Wazo Gomvi: Kabla ya Kujitoa CHADEMA Ingeeleza Hili Kwanza...

Sasa unakuwa synonym wa upuuzi...unaandika kana Kwamba Chadema waliruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa kuandaa wagombea wao...UNAANDIKA UJINGA SANA YAN!
 

Mkuu naona unabariki na kuhalalisha sera za kiharamia.
Unaipenda kweli hii nchi au kwa kuwa uko ‘mbinguni’ Marekani basi si tatizo kwako tukitawaliwa na magenge ya uhalifu ambayo hapo mwanzo yalikuwa vyama vya siasa?
 
Ni lini CCM wamekuwa wakiheshimu sheria walizotunga wao wenyewe? usiniambie kuwa hili limeanza baada ya kuja Magufuli...
Hata kama sitasema hivyo, ujio wa Magufuli na staili yake ya uongozi na mambo mengine yasiyostahili kuandikwa hapa; yanafanya hali hii ya sasa iwe tofauti saaaana, na ile ya miaka iliyopita..., wewe hilo hulioni?

Hatukuwahi kusikia vyama vikipigwa marufuku kufanya siasa..., hii ni haki inayosimamiwa na Katiba. Hakuna aliyethubutu kuikiuka huko nyuma hata kama walitamani iwe hivyo.

Tuliona Mahakama, angalao kwa kiasi fulani zikijitahidi kulinda haki na usawa. Kuna wapinzani walioonewa na kuporwa ushindi, wakaenda mahakamani wakasikilizwa. Leo hii kwenda mahakamani ni kupoteza muda, au wewe huoni tofauti hiyo?

Sikuwahi kusikia haya matatizo ya kipumbavu kabisa ya watendaji kujificha na kufunga ofisi wasipokee fomu za wapinzani. Unaweza kutoa mfano wowote wa aina hiyo uliotokea huko nyuma?

Kauli tu zinazotolewa na viongozi : 'nikulipe mshahara, nikupe gari,..,n.k', ni kiongozi yupi aliyewahi kutoa vitisho vya aina hiyo huko nyuma.

Na ni kwa tofauti hizi ndio maana upinzani ulianza kukua na kushamiri..., na wananchi kuanza kuwa na uhuru wa kuwachagua viongozi wao kwa uwazi na bila vitisho.

Sasa hivi, kila jambo ni vitisho na kutumia polisi kudhibiti hata hiyo fursa ndogo iliyosalia.

Baada ya yote haya, bado unaweka mawani ya mbao usione utofauti kati ya sasa na huko tulikotoka. Hii ndio sababu unayofanya watu wasielewe lengo lako hasa ni nini unapoleta mada kama hizi hapa JF.
 
we mzee kumbe unatakiwa ufe ili kizazi kiendelee japo sikuombei hilo mungu anisamee . we mzee hujui kama ofsi zilifungwa na fomu hazkuludishwa baadhi mpaka watu wakapiga kelele ndpo jafo akasema watendaji waskimbie mwandishi gan wew wahovyo unaeandika bila kufatia, hivi hata kwa mawazo ya kawaida vyama vyote vya upinzani vimeshindwa kujaza form emu waache chadema je ACT wazalendo nayo haikufundisha watu wake nimalize kwa kukutukana
 
Mkuu
 
Kweli Sasa Umezeeka, Hata zile Busara za Mawazo zimekupotea Mzee wetu wa Kijiji.[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Imenibidi nirudi kwenye mada yako, nisome ile sehemu ambayo sikuisoma nilipoanza kuweka mawazo yangu juu ya mada hii.

Mzee Mwanakijiji, ukiwa mtu mwenye dhamira ya kweli, huru kabisa, na kusukumwa tu na mapenzi ya usalama wa nchi yako; sijui ni kipi kitakachokupa msukumo uyaandike hayo uliyoandika hapo juu!

Lakini hata kama msukumo unatokana na maslahi yanayotokana na kazi unayoifanya, nadhani dhamira ile ile ya kulijali taifa lako itakufanya uwe na mstari usioweza kuuvuka katika utetezi wa maslahi binafsi zidi ya ustawi wa taifa lako.

Nadhani nimehitimisha uchangiaji wangu katika mjadala wa mada hii.
 
Miaka yote watu wanajaza fomu, wengine ni wenyeviti wana mihura zaidi ya mmoja eti hawajui kujaza fomu akili za maji ya bendera ya kijani hizi.
 
Huyo mzee amekuwa mtu wa hovyo sana. Hata mimi nasikitika zamani kupoteza muda kumfuatilia. Kwasasa anafikiria kama mtu aliyechanganikiwa kabisa, hawezi tena kuhoji wala kuchanganua.
 
Eti mtu adinde kwenye ofisi za tume/kata "hatutoki hapa bila kupokea form" sasa si utafunguliwa kesi ya kuchochea vurugu kwani nani asiejua?

Au kama mpokeaji haonekani wewe utakomaa mpaka sangapi kumsubiri mtu asionekana
 
Mzee Mwanakijiji unafahamu yote yaliyofanyika ila tu unatimiza wajibu kama ambavyo Selemani Jafo anafanya.
Hamuwezi kuaminisha na hamna haki ya kuwafanya watanzania wajinga kwa hilo. Kanuni ya mabadiliko inasema "nothing static". Watanzania kama siyo wamebadilika basi wana-undergo evolution process. Kwahiyo unahitajika uongo wa hali ya juu zaidi kumdanganya mtanzania huyu.
Kurudisha nyuma historia kuna kazi.
 

Mvua huwa inanyesha jangwani.

Amandla.......
 
Leo nimesoma mahali kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kuwa kuna kuna chama kimeandikishwa kama Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) kwa hiyo waliojaza ACT Wazalendo walistahili kuenguliwa kwa sababu hamna chama kama hicho. Huyu Mheshimiwa amesahau kuwa acronym ikiwekwa kwenye parantheses baada ya jina kamili lenyewe inamaanisha kuwa acronym hiyo inaweza kutumika badala ya jina kamili. Katika mazingira kama haya isingesaidia kitu hata kama wangerudisha fomu siku ya kwanza maana inaelekea kuwa wasimamizi walikuwa hawana nia ya kuhakikisha kuwa wale wote waliotaka kugombea wanapata nafasi hiyo. Ili kukata mzizi wa fitna fomu ZOTE zilizowasilishwa zingewekwa wazi ili wananchi wajionee wenyewe.

Amandla.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…