Wazo Muflisi: Alijaribu Kujitenga lakini Anarudi Bila Tenga...


Hakika umeandika kikubwa sana!
 
Kiufupi Tanzania ina sheria mbovu sana .....
Mwenye madaraka anajitapa sheria zile zipo za kuwashughulikia ...

Wananchi wao kazi yao ni kushangilia kila linalosemwa na Rais ...ndio maana humu kuna watu wanafurahi wapinzani washughulikiwe ...

Lakini hawaoni wala kujiuliza kwanini watu wanaumizwa tena makusudi kwa kukosoa uongozi ...

Wanaona bora zitumike njia za mtangulizi kuweka mambo sawa ...lakini kuna siku hali hii itageuka kwetu wote na kuhamaki kama katiba itabaki hii ya miaka 47 iliyopita
 
Kujikosha kuwa yeye ni mama alikula matapishi matakatifu ya Bw. Yule lakini bahati mbaya yakawa magumu yakashindwa KUMENG'ENYEKA si kwa maji wala umeme simu zenyewe zikashindwa kupigika Mama shingoni akakabika mratibu mkuu akaona isiwe tabu akajitoa pembeni akakaa. Kijana aliyekuwa nje akarejea akiwa kibri mabega juu akagonga koromeo la mama mwisho matapishi matapikwa yakatapikwa kwa mara ya pili. Mwishowe akaona ajilie ngogwe alizokuwa kazianika Juanita kwa ajili ya mbegu msimu ujao kazimeza ngogwe zikamvuruga tumbo kiasi . Mkeka ukasukwa upya tunasubiri.
 
Magufuli alikuwa-
1. Alizuia shughuli halali za vyama vya siasa hususan mikutano na maandamano
2. Alikuwa ameitisha Mahakama iamue kwa kuipendelea Serikali
3. Aliliteka Bunge likawa kama kitengo cha Ikulu
4. Alinyang'anya fedha za wafanyabiashara na kuwatupa rumande bila makosa
5. Alikuwa MWONGO sana kwa kuwa alijuwa Watanzania ni wajinga. Alidai anajenga miradi kwa fedha za ndani kumbe anakopa kwenye mabenki ya nje
6. Alidhibiti uhuru wa maoni na kuvitisha kuvifungia vyombo huru vya habari ambavyo vingeripoti kinyume na matakwa yake
7. Aliiba uchaguzi wote wa 2020 na kutuachia wabunge aliowateua yeye
 
Nadhani urais ni mgumu sana. Huwezi kuwa rais bora kwa kutumia informal advisors. Nadhani wakwe akina Mchengerwa inawezekana ndiyo washauri wake wakuu. Ninaamini taasisi ya urais haiweze kumpotosha bali hao wapembeni. Arudi kwao wenye taasisi watajua namna ya kuweka mambo sawa, hajachelewa
 
Doooh...hoi bin taabani....kweli asali ni tamu sana.Watu wanaona wale tu hata kama hawatakiwi.,🤔
 

Mama mbona wasiwasi wake tu?

Alikuwa nayo nafasi ya kusimama katika haki na akaungwa mkono na walio wengi.

Nchimbi mbona anaongea lugha nzuri na anaeleweka? Kwani angeongea kama Nchimbi shida ilikuwa wapi?

Asingekubaliana na teka teka nani angekuwa na taabu naye?

Tatizo lake kulewa madaraka akisikia katiba mpya anaona urais wake 2025 unakuja kwenda na maji.

Laiti angejikita kwenye kujenga legacy yake kuliko 2025 mbona alikuwa na yote ya kupata?

Alipo sasa na ajiangalie asije akaanguka.

Kwani yaliisha je na yule mwamba aliyeambiwa mgombea shuruti awe mwanamke?
 
Cha maana ni kuacha kuwapa meno hawa watumishi wetu (wakiwa na meno kuna uwezekano wa kututafuna sisi maboss wao)

Taasisi ziwe na nguvu na Rais abaki kuwa ceremonial (kuhakikisha sheria na misingi ya haki pamoja na Dira ya taifa inafuatwa)...

Unless otherwise kila baada ya miaka mitano au kumi tutakuwa tunaelekea / tunapelekwa popote dereva anapotaka....

That said atlease bwana yule kulikuwa kuna vision fulani kwamba anataka kwenda pale as of now nadhani ni kama Jahazi linapelekwa na upepo...
 
Na aendelee kuua na kuteka watu kama bwana yule.
 
Ukisha kula ukavimbiwa unasahau kuna kunawa mikono na mara unapitiwa na usingizi mzito nakukoroma....
 
Tatizo karibu wote tunamuangalia rais kama ugonjwa, wakati rais ni dalili ya ugonjwa tu.

Ugonjwa upo katika jamii yote.

Mtoto anavyolelewa tu ni tatizo, sasa unategemea huyu mtoto akija kuwa rais ataongoza nchi vizuri?
Shida kubwa kwetu Watanzania ni kutoa lawama kwa jambo fulani,bila kufanya tafiti ya kina juu ya chanzo chake ni kipi?

Kuna rafiki yangu mmoja aliwahi niambia "utafanyaje siku ukigundua kwamba wewe ndo chanzo Cha tatizo"Watanzania tujitafakari,haya tuonayo kwa viongozi wetu ni zao letu wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…