EEEEEeeeeNNNnnnHEEEeee. 'The Monk', Bhwanah!Ndio maana Kuna wakati unawaza mambo yasiwezekana mfano Bora nchi wakabidhiwe consultants waendeshe. Tuwe na Rais kama mfalme Kwa maana ya Alana tu ya mamlaka ya taifa.
Hao jamaa wakamate Kila kitu. Kuanzia kukusanya Kodi, kusimamia uendeshaji wa miradi na mambo yote Kwa mujibu wa dira na malengo ya taifa.
Kurekebisha hili tatizo kwenye jamii itatuchukua muda sana, na hasa Kwa vile hatuanfalii chanzo Cha tatizo, tutaangalia matokeo ya tatizo.
Nadharia hiyo ya 'consultants' nilisha igusia sana humu kutokana na viongozi wetu hawa kudhani kuwa sisi wenyewe (waTanzania) hatuna uwezo wa kufanya lolote la maana katika maendeleo ya nchi yetu na kwa hiyo wao wakiamini kila jambo wapewe watu toka nje kuja kuliendesha. Huwa nashindwa kujua kwa nini viongozi hao hao wao hawajijumuishi katika hao waTanzania wengine; kwa maana kwamba nafasi zao huwa hawafikirii kamwe zitafutiwe watu toka nje kuja kuzisimamia.
Swala la 'consultants' sina tatizo nalo kabisa, nisilo kubaliana nalo ni fikra za kudhani waTanzania hawawezi kufanya vizuri katika nyanja hizo hizo tunazo watafuta 'consultants'. Mbaya zaidi ni hapo hawa viongozi wetu wanapofikiri kuwa hata uwezo wa kujifunza mambo tusiyo yajuwa kwa sasa, sisi waTanzania hatuna. Fikra za namna hii zinaua moyo wa taifa, na kulifanya liwe tegemezi miaka yote.
Kwa maoni yangu, kinacho takiwa kwa nchi yoyote , ni kwa wananchi wake kujiamini kwamba wanaweza kufanya kinachoweza kufanywa na binaadam mwingine yeyote katika kuleta maendeleo yetu. Viongozi wanatakiwa wawe mstari wa mbele kusukuma moyo huo wa uthubutu wa wananchi, siyo kuwakatisha tamaa.
Tatizo ni moja tu. Kukosekana kwa viongozi wenye uamini huo na kuweka taratibu za kusimamia juhudi hizo ziwe na ufanisi.