Hii mada si mpya, tulishwahikuijadili wakati wa Ubunge. Nipo katika rekodi nikihoji mantiki ya kurudisha fomu dakika za mwisho.
Tukasema kuna technical issues ambazo Wapinzani lazima wajue namna ya kuzikwepa.
Katika mazingira ya leo hilo haliwezi kutatua matatizo wanayoyapata
"Nyani Ngabu, post: 33416398, member: 188"]
Sina hakika kama CDM wana idara ya 'Compliance' iliyo na compliance officers.
Kama hawana, ni vyema wakafikiria kuanzisha idara kama hiyo itakayohakikisha kuwa chama na wagombea wake wa ngazi zote wanakuwa in full compliance with election law.
Mbunge hawezi kufanya kampeni nje ya eneo lake.
Akiwa ndani ya jimbo lake haruhusiwi kuongelea jambo lolote isipokuwa ''shida''
Huyo compliance officer atafanya nini?
Mwenyekiti wa chama cha upinzani haruhusiwi kufanya maikutano nje ya jimbo lake.
Iwe ni ACT au Chadema! Compliance officer atafanya kazi kitongoji gani?
Shughuli za siasa hadi 2020, compliance officer atafanya kazi lini na wapi?
I mean tuweni wakweli wa nafasi zetu
Idara kama hiyo pia inaweza kutoa mafunzo kwa watendaji wa chama kuhusu chaguzi na mambo mengine yahusuyo sheria kwa ujumla katika sehemu mbalimbali nchini hata nyakati ambazo si za uchaguzi.
Mwenyekiti wa chama haruhusiwi mikutano, huyo compliance office atatoa mafunzo wapi?
Umezungumzia kuhusu chama ku cover all the bases. Ni kweli. CDM hawawezi kabisa ku afford kutenda 'unforced errors'.
NCCR? ACT?
Kuna unforced error lakini tusifumbie macho uhuni unaoendelea kwa kisingizio hicho.
Unaamini kabisa CCM wamejaza fomu kwa usahihi nchi nzima na kwamba walikuwa na Wanasheria kila kitongoji!
CDM inapaswa kuifanya kazi ya CCM/ serikali kuinyanyasa iwe ngumu sana. Lakini siyo kuwarahisishia CCM na serikali yake kuwanyanyasa kupitia makosa yao madogo madogo ya kiufundi.
Kuchukua fomu kunahitaji ufundi gani?
Watu walikatwa mapanga kuchukua fomu! Hawa waliokatwa mapanga walifanya makosa gani ya kiufundi?
Kuna makosa ya Upinzani na moja nimelieleza katika uzi wa Mwanakiji wiki moja kabla.
Kwamba mazingira yaliyopo yalitengenezwa watu wajiandikishe kujenga uhalali wa uchaguzi
Watu wamejiandikisha ,kilichofuata ni kuengua wagombea ili ushindi wa asilimia 99 upatikane
Hili mbona wengine tuliliona hata kabla ya juzi au jana.
Tuliwaambia Wapinzani wanachokifanya ni jaribio la kuhalalisha madhaifu.
Leo nashangaa wanalalamika!
Nasi wananchi tuna shea yetu. Tumekuwa ''partisan'' au washabiki sana kiasi kwamba tunadanganywa na akina Mwenezi na kukubali kuwa kuna makosa wamefanya wapinzani
Hatujishughulishi kuangalia kama kuna ukweli, tunalaumu tukifumbia macho mapanga vichwani
''Nione umamtangaza mpinzani''! halafu leo tunadhani kuna matatizo ya ufundi!