Wazo Gomvi: Kabla ya Kujitoa CHADEMA Ingeeleza Hili Kwanza...

Mzee mwanakijiji unauliza maswali ya kisomi kwenye mchakato wa uchaguzuzi wa kiprimitive. Sio kweli kwamba ccm wanajua kujaza fomu kuliko wapinzani. Elimu ya kibongo wewe unaijua uelewa hauna huyu ni chadema au ccm. Kwanza elewa kwamba fomu haziko pale kutuchagulia kiongozi, fomu zimewekwa kutupa taarifa zamgombea tutakaye mpigia kura. Msimamizi au msimamizi msaidizi wa uchaguzi sio msimamizi wa mtihani ni mwelekezaji wa fomu anayotoa kama ilivyo kwa afisa uhamiaji anapokupa fomu ya kuomba passport. Fomu ni mchakato wa kupata taarifa za mwombaji wa nafasi ya uongozi sio paper ya kutuchagulia wa kuingia kidato cha kwanza. Hii ndio demokrasia tunayotaka itupeleke kwenye uchumi wa kati.
Asikudanganye mtu ccm haijatoa semina elekezi yoyote kwa wagombea wao kilichowasaidia ni wasimamizi wa uchaguzi kuwaelekeza jinsi ya kujaza na sehemu nyingine kuwajazia fomu zilizokosewa. Kwa upande wa wapinzani fomu zao nyingi zilihujumiwa ikiwa ni pamoja na kujaziwe zingine zenye makosa ya makusudi kwa wale waliojaza kwa usahihi.
Kurudisha fomu mapema hakuwasaidii wapinzani kwa sababu wasimamizi wanapata muda mzuri wa kuzihujumu fomu na ndio maana zinaporejeshwa dakika za mwisho wanafunga ofisi na kukimbia kwa kuhofia kwamba wakizipokea hawatapata muda wa kuzihujumu zitakuwa sahihi hivyo wanaona ni afadhali kukwepa kuzipokea kuliko kupokea halafu ukampitisha mpinzani. Watendaji wa vijiji na mitaa walipewa maelekezo ya kuwafyeka wapinzani mapema ili watu wasiingie kwenye uchaguzi. Hivyo theoretically utaona wapinzani ni wazembe lkn practically wapinzani kukwepa hujuma za ccm na watendaji wa serlikali ni vigumu sana.
 
We jamaa sijui umekula maharage ya wapi wewe??
 
Bravo kaka
 
Chadema hawapo tayari kushika dola,

Tunawapima kwenye mambo kama haya na kuwaona kuwa hamtoshi,

Sasa Chama kina wagombea ambao hata kujaza fomu hawawezi??
 
Mzee unasikitisha Sana...wakati mwingine uwe unatuoia tu...hata ukiwashwa
 
Mzee Mwanakijiji, nimekuheshimu sana muda wote tangu nimekufahamu.

Hivi katika tathmini yako ya haya yanayotokea wewe unaona lawama ielekee kwa victim wa udhalimu?

Huyo mdhalimu Una neno gani kumhusu ?
 
5. CDM iliwaandaa watu wake vipi kubanana na wale wasimamizi ambao walikuwa wanaonekana kweli kuwakwepa. Hivi kweli CDM na vijana wake hakuna watu wenye kusema "hatutoki hapa hadi mpokee fomu zetu"? Ni upinzani gani huu!


Mkuu unahabari hadi sasa hivi vingozi wa upinzani wanaendelea kuwajibika mahakamani kwa kifo kilichosababishwa na askari kufyatua risasi wakati wa uchaguzi wa Kinondoni?

Unaongeleaje faulo walizofanyiwa wagombea kabla hata ya kujadili jambo la ujazaji na urudishaji wa hizo form?
 
Wangetumia mbinu gani katika mazingira haya ya awamu hii?

Je hakuna faulo za wazi zinazofanyika? Faulo zinapofanyika na kulindwa na nguvu ya dola, ungekuwa wewe kiongozi ungefanya nini?
 

Hujasema sababu za kuenguliwa.
 
Hivi unaongea nini wewe?
 
Mtu aliyezoea kupiga mawe nyumba ya vioo dawa yake ni kumwekea vyuma ili akirusha jiwe kizembe lidunde na kurudi kwake.

Hao wasimamizi hawataacha kufanya hivyo mpaka watakapoona malipo ya matendo yao maovu kuwa ni hasara kwao.
Kwa sasa malipo ya matendo yao ni furaha na anasa wanazopata baada ya kupandishwa vyeo.
 
Bado mnahaingashana na hizi siasa za bongo?toka 2000 mi mshabiki tu
 
Siku hizi ninapata shida sana kukusoma MMK; kiasi kwamba hadi nimefikia mahali nikiona mada yako, nasita kuisoma.
Hii mada nimeiona tokea mwanzo ilipowekwa hapa. Nikaghaili kuifungua.
Mwisho wa siku, uvumilivu ukanishinda, nikafungua kuchungulia kuna nini.

Baada ya kuanzia kusoma mwisho wa mada na kufikia maswali uliyouliza, nikajikuta nikiunga mkono maswali yale.

Kiufupi, ningependa sana CHADEMA waeleze, wajibu maswali hayo moja baada ya jingine.
Haya maswali ndio msingi imara wa uimara wa CHADEMA, na ndio hayo hayo wengi tunaopenda upinzani wa kweli na wenye nguvu wawe na uwezo wa kusema tulifanya hiki na hiki kuwafikia wananchi huko waliko, sio kwa mikutano tu, zipo njia nyingi za kufanya hivyo.

CHADEMA, au kama wapo wawakilishi wao hapa, wekeni majibu juu ya maswali aliyouliza Mkuu Mwanakijiji, haya ni maswali ambayo nasi wengine tunayo shauku kubwa kujua majibu yake.

Sikusoma hadi mwanzo wa mada, kwa hiyo sijui huko juu mada inaeleza nini. Kama anawashabikia CCM, na hasa mtu wake kama kawaida yake, hayo nayapinga, hata bila kuyasoma.
 
Tatizo Hawa watu wamegoma kujua kuwa siasa ni Game Of Timing. Kwenye siasa unapokosea ni furaha na ushindi kwa mpinzani wako. CCM walijiandaa kuwachinja wapinzani wao kwa style hii. Ndio maana wao CCM hakuna mgombea aliyejaza form nyumbani kwake. Wote walijaza chini ya uangalizi wa wanasheria wa chama walio sambazwa nchi nzima.
 
Mzee Mwanakijiji

Hoja zako zina mantiki katika mazingira fulani, haya yaliyopo zinakosa nguvu

1. Wapinzani wanaweza kutekeleza yote uliyosema lakini hali ikabaki kama ilivyo
Dahamira ya uovu ambayo haiwezi kukosa sababu halali au za kutunga

2. Polisi anaposimama akisema ''CCM watembee kifua mbele ndiyo wenye dola'' ,unategemea nini?

Mgombea anaweza kurudisha fomu siku 5 kabla na ikatungwa sababu analeta vurugu, Polisi wakatenda yao.

Ndiyo hayo hayo ya vijana kukusanyika wakimtaka msimamizi awepo, wataishia kupigwa mabomu

3. Hivi makatibu kata walioitwa nani atathubutu kuwaambia wanafanya makosa?

3. kuchukua Fomu watu wamekatwa mapanga na hakuna hatua, hivi hapo kuna dhamira njema?

4. Mgombea anaweza kurudisha fomu na msimamizi akakaa nazo na muda ukifika akasema majibu hayo hayo

Orodha inaendelea, na kwahilo hata uzembe wa Wapinzani unapata utetezi! Uhuni unazidi uzembe

Hivi unakubaliana na hoja kwamba CCM waliweka wanasheria kila kitongoji n.k.!!

Katika uongo wa namna hii hivi tunahitaji darubinu kubaini kuwa Dhamira imetimizwa kwa uzuri na ubaya

Nafsi zinawasuta hadi kusema uongo wakiangalia kamera, nini kinawashinda?
 
Maswali ya kipumbavu. hv unaishi Tanzania kweli?Hakuna technical zilizojitokeza ni uhuni mtupu wa CCM na serkali yake. Achana na na hoja za kitoto. Nyambafu
Nikiacha hilo la "maswali kuwa ya kipumbavu", ninakubaliana nawe kabisa katika hayo mengine uliyoyaandika kuhusu "kuwepo na technical zilizojitokeza...."

Lakini, pamoja na kukubaliana nawe katika hilo, je wewe huoni kwamba kama CHADEMA waliyafanya maandalizi ambayo Mzee Mwanakijiji kayawekea maswali, kwamba hiyo ni kwa faida ya CHADEMA yenyewe?

Mimi ningependa CHADEMA wawe wameyatimiza yote hayo yaliyowekwa kwenye maswali ya mleta mada, kwa sababu kuu mbili:

Mosi, huo ndio ungekuwa ushahidi usiopingika kwamba CHADEMA wamehujumiwa kwa sababu watu wao waliandaliwa ipasavyo, na wasingeweza kufanya makosa yanayodaiwa waliyafanya na kutopitishwa kuwa wagombea. Tungejua bila ya shaka yoyote, kwamba hizi ni hujuma zinazofanywa na watumishi wa serikali.

Pili, kufanya yote yale yaliyoulizwa kwenye maswali ni kuiimarisha CHADEMA yenyewe, hadi katika ngazi za chini kabisa. Ni mpuuzi gani atakyechezea CHAMA chenye wanachama walioiva barabara na kuzijua haki zao ipasavyo. Hao wanaofunga ofisi na kukimbia wasingethubutu kamwe kufanya upuuzi huo.

Naomba CHADEMA wayajibu maswali yaliyowekwa na Mzee Mwanakijiji.
 
Zamani wewe Mwanakijiji ulikuwa angalau na busara kidogo, Lakini sasa tangu Magufuli aingie madarakani unaonekana umepoteza mwelekeo. Unachojua ni kumtetea Magufuli na serikali yake na yote mabaya ambayo anayoyafanya unaona ni sawa. Hivi ufikiri wako umehamia wapi? Wewe kwa akili yako unaona ni sawa CDM kukatwa wagombea wake kwa asilimia 96%, ACT wanaambiwa hakitambuliki na msajili na malaki ya wagombea wa vyama hivyo viwili wameenguliwa, watendaji wa serikali wanachana forms za wapinzani waziwazi na wagombea wanaambiwa wakashtaki popote! Forms zingine za wagombea za wapinzani zimeongezwa sifuri, hivi kweli kuna mtu anayeweza kuandika 19790 na watu zaidi ya elfu moja wakosee hizo numbers??? Acheni utani, mkitaka kuiba basi muwe na akili kidogo! Tanzania hakuna DEMOKRASIA wala uchaguzi uliofanyika kihalali na huyu Magufuli sasa anafanya waziwazi...KAMA ANAPENDWA ANAOGOPA NINI KUFANYA UCHAGUZI WA HALALI? Kwanini anakamata watu kwa kutoa mawazo yao? Kusema tu vyuma vimekaza unapaswa ukamatwe??? Serikali ya Magufuli ni duni na primitive kuliko serikali zote zilizopita. Wewe Mwanakijiji unatetea uovu au ni hulka ya Wasukuma kutetea home ports wao? Tumia angalau sense kidogo....uonevu wa wazi lakini unabwabwaja tu...unataka vyama vingine vifanye nini zaidi? Mwambie Magufuli na serikali waache uonevu na kuua watu....Watanzania wanahitaji kuheshimiwa asituletee mambo ya Usukumani. Mmezoea kuua watu wasio na hatia....Mnaua wazee(Mababu na Mabibi zenu), Mnaua Albino, mnachuna ngozi watu na mnaongoza kwa kubaka watoto huko Geita na sasa mnaanza kuleta matatizo nchi nzima...BAKINI HUKO HUKO NA MATATIZO YENU!
 
Hivi unakubaliana na hoja kwamba CCM waliweka wanasheria nchi nzima, yaani kwa idadi ya wanasheria tulio nao wote wakiajiriwa hata wilaya moja haitoshi, I mean kuanzia vitongoji n.k.
Hapa tunaweza hata kuanza kuuliza swali.
Je, ni jukumu la nani kuelimisha walengwa (wagombea).
Hili sio jukumu la Tume ya Uchaguzi kwa Vyama vyote? Kama fomu ina mambo ya kisheria ambayo sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuielewa, kwa nini liwe jukumu la vyama vya siasa kutoa tafsiri ya fomu hizo?

Kwa nini fomu zenye lugha rahisi, inayoeleweka na mtu wa kawaida hadi huko vijijini isitumike?

Je, CHADEMA wanaweza kwenda mahakamani kudai/kupinga hili na wakasikilizwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…