Cherenganya
JF-Expert Member
- Jan 21, 2018
- 2,309
- 1,785
Paragraph yako ya tatu, umetoa utumbo na firigisi badala ya hoja,. Kwahiyo kama mwenyekiti wa serikali za mtaa hana uwezo wa kuandika vizuri anakuaje kiongozi katika karne hizi ambazo kila mtaa una DIGRII za kutosha.Mapendekezo ya wagombea ni suala la wananchi husika ku propose kiongozi wanayemtaka.
Hizo technicalities lazima ziwe rafiki kwa uchaguzi, kwa mfano kama mtu ni jambazi na ana record hiyo ni automatic rejection.
Lakini kuongeza vipengele utafikiri mtihani wa form IV , hiyo ni kuua demokrasia.
Mimi CCM damudamu lakini nisingependa kushindana na ombwe.
Technicalities haziwezi kukimbiwa kwakua ndizo zinazoibeba tasnia ya Sheria duniani, namna vifungu vinavyo tafsiriwa, na ndipo tunapoweza kumpima mwanasheria.
Hivyo ukikutwa na kosa la "technicalities" usilalamike tafuta sheria inayothibitisha kinyume na hicho walichosema.
CCM waliangalia udhaifu wenu na kuufanyia kazi, ni wakati nanyi kuangalia udhaifu wao ili muwapige bao.