Wazo fyatu: Kuna michezo ingewafaa wanawake zaidi na mengine ingebaki ya wanaume tu

Wazo fyatu: Kuna michezo ingewafaa wanawake zaidi na mengine ingebaki ya wanaume tu

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Huwa naona michezo ya mpira wa miguu ya timu za wanawake na ngumi inayohusisha wanawake kama haina mvuto mkubwa sana kwa watu wengi.

Hili suala lisichukuliwe kama ni ubaguzi wa kijinsia kwa sababu hata wengi wa wanawake wenyewe wanavutiwa zaidi na timu za mpira wa kiume kuliko timu zao.

Mimi nafikiri ingekuwa na maana zaidi wanawake wajikite kwenye michezo kama Netball(mpira wa mikono), Tennis, kuogelea na mingine ambayo wangeweza kufanya vizuri na kupewa umuhimu zaidi. Hii mingine kama soka, ngumi na mieleka wangewaachia wanaume tu.
 
Mpira hapana,wanawake pia wacheze.

Ila sio ndondi kwa aina zake.hii michezo ya kupigana huwa naona ni ya kiwaki hata kwa wanaume,achia mbali hao wanawake.
Unaweza kunitajia mchezaji mmoja wa mpira wa wanawake bila ku Google?
 
Hujawahi ona wanaume wakicheza rede wewe
Rede kwa mwanaume ni kwa ajili ya kuangalia pichu za mamanzi peke yake.

Kipindi kile tupo watoto hatukuwa serious na rede kama rede,ila kuchunguza mademu.
 
Mimi nafikiri ingekuwa na maana zaidi wanawake wajikite kwenye michezo kama Netball(mpira wa mikono), Tennis, kuogelea na mingine ambayo wangeweza kufanya vizuri na kupewa umuhimu zaidi.

Miaka kadhaa ijayo, maybe 30, 40, 50 n.k hiyo michezo ya wanawake unayoona haina umaarufu kwa sasa itakuwa maarufu.

Nyuma kidogo soka la wanawake lilivyoanza Ulaya na nchi za Amerika, haukuwa ukivutia sana kutizamika sababu ya kufanya ulinganifu na namna wanaume wanacheza.

Lakink kwa sasa hivi timu za taifa za wanawake kama USA, Canada au Netherlands zikiwa zinacheza, ni kama unawazama mpira wa wanaume tu.
 
Mchezo wa mpira kwa wanawake ni mpango wa haki sawa na zaidi sana umebase ku promote usagaji
Kuna mtu aliwahi kusema hivi pia sikuwahi kumwelewa,. Unaweza kutufafanulia zaidi kiongozi??
 
Hata sasa hivi huko Ulaya, Canada na USA soka la wanawake bado halina msisimko sana, kinachowasaidia sana ni kwa sababu taasisi na mashirika mbalimbali yanawekeza pesa nyingi kwenye hiyo michezo pamoja na sera za usawa, ila bado passion ya raia sio kubwa kivile.
 
Huwa naona michezo ya mpira wa miguu ya timu za wanawake na ngumi inayohusisha wanawake kama haina mvuto mkubwa sana kwa watu wengi.

Hili suala lisichukuliwe kama ni ubaguzi wa kijinsia kwa sababu hata wengi wa wanawake wenyewe wanavutiwa zaidi na timu za mpira wa kiume kuliko timu zao.

Mimi nafikiri ingekuwa na maana zaidi wanawake wajikite kwenye michezo kama Netball(mpira wa mikono), Tennis, kuogelea na mingine ambayo wangeweza kufanya vizuri na kupewa umuhimu zaidi. Hii mingine kama soka, ngumi na mieleka wangewaachia wanaume tu.
Ni mazoea tu toka enzi na enzi. Tumehubiriwa kazi, michezo, mavazi, etc kati ya two sexes. Vizazi vijavyo ,wanaozaliwa leo wakikuta wanawake katika michezo hiyo hawataona distinction! Ni sawa na ushogo, tunaona ni ushenzi kwa vile tumezaliwa tukiambiwa hivyo kila dakika kuwa ni dhambi, Mungu hapendi, jamii haipendi, tukachukia ushoga. Vizazi vijavyo after say 500 yrs kitakuwa kitu cha kawaida!
 
Hivi Taifa stars inaweza kufungwa na timu ya Taifa ya wanawake ya Brazil?
 
Umenikumbusha rede nikiwa mdogo 😁😁 nilikua napenda kuwa matazamaji wa huu mchezo mno😊

Je jee uliishia tu kupenda kuwa mtazamaji? Sema ukweli nikupe zawadi. 😂

Sisi tunaocheza Aikido na Wu-Shu tufanyeje?😂😂😂
 
Je jee uliishia tu kupenda kuwa mtazamaji? Sema ukweli nikupe zawadi. 😂

Sisi tunaocheza Aikido na Wu-Shu tufanyeje?😂😂😂
Ukiangalia rede kuna uhakika wa kuona chupi🤣
 
Back
Top Bottom