Wadau wanaoamini katika ubia natafuta wazo la biashara na uwekezaji usiozid milion 100.
Nina parameters zangu
1. Mwenye wazo awe shareholder wa biashara yenyewe hata kama hana mtaji wa pesa. Akili ni mtaji mkubwa
2. Biashara iwe ya uzalishaji wa product flani na sio biashara ya kununua na kuuza
3. Uzalishaji uwe dsm hata kama malighafi inatoka popote
4. Bidhaa iwe na faida inayodhirika na sio faida mtambuka. Kuwepo na uhitaji kidogo wa kusimamiana na auditing rahisi
5. Isiwe bidhaa ya msimu wala inayoleta faida kimagumashi. Isilete mgogoro na TRA.
Wazo zuri tutaanza kikao mara moja.
Habari Mkuu;
1. Spice, Herbs and Fruits value addition/processing.
a. Extracts (Spices, herbs and fruits)
Extract maarufu kuliko zoteni Vanilla, ingawa zinaweza andaliwa nyingine nyingi kama mango, apple/cider, tamarind, pineapple, orange, lime, lemon, lemongrass, cinnamon, mint, rubber vine fruit, ginger etc. Tanzania matunda yapo mengi(moja ya marketing ideas ni ku-provide a taste of ''exotic"). Malighafi zote zipo, na vitendea kazi vyote vinapatikana hapa bongo. M
Masoko ni mtu binafsi, mama/baba ntilie, bakery zinazofunguliwa kila siku, restaurants, hotels etc.
b. Essential Oils(Spices, herbs and some fruits(parts of a fruit(s)))
Essential oils ni mafuta yatokanayo na viungo na mitishamba mbalimbali, kama ganda la chungwa, limao(lime, lemon), cinnamon, cardamom, lemongrass, mint, eucalyptus leaves, pine needle leaves, ginger, garlic, rosemary, rose(the flower), na serikali ikija kuufikiria bangi(CBD essential oil) etc.
Matumizi ni Aromatherapy, Pharmaceutical na Food&Beverage sectors.
Masoko ni watu binafsi, vituo vya massage, wellness and relaxation Spa, kama ingrident ya sabuni na perfume (Essential oil tutakayozalisha ikiwa Aromatherapy grade).
Makampuni ya dawa(kama essential oil tutakayozalisha itakuwa Pharmaceutical grade).
Makampuni ya vyakula na vinywaji(food and beverage) kama essential oil tutakayozalisha itakuwa Food grade.
c. Oleoresins( Spices and herbs)
haya ni mafuta-mgando(semi-solid) yatokanayo na uchakataji wa viungo na mitishamba. Yanasifa ya kuwa na vitu vingi zaidi ya essential oils.
matumizi yake ni mengi kuanzia utengenezaji wa mabomu ya machozi (vurugu zitokeapo, yanatumika sana kote duniani) mpaka kwenye mapishi,vinywaji, rangi za chakula na vinywaji.
Mfano ni ginger, turmeric, garlic, onion, cinnamon, cardamom etc.
NB; Kama utakuwa huru na kukubaliana na uwekezaji katika maeneo mengi tanzania, nitatoa idea nyingi zaidi.
NB: Mtaji wangu ni idea(wazo), bado sijafanikiwa pesa.
Ahsante.