Nampurukano
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 1,196
- 1,456
Mzee mwanakijiji unauliza maswali ya kisomi kwenye mchakato wa uchaguzuzi wa kiprimitive. Sio kweli kwamba ccm wanajua kujaza fomu kuliko wapinzani. Elimu ya kibongo wewe unaijua uelewa hauna huyu ni chadema au ccm. Kwanza elewa kwamba fomu haziko pale kutuchagulia kiongozi, fomu zimewekwa kutupa taarifa zamgombea tutakaye mpigia kura. Msimamizi au msimamizi msaidizi wa uchaguzi sio msimamizi wa mtihani ni mwelekezaji wa fomu anayotoa kama ilivyo kwa afisa uhamiaji anapokupa fomu ya kuomba passport. Fomu ni mchakato wa kupata taarifa za mwombaji wa nafasi ya uongozi sio paper ya kutuchagulia wa kuingia kidato cha kwanza. Hii ndio demokrasia tunayotaka itupeleke kwenye uchumi wa kati.
Asikudanganye mtu ccm haijatoa semina elekezi yoyote kwa wagombea wao kilichowasaidia ni wasimamizi wa uchaguzi kuwaelekeza jinsi ya kujaza na sehemu nyingine kuwajazia fomu zilizokosewa. Kwa upande wa wapinzani fomu zao nyingi zilihujumiwa ikiwa ni pamoja na kujaziwe zingine zenye makosa ya makusudi kwa wale waliojaza kwa usahihi.
Kurudisha fomu mapema hakuwasaidii wapinzani kwa sababu wasimamizi wanapata muda mzuri wa kuzihujumu fomu na ndio maana zinaporejeshwa dakika za mwisho wanafunga ofisi na kukimbia kwa kuhofia kwamba wakizipokea hawatapata muda wa kuzihujumu zitakuwa sahihi hivyo wanaona ni afadhali kukwepa kuzipokea kuliko kupokea halafu ukampitisha mpinzani. Watendaji wa vijiji na mitaa walipewa maelekezo ya kuwafyeka wapinzani mapema ili watu wasiingie kwenye uchaguzi. Hivyo theoretically utaona wapinzani ni wazembe lkn practically wapinzani kukwepa hujuma za ccm na watendaji wa serlikali ni vigumu sana.