cha ajabu kuna mijitu humu inamsupport kuwa inawezekana....unajua humu kuna watu akili zao ni finyu sana kutokana na mazingira waliyokulia.
Chukulia scenario hii, mtu amezaliwa kariakoo, akasoma shule ya msingi mnazi mmoja, Secondary olevel na high school akasoma jangwani, au zanaki, au azania na au tambaza, chuo akasoma CBE dar campus....unategemea nini? Ndiyo kama huyu. Unakuwa na watu unawaona wasomi lakini mazingira walimokulia yamewaficha bongo zao they can not think beyond the box.
Yaan ni matatizo makubwa sana haya, watu wanakurupuka tu kucopy na kupaste kutaka kuwauzia watu mbuzi kwenye gunia bila ata kujua kuwa mazingira na demand ya huko walikocopy sio mazingira na demand ya hapa kwetu.
Wakiona kwenye internet jinsi library zinavyojaa huko Ulaya na Amerika na kuwa ni biashara ya uhakika basi nao anakurupuka tu bila ata kujua kuwa huko sio hapa na kuwa demand ni tofauti kabisa.
Picha: Wananchi wa Mbeya wakubwa kwa wadogo, wanaume kwa wanawake wamejazana library(NDOTO ZA MCHANA)
Hello Jamii forum members:
Wazo hilo hapo juu nawasilisha kwa ushauri; Mimi nimefanyia ANALYSIS nimeona ni social enterprise nzuri kwa watu wa rika zote; wanafunzi na wasio wanafunzi.
Jambo la msingi nataka project iwe designed kuwafanya watu wote wapendao kujisomea (makundi yote) iwe ndo sehemu yao ya kupata maarifa na kukutania kwa discussion ya masuala yao ya kitaalamu.
HIVI NDO NAANDAAA
BUSINESS PROPOSAL ( MIMI MWENEYEWE NDO FANI YANGU). KWA MWINGINE YEYOTE ATAWEZA JADILI NAMI KUONA NAMNA ANAVYOWEZA KUNITUMIA MIMI KUANDAA SUCH BUSINESS PLAN KWA AJILI YA KUFANYA IMPLEMENTATION SEHEMU NYINGINE YOYOTE (HASA KWENYE MAJIJI).
VISIT ME AT:
KIMI DEVELOPMENT CONSULT LIMITED
Eti kafanya analysis kuwa kuna demand, watu watakuwa
wanakusanyika kwenye hiyo library kujisomea na kukutana na kufanya discussion ya masuala ya kitaalam?really?
Picha: Wananchi/wasomi/vijana wa wamekutana jioni/weekend wakijadialiana masuala ya Kitaalam, na ndivyo wanavyofanya kila siku jioni baada ya kazi na kila weekend.(NDOTO ZA MCHANA)
Hivi kwani hao wasomi na wataalam walioko Mbeya kwa sasa uwa wanakusanyika wapi kujadiliana hayo mambo yao ya kitaalam??
Kumbuka hapa hazungumzii makongamano, warsha, semina au mikutano ambayo uwa inafanyika kwenye kumbi na wala hatuzungumzii vikao vya harusi ambavyo kwa Tanzania hufanyika pia kwenye ma-bar bali hapa
anazungumzia ENEO LA KUJADILIANA MAMBO YA KITAALAM.
Sasa je tatizo hilo lipo? maana ni lazima kwanza kuwe na tatizo la eneo la hao watu kukutana ndio hiyo library sasa ije kutatua hilo tatizo, maana huwezi kubini mbinu ya kutatua tatizo ambalo halipo.
Picha: Wananchi/wasomi?vijana wamekutana jioni/weekend wakijadialiana masuala ya Kitaalam, na ndivyo wanavyofanya kila siku jioni baada ya kazi na kila weekend.(NDOTO ZA MCHANA)
Huu ni ukanjanja tu huu, kaona nchi za wenzetu watu wanakusanyika library kudiscus basi anadhani na hapa Tanzania basi ikiwekwa hii watakuwa wanakusanyika KUJADILIANA MAMBO YA KITAALAM, alafu eti ndio Consultant mwenyewe.
Akimkuta hapo mtu asiyejua atamwambia nimeishafanya analysis, mimi ni msomi, nimeishaona kitaalam, wewe anzisha tu hii ina soko sana, kumbe soko kaliona kwenye net huko Ulaya na Amerika alafu anawauzia wajinga mbuzi kwenye gunia yeye anachukua pesa yake anaishia wateja wanaenda kuimplement wateja wanazama na kufilisika, yeye hawatamuona tena.
HIVI NDO NAANDAAA BUSINESS PROPOSAL ( MIMI MWENEYEWE NDO FANI YANGU). KWA MWINGINE YEYOTE ATAWEZA JADILI NAMI KUONA NAMNA ANAVYOWEZA KUNITUMIA MIMI KUANDAA SUCH BUSINESS PLAN KWA AJILI YA KUFANYA IMPLEMENTATION SEHEMU NYINGINE YOYOTE (HASA KWENYE MAJIJI).
VISIT ME AT: KIMI DEVELOPMENT CONSULT LIMITED
Saiz vishoka hawapo tanesco na waganga wa jadi, sikuhizi kila aliyeweza kudesa huko chuo na anayejua kucopy na kupaste kutoka kwenye internet nae anataka aitwe Consultant na awalie pesa wasiojua.