Wazo Muflisi: Alijaribu Kujitenga lakini Anarudi Bila Tenga...

Wazo Muflisi: Alijaribu Kujitenga lakini Anarudi Bila Tenga...

Tatizo karibu wote tunamuangalia rais kama ugonjwa, wakati rais ni dalili ya ugonjwa tu.

Ugonjwa upo katika jamii yote.

Mtoto anavyolelewa tu ni tatizo, sasa unategemea huyu mtoto akija kuwa rais ataongoza nchi vizuri?

Kwa mara ya kwanza JF ninasoma maneno ambayo nami nimekuwa nikiwaeleza watu mara nyingi...

Kwamba matatizo yeyote ya kiutendaji, mienendo au tabia tunazoziona kwa viongozi wetu hizo ndio tabia tulizonazo Watanzania...

Tunahangaika kumkunja samaki aliyekwishakuwa mkavu...
 
Tatizo siyo bwana yule na wala siyo bibi huyu, bali tatizo ni kwamba Katiba tuliyonayo ni mbovu na Sheria zilizopo ni kandamizi, hazifai.
Vijana kama hawa ni wakati sahihi wajitokeze vinginevyo hakuna namna maana katiba haitabadilika kuwa ya wananchi wala hakuna kiongozi atakayekuwepo kwa kuchaguliwa kwa kura halali.
 
Nafikiri Kumfananisha Nchimbi na Rais wa Nchi ni kosa kimkakati.

Mkuu ninadhani kumrejea Nchimbi ni katika kuonyesha nia njema iliyopo pande zote kuwa tunajenga nyumba moja.

Kwamba hilo linaweza kumgharimu Nchimbi? Huo mbona utakuwa ni udhaifu nwingine Tena uliopitiliza?

Ni uungwana kuwatuza wanaofanya vyema na kuwaeleza wenye kukosea ili ikiwezekana nao wafanye vyema.

Kwa jana Rais ametuma Meseji kubwa kadhaa ambazo ni muhimu kuziangazia zaidi.

1. Anaamini 4R zipo kwa ajili ya kuliponya taifa.

Mkuu laiti angetambua hii nchi si yake wala ya chama chake peke yake tungepiga hatua kubwa sana katika nyanja zote.

Fikiria angekuwa na tafsiri halisi ya hizo anazoita 4R unadhani kungekuwa na manung'uniko wapi au hizi tekaji?

Kwamba kuna manung'uniko na watu wanatekwa wewe huoni hizo 4R zake ni geresha tu?

Bahati mbaya ni kuwa hiyo juzi kaipoteza nafasi yake muhimu mno ya kuliunganisha taifa.

2. Anaumizwa na yanayoendelea nchini na ameagiza uchunguzi ufanyike, alitudokeza kuwa uchunguzi uko katika hatua nzuri.

Angekuwa anaumizwa na yanayoendelea unadhani angesema kifo ni kifo tu?

Unadhani asingeona umuhimu wa uchunguzi huru?

Unadhani asingeona wenye kuchukizwa na ya namna hii si wenzake?

3. Amechukizwa na mabalozi kuingilia mambo ya ndani yanchi. Amekuwa wazi waseme lakini waimuelekeze nini cha kufanya.

Kwamba amechukizwa na hisia na pia yakiwamo maoni yao?

Kwanini haoni mabalozi kuyaongelea ya kutekana ni katika kutambua machungu wanayoyapitia wahanga na familia zao?

Kwamba watu wanatekwa hudhani hilo litamfikirisha na kumchukiza kila mtu, isipokuwa watekanyara au washirika wao?

Kwanini kama naye anakasirishwa na tekaji hizi asione huku ni kuungwa mkono na hata akaonw ni fursa kuweza kupata usaidizi wa kiufundi au kimawazo kuelekea kwenye ufumbuzi wa kudumu?

4. Ameangazia vyama vya siasa kutaka kuleta taharuki na fujo (kwa kile alichotueleza kuwa kulikuwa na kikao cha ngulelo) na kusisitiza yeyote atakayefanya hivyo atashughulikiwa. hili wapinzani wake hawakulitarajia na hawakulipenda.

Iweje kuangazia ya vyama vya siasa kuwa ni kutaka kuleta taharuki isiyojulikana badala ya kuiangazia taharuki ya watekaji ambayo tayari ipo?

Kwani yeye amekuwa nabii ndugu?

Kwani hata hizi lugha za jumla jumla zimewahi kutoa majibu yenye tija wapi?

Hizi si ndiyo zinazoitwa maneno matupu yasiyovunja mifupa?

5. ameonesha wazi maandamano yanayopangwa tarehe 23 Septemba hayataisha vizuri endapo yakifanyika. (pale aliposema nchi italindwa kwa gharama yeyote).

Sep 23 ni kupaza sauti kudai uchunguzi huru.

Kwanini awaye yote adhani hayataisha salama?

Kwani yeye asingependa kuwajua wabaya wetu?

Kama mtuhumiwa anaweza kuwa yeyote vipi baadhi ya watuhumiwa wakawa ndiyo wanaofanya uchunguzi?

Kwa mtazamo wangu, kama haya ndiyo anayoyawaza basi aendelee kusimama imara. Rais hatakiwi kuwa neutral. Nadhani amewasurprise wapinzani wake kwani walitegemea atakuwa mkimya au kuongea kwa kile wanachokiita wao 'busara". sasa ni wasaa wa kuona nini kitafata.

Neutral itakuwa ni kitu gani?

Hudhani sote akiwamo yeye tulipaswa kusimama na haki tu.

Kwamba ame wa surprise watu kwa kutokuchagua kusimama na haki, wewe unaona kuna cha kumpongeza hapo?

Kwa mawazo yàngu:

Wewe kama yeye suala la utekaji wala haliwafikirishi kwa lolote.

Kwamba kwenu siyo kuwa hilo ni none issue?
 
Nilikuwa wa kwanza kusema Mama arudishe siasa za kuwashughulikia Wapinzani bila kuingiza mambo hayo kwenye uchumi.

Mifano Iko Mingi sana kuanzia Uganda,Rwanda,Egypt,China nk.

Bwana wako yule alikuwa haelewi yeye akaleta chuki zake Hadi kwenye Uchumi,Hali ikawa mbaya wawekezaji wakakimbia, account zikaanza kufungwa ,watu kubambikiwa Kodi Kwa sababu pesa imepungua na Biashara kukaba kiasi kwamba vilio vya vyuma kukaza vilitamalaki.

Rais awashughulikie Wanasiasa uchwara na vibaraka wote ila silete siasa za ujamaa hapa.

Mwisho kama unaembeba habebeki unategemea uendelee kumbeba? Una mdamp tuu unasonga mbele mwenyewe.
Wawekezaji wapi walikimbia na sasa wamerudi? Hebu wataje hapa
 
Hayo yote yalikuwa yanatabirika kirahisi sana na baadhi yetu tuliyatabiri kwa namna tofauti tofauti.

Ila, tulipojaribu kuwaambia, tukaishia kuchekwa na kuitwa ‘Sukuma Gang’ na majina mengineyo.

Wengine walitubeza kwamba hatuamini kilichotokea na wala hatuamini kinachoendelea na kwamba tuko kwenye ‘denial’ flani hivi.

Wengine wakawa hawachoki na hawaachi kutukumbusha kwamba Ngosha keshakufa na harudi tena.

Wapo baadhi yao, wachache kwa idadi, walioenda mbali zaidi na kusema kwamba tayari Ngosha huko aliko keshaoza na kuoza.

Dah! Basi tena….tukawa hatuna la kusema zaidi tu ya kuwakumbusha kwamba ni muda tu ndo utaoongea.

Wanasemaga hayawi hayawi na yame……

Sasa sijui imekuwaje tena maana vilio vimeongezeka na Ngosha hayupo na wala hatorudi tena.

Ushauri mdogo tu….maishani mtu ukitumia tajiriba [experience], busara za kawaida [common sense], kuyaangalia na kuyatathmini mambo kwa kutumia akili na uhalisia na si hisia, kwa kiasi kikubwa utajikuta unafanya maamuzi mengi yaliyo sahihi kuliko yale yasiyo sahihi.
Duh umenikumbusha sukuma gang sijui ule upepo uliishia wapi, bongo vichwa maji sana 😅😅
 
Tanzania hakuna siasa za Vyama vingi ni maigizo.
Correct observation. Basi mkuu usisumbuke sana na wapinzani. Comment unazotoa kuhusu wapinzani huwa hazina sense hata kidogo. Bora ubakie na propaganda za maendeleo tu. Hizo zinakufaa sana.

Hata Mkapa alishawahi kukiri kuwa hana imani kabisa na dhana ya upinzani Afrika ingawa kimataifa alikuwa anahangaika kutambulika kama "Statesman". Akaaminiwa jukumu la kuwa msuluhishi wa migogoro ya nchi jirani kati ya vyama tawala na vya upinzani!

Hii ndio ajabu ya viongozi wa CCM. Hawana ujasiri wa kuwa kama Museveni, Mugabe au Kagame. Wanataka kupendwa na "mabeberu" huku wanatenda kama Kim Jong Un, Mobutu, na Idi Amin. JK naye anazunguka Afrika kama msimamizi na mshauri wa chaguzi za vyama vingi na demokrasia! Kuna wakati nilikutana na jamaa wa Cameroon, Yaounde, wakawa wanaongea kwa hisia na machozi jinsi JK alivyo "humble" na kuhuzunika jinsi walivyo na bahati mbaya kutopata Rais wa aina ile! Wao wana "mzuka" wa Paul Biya hadi leo. Nilitabasamu na kuwaza hawa jamaa they know not what they are wishing for.

Mshauri Rais wako abadili sheria kurejesha mfumo wa chama kimoja cha siasa ili aepukane na hao "makhuluku tabu" wake. Bila hivyo atabakia nao hadi wamuangamize. Binadamu hawezi kuwa kama sanamu. Binadamu ni dynamic. Kutegemea Watanzania watatulia tuli huku unawanyoa kama Jomo Kenyatta alivyomuambia Nyerere haitawezekana tena. Generations change.
 
Nilikuwa wa kwanza kusema Mama arudishe siasa za kuwashughulikia Wapinzani bila kuingiza mambo hayo kwenye uchumi.

Mifano Iko Mingi sana kuanzia Uganda,Rwanda,Egypt,China nk.

Bwana wako yule alikuwa haelewi yeye akaleta chuki zake Hadi kwenye Uchumi,Hali ikawa mbaya wawekezaji wakakimbia, account zikaanza kufungwa ,watu kubambikiwa Kodi Kwa sababu pesa imepungua na Biashara kukaba kiasi kwamba vilio vya vyuma kukaza vilitamalaki.

Rais awashughulikie Wanasiasa uchwara na vibaraka wote ila silete siasa za ujamaa hapa.

Mwisho kama unaembeba habebeki unategemea uendelee kumbeba? Una mdamp tuu unasonga mbele mwenyewe.
kipindi cha magufuli hali ilikua nzuri kulinganisha na sasa,
 
Tatizo karibu wote tunamuangalia rais kama ugonjwa, wakati rais ni dalili ya ugonjwa tu.

Ugonjwa upo katika jamii yote.

Mtoto anavyolelewa tu ni tatizo, sasa unategemea huyu mtoto akija kuwa rais ataongoza nchi vizuri?
Nimesema hili zaidi ya mara Elfu,Elimu ya Tanzania inatengeneza wapiga kura wajinga,watoto wajinga,wazazi wajinga,viongozi wajinga...walimu wajinga,future itakuaje bright??hata rais awe smart kiasi gani,waliomzunguka??anao watawala??..
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Rais Samia alitaka kupendwa. Rais Samia alitaka kukubalika. Rais Samia alitaka kuoenakana yeye siyo kama yule. Baada ya kuapishwa kufuatia maombolezo ya kifo cha Bw. Yule mara moja watu walianza kusema sasa "wanashusha pumzi". Wapo watu walisherehekea na wakajua kuwa sasa angalau wanaweza kuhema. Hali ya kuwa roho juu kisa bwana yule asiyelala na mwenye kukesha na mafaili hadi chumbani ikashuka. Watu wakaanza kutembea na kuchekeana bila kuogopana.

Upinzani ulishukuru zaidi kwana Bw. Yule aliwabana kweli kweli. Lakini upinzani dhidi yake ulikuwa wazi kabisa na kamili; mgogoro wake na upinzani na dhana ya demokrasia watu waliijua kabla hajaingia madarakani. Hakuwahi kuwa na ahadi za kidemokrasia hata kama aliziimba kidogo. Watu walijua kuwa yeye alichotaka ni "kazi" watu wakakutane kwenye kampeni. Hakutaka kuendekeza siasa za kushindana; walipojaribu kujitutumua vyombo vya dola vya nchi hii vikaingia kumfanya Bw. Yule atawale bila kuzingwazingwa.

Wale wajomba zetu walipojaribu kusema hakuwapepesea macho; na aliwaonesha kweli yeye hawajali kivile pale alipokataa kabisa kwenda kubeba tenga lake kulipeleka huko waliko kuwaomba. Kama aliwaomba aliwataka wao waje kwake ndio awaombe. Tena waje na matenga yao kwanza! Alikataa sana ile hali ya "kujidhalilisha". Sasa Rais Samia alipoingia madarakani siyo tu alitaka kupendwa na watendaji serikali ambao walikuwa roho juu hata kwenda Dubai ilikuwa Mbinde bali alitaka kupendwa na wajomba zetu huko nchi za Magharibi. Rais Samia katika kupendwa huko akaamua kujitenga kimaono na kiutendaji na Bw. Yule.

Bw. Yule alikuwa anafokafoka; mama hakasema yeye hafoki. Huku kijijini Mama akaanza kujulikana kwa "Mama Nahaya Mkayaangilie". Mama hakutaka watu waondoke wamenuna; alijua kuwabembeleza na hata akiwatimua kazi hakutaka wajue ni yeye amechukizwa. Mama akakwepa kabisa kutimua watendaji wabovu papo kwa papo japo anafanya hivyo kimya kimya. Niliandika mahali kuwa Rais Samia ni Simba Mwendapole.

Sasa haya ya juzi ndio yamefunua kuwa jani halitui mbali ya mti na kuwa atapikaye hutapika mbele yake. Mama alijaribu kuwapendeza wapinzani, amejaribu kuwatetea watu wabovu na kwa namna alibariki ulaji wa "urefu wa kamba zao" kumbe wajanja wakala na kamba zenyewe! Mama ambaye alisifiwa kuwa yeye hafokei watu juzi kwenye sherehe za Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mama akajikuta amegeuka kama Bw. Yule.

Yaani, kama hotuba ile ingetolewa kwa sauti ya Bw. Yule kuna watu wangebeba mashada ya maua na kumwambia mama kumbe umerudi! Sasa alivyojitenga vyote vile, na juhudi zote za 4R zimekuwa sasa ni juhudi za 4K - Kugeukana, Kukimbizana, Kutoleana Macho na Kupigana Mikwara! Alijaribu kujitenga na habari za Bw. Yule; lakini sasa karudi tena karudi na naona na tenga analipiga mkwara. Tunakoelekea jina la Bw. Yule litaanza kuimbwa mbele zake kama alama za kumuunga mkono.
Hawezi kufikia Bwana yule,Bwana yule alikuwa simba wa yuda akiunguruma, swala wote wanakimbia.
 
Umemsikiliza Jenerali Ulimwengu?
Rais anapokosea kosa lake ni kubwa kwa sababu ya nafasi yake.
Naelewa yote hayo, nimeandika mpaka kanuni ya Noblesse Oblige, to whom much is given, much shall be required.

Ukiwaomba mamilioni ya watu uwaongoze, obviously unaomba dhamana kubwa, na ukikosea, lawama zake ni kubwa.

Simtetei rais, rais ana wajibu mkubwa, rais ana wajibu wa mwisho. Rais ana lawama kubwa kabisa na za mwisho kabisa.

Naelezea tatizo lilivyo kubwa kushinda kumuangalia rais tu.

Kwa mfano, kama tuna tatizo katika mfumo unaotupa viongozi, chujio hili la kupitia familia, shule, vyuo, ajira, uongozi serikalini, bunge, uwaziri, urais sio tu lina matobo yanayopitisha watu wabovu, bali pia chujio lenyewe lina uchafu umaowachafua mpaka waliokuwa wasafi, hapo tutategemea vipi kupata kiongozi mzuri?

Kama familia hazijui na hazijali malezi bora, walimu hawafundishi vizuri, ajira ni kwa kujuana na watu hawana nidhamu kazini, siasa zimejaa kutukanana, visasi na rushwa, na anayeweza kufanya ushenzi zaidi ndiye anayeweza kupanda juu zaidi, hapo tutategemea vipi tuwe na rais msafi mwenye weledi?

Katika mfumo huu, una haki ya kumlaumu rais, maana yeye ndiye mwenye dhamana kubwa, lakini, hata ukimtoa huyo rais ukamuweka mwingine, utampata msafi na mzuri?

Huoni kwamba kuna tatizo katika jamii nzima hapo?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Rais Samia alitaka kupendwa. Rais Samia alitaka kukubalika. Rais Samia alitaka kuoenakana yeye siyo kama yule. Baada ya kuapishwa kufuatia maombolezo ya kifo cha Bw. Yule mara moja watu walianza kusema sasa "wanashusha pumzi". Wapo watu walisherehekea na wakajua kuwa sasa angalau wanaweza kuhema. Hali ya kuwa roho juu kisa bwana yule asiyelala na mwenye kukesha na mafaili hadi chumbani ikashuka. Watu wakaanza kutembea na kuchekeana bila kuogopana.

Upinzani ulishukuru zaidi kwana Bw. Yule aliwabana kweli kweli. Lakini upinzani dhidi yake ulikuwa wazi kabisa na kamili; mgogoro wake na upinzani na dhana ya demokrasia watu waliijua kabla hajaingia madarakani. Hakuwahi kuwa na ahadi za kidemokrasia hata kama aliziimba kidogo. Watu walijua kuwa yeye alichotaka ni "kazi" watu wakakutane kwenye kampeni. Hakutaka kuendekeza siasa za kushindana; walipojaribu kujitutumua vyombo vya dola vya nchi hii vikaingia kumfanya Bw. Yule atawale bila kuzingwazingwa.

Wale wajomba zetu walipojaribu kusema hakuwapepesea macho; na aliwaonesha kweli yeye hawajali kivile pale alipokataa kabisa kwenda kubeba tenga lake kulipeleka huko waliko kuwaomba. Kama aliwaomba aliwataka wao waje kwake ndio awaombe. Tena waje na matenga yao kwanza! Alikataa sana ile hali ya "kujidhalilisha". Sasa Rais Samia alipoingia madarakani siyo tu alitaka kupendwa na watendaji serikali ambao walikuwa roho juu hata kwenda Dubai ilikuwa Mbinde bali alitaka kupendwa na wajomba zetu huko nchi za Magharibi. Rais Samia katika kupendwa huko akaamua kujitenga kimaono na kiutendaji na Bw. Yule.

Bw. Yule alikuwa anafokafoka; mama hakasema yeye hafoki. Huku kijijini Mama akaanza kujulikana kwa "Mama Nahaya Mkayaangilie". Mama hakutaka watu waondoke wamenuna; alijua kuwabembeleza na hata akiwatimua kazi hakutaka wajue ni yeye amechukizwa. Mama akakwepa kabisa kutimua watendaji wabovu papo kwa papo japo anafanya hivyo kimya kimya. Niliandika mahali kuwa Rais Samia ni Simba Mwendapole.

Sasa haya ya juzi ndio yamefunua kuwa jani halitui mbali ya mti na kuwa atapikaye hutapika mbele yake. Mama alijaribu kuwapendeza wapinzani, amejaribu kuwatetea watu wabovu na kwa namna alibariki ulaji wa "urefu wa kamba zao" kumbe wajanja wakala na kamba zenyewe! Mama ambaye alisifiwa kuwa yeye hafokei watu juzi kwenye sherehe za Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mama akajikuta amegeuka kama Bw. Yule.

Yaani, kama hotuba ile ingetolewa kwa sauti ya Bw. Yule kuna watu wangebeba mashada ya maua na kumwambia mama kumbe umerudi! Sasa alivyojitenga vyote vile, na juhudi zote za 4R zimekuwa sasa ni juhudi za 4K - Kugeukana, Kukimbizana, Kutoleana Macho na Kupigana Mikwara! Alijaribu kujitenga na habari za Bw. Yule; lakini sasa karudi tena karudi na naona na tenga analipiga mkwara. Tunakoelekea jina la Bw. Yule litaanza kuimbwa mbele zake kama alama za kumuunga mkono.
Ogopa Sana, mtu mwenye akili ndogo, low self esteem, asiyejiamini,
Nilikuwa na boss wangu, Engineer, ana pesa nyingi Sana, ila Mambo ya ufundi hayupo vzr, sasa tukiwa kwenye mazungumzo, nikimbishia, anakasirika hatari, akanijengea bifu balaa, sasa, Ili hoja zake zikubaliwe, aka wa anatumia cheo,vitisho, maturity, kejeli, lugha za hovyo,
Mungu alimpa pesa, lakini akamnyima physical strength na body physique, ana ka mwili kadogo, na sauti ndogo, sasa alinichukia kwanza, ni booming sound, Gym body, akawa ana kuwa intimidated, hapo karata yake, ni vitisho vya kufukuza kazi, na matusi,hatari Sana,
Sasa samia anajua watu wanamuona kichwa panzi, mama mmoja kilaza, sasa anatumia nguvu kuumiza ili watu wamuogope,
Ila ajue tu, hata makaburu wa South, walitisha, Leo wapo wapi!
 
Kwa mara ya kwanza JF ninasoma maneno ambayo nami nimekuwa nikiwaeleza watu mara nyingi...

Kwamba matatizo yeyote ya kiutendaji, mienendo au tabia tunazoziona kwa viongozi wetu hizo ndio tabia tulizonazo Watanzania...

Tunahangaika kumkunja samaki aliyekwishakuwa mkavu...
Exactly mkuu.

Watu wanapenda quick fix solutions, masuluhisho ya mkato mkato, ambayo yanapenda sana kuangalia nani alaumiwe, kuangalia mtu, badala ya kuangalia tatizo kwa kina katika ngazi ya jamii nzima.

Kuangalia tatizo katika ngazi ya jamii nzima si kitu ambacho watu wengi wanapenda, kwa sababu hapo utaliona tatizo kwa ukubwa wake na kazi ilivyo nzito, na watu hawapendi kazi nzito, wanapenda quick fixes.

Hatujaangalia malezi ya watoto, hatujaangalia elimu shuleni, hatujaangalia nidhamu ya kazi kazini, hatujaangalia uthabiti wa chaguzi na siasa zetu, hatujaangalia vetting systems katika national politics zetu. Sehemu zote hizo nilizozitaja zina uozo mkubwa.

Sasa tunategemea vioi tuwe na rais mzuri sana kama hiyo mifumo yote aliyopitia ina matatizo?

Mfano. Rais kalelewa kwenye familia iliyompa childhood trauma, kazoea kushindana shindana kwa mipasho na watoto wa mke wa kwanza katika familia yao, akija kuwa rais anaendeleza saikolojia ile ile, mtu yeyote anayempinga kifalsafa na kisiasa tu anamkumbusha wale watoto wa mke wa kwanza na childhood trauma yake. Badala ya kutumia akili kukaa pamoja na wapinzani, analeta utawala wa kujimwambafy kwa mabavu.

Tumeona hiki kwa Magufuli na Samia. It is a feature of our culture.

Ni kama hawa marais wanasema "Sisi tumebwengwa sana tulivyokuwa watoto, tumepigwa sana. Sasa tumekuwa marais ni zamu yetu na sisi kupiga mtake msitake".

Rais gani anasema "Kifo ni kifo tu?"

Haya kifo ni kifo tu, tumuue na yeye? Si kifo ni kifo tu?

Huyu rais ukimsikiliza unaona katiba hana uwezo.

My point is, sawa, rais anastahili lawama.

Lakini je, yeye ndiyo chanzo cha matatizo yetu? Au haya ni matatizo ya kimfumo na ndiyo maana hata baada ya Magufuli kufariki na sisi kubadiki rais matatizo yaleyale yanajirudia tu?
 
Ogopa Sana, mtu mwenye akili ndogo, low self esteem, asiyejiamini,
Nilikuwa na boss wangu, Engineer, ana pesa nyingi Sana, ila Mambo ya ufundi hayupo vzr, sasa tukiwa kwenye mazungumzo, nikimbishia, anakasirika hatari, akanijengea bifu balaa, sasa, Ili hoja zake zikubaliwe, aka wa anatumia cheo,vitisho, maturity, kejeli, lugha za hovyo,
Mungu alimpa pesa, lakini akamnyima physical strength na body physique, ana ka mwili kadogo, na sauti ndogo, sasa alinichukia kwanza, ni booming sound, Gym body, akawa ana kuwa intimidated, hapo karata yake, ni vitisho vya kufukuza kazi, na matusi,hatari Sana,
Sasa samia anajua watu wanamuona kichwa panzi, mama mmoja kilaza, sasa anatumia nguvu kuumiza ili watu wamuogope,
Ila ajue tu, hata makaburu wa South, walitisha, Leo wapo wapi!
Tatizo Tanzania watu smart hawapandi ngazi, labda kwa bahati tu, kwa sababu ili upande ngazi unatakiwa kuwa chawa na watu smart hawawezi uchawa. Wajinga ndio wanaweza uchawa na wanapanda ngazi.

Na inawezekana ndiyo maana mtu kama huyo bosi wako ukimbishia anakasirika sana, kwa sababu yeye kashazoea kuwa chawa na kupanda ngazi, anategemea na wewe uliye chini yake uwe chawa wake, ukimbishia anaona umemnyima haki yake ya kikatiba ya kukufanya uwe chawa wake.

Tusipolimaliza tatizo hili na kuweka meritocracy matatizo mengi sana tutashindwa kuyamaliza.
 
Sifa za kuwa Kiongozi ni zipi huko kwenu ambazo ziko tuned?

Kwamba sijui ujamaa vs unepari si upinge hoja yangu Kwa hoja badala ya kujiswmesha kwa majigambo kama mabondia wanaojiandaa Kwa pambano.

Nasisitiza hakuna kuingiza ujamaa kwenye uchumi,hizo ziishie kwenye siasa za majukwaani na leadership style,mifano nimeshaiweka.
Najuwa, elimu ya kukariri haikupi uwezo wa kutambua kwamba hakuna hata serikali moja duniani inayoweza kutawala bila ya siasa kuunganika na uchumi. Serikali zipo kutengeneza sera zinazo endesha maisha ya watu, ikiwa ni pamoja na uchumi. Kiufupi ni kwamba wewe ni hodari tu wa kuokota hizi habari toka kwenye magazeti na vyanzo vingine, zaidi ya hapo huna uelewa mzuri na yanayozungumziwa katika taarifa hizo unazo weka humu.
 
Back
Top Bottom