Hasa huo ushujaa unaopigiwa chapuo

Isije kuwa kasumba za kumtukuza marehemu ilihali wakati wa uhai wake mlizinguana na kutukanana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makumbusho ya Taifa ( National Museums) sio National Archives. Hawa wanazungumzia Presidential Libraries kama ile anayojengewa Obama Chicago. Ni taratibu ya Kimarekani.

Amandla...
Sawa ila hilo ni jukumu la makumbusho ya Taifa, lisiachwe pekee kwa wahusika.
 
Huu msiba mbona umepoa sana? Ule wa marehemu Ruge na Mengi ulikuwa active sana. Kulikoni Wamatumbwi wenzangu?
 
Mkuu Mimi sioni mantiki ya kuwa na Makaburi makao makuu ya nchi japo si wazo baya pia ila mimi naona Badala ya kutengeneza eneo moja na kuzika hawa dignitaries ni bora kwa Top Dignitaries kama Rais, VP au PM au Speaker wazikwapo vijijini kwao basi hapo pajengwe Library na viwekwe vitu vya hao viongozi hii itachangia utalii na mambo mengine mazuri katika huo mji, Inshu ya kuwa na national cemetery kwangu naona italeta Jam na kumbuka waamuzi wa mwisho wa Mpendwa wao azikwe wapi ni family hata mtu awe Rais ila still familia ndio final say japo ita consult na Serikali ndio mana baadhi ya familia baada ya ile Final tribute basi kunakuwa na Private burial inayo consist family members na waalikwa wachache, Fare thee well Ben
 
Kwa hiyo wengi ndo watapata nafasi ya kwenda Dodoma?

Msingi ni kwamba mtu akitaka kutembelea anakwenda eneo moja anakutana na hao "heroes" wote

Sio sasa utaenda Monduli kwa Sokoine halafu ukatishe uende Monduli kwa Lowassa ukitoka hapo uende Zenji kwa Dkt Ali upitie na Mkuranga kwa Mwinyi unaunga Masasi kwa Che Nkapa unapitia Ruangwa kwa Majaliwa unarudi Dodoma kwa Chigweyemisi upandishe Milimani kwa Msuya bado Butiama kwa Mwalimu sijui kwa Warioba

Ikiwa sehemu moja chini ya Makumbusho ya Taifa mji mkuu(Dodoma) kama walivyopanga unatunza historia na pia ni sehemu ya utalii wa kihistoria
 
Mkuu Mimi sioni mantiki ya kuwa na Makaburi makao makuu ya nchi japo si wazo baya pia ila mimi naona Badala ya kutengeneza eneo moja na kuzika hawa dignitaries ni bora kwa Top Dignitaries kama Rais, VP au PM au Speaker wazikwapo vijijini kwao basi hapo pajengwe Library na viwekwe vitu vya hao viongozi hii itachangia utalii na mambo mengine mazuri katika huo mji, Inshu ya kuwa na national cemetery kwangu naona italeta Jam na kumbuka waamuzi wa mwisho wa Mpendwa wao azikwe wapi ni family hata mtu awe Rais ila still familia ndio final say japo ita consult na Serikali ndio mana baadhi ya familia baada ya ile Final tribute basi kunakuwa na Private burial inayo consist family members na waalikwa wachache, Fare thee well Ben

Kuna kazi ukifikia level fulani unakua wewe ni mali ya Jamhuri sio familia tena

Kama ilivyokua kwa mujibu wa sheria(Ambayo naambiwa ilishafutwa??)
 
wazo zuri ila dah
nikiambiwa nitaje mashujaa bongo kwa haraka haraka naweza kumtaja diamond kiutani utani hivi hivi
neno mashujaa ni neno zito na kwa hapa bongo duh sijui hata nimtaje nani
 
Kuna kazi ukifikia level fulani unakua wewe ni mali ya Jamhuri sio familia tena

Kama ilivyokua kwa mujibu wa sheria(Ambayo naambiwa ilishafutwa??)
Mataifa ya wenzetu yanaheshimu sana mazishi inshu za public zitafanyika ila Katika kuzika Family ndio itaamua, Nadhani pia umefatilia Msiba wa Bush Sr 41, sijajua sheria zetu
 
Mataifa ya wenzetu yanaheshimu sana mazishi inshu za public zitafanyika ila Katika kuzika Family ndio itaamua, Nadhani pia umefatilia Msiba wa Bush Sr 41, sijajua sheria zetu

Nimefuatilia mkuu

Mambo mengi huku kwetu yanaendeshwa msalagambo ndo maana watu wanaamua kufuata mila zao wakazikwe mashambani

RIP BWM
 
Sawa
[/QUOT
Eneo la Mashujaa lililokuwa limetengwa huko Dodoma kwa ajili kuzika viongozi lilishageuzwa matumizi yake. Rais Magufuli alimwuliza Mkapa endapo angetaka azikwe hapo, akakataa, vivyo hivyo kwa Mwinyi na Kikwete. Kwa kuwa JPM naye hakutakwa azikwe hapo, basi eneo likapatiwa matumizi mengine.
 
Back
Top Bottom