Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Anasema sasa sio 4R tena bali ni 4K!Hilo kako kweli ni wazo muflis, kabisa tena.
Kazi ya Mungu haina makosa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anasema sasa sio 4R tena bali ni 4K!Hilo kako kweli ni wazo muflis, kabisa tena.
Kazi ya Mungu haina makosa.
Nani "anasema"?Anasema sasa sio 4R tena bali ni 4K!
Ni kweli lkn angalau yeye anafunika mvi. Wengine hata mvi za ndani watoto wanaziona mitaaniKufunika kichwa sio uchamungu, anaficha mvi tu. Uchamungu ni vitendo zaidi
Mzee nimefurahi kukuona upo kama fulani...heshima kwakoAnamcha Mungu gani?
IO...heshima yakoNi uchumi upi huo unaongea? Lete data. Ukitaka kuengelea inflation imezidi, unemployment ni zaidi ya 40%, ukiongelea wawekezaji sioni mwekezaji gani huyo wa maana toa reference. Impact ya economic growth ya sasa hivi na kukua kwa GDP kama kutatokea ni kutokana na infrastructure investment zile za Bwawa ambalo litatoa impact kubwa, meli zilinunuliwa, ndege zilinunuliwa na viwanja vya ndege vilijengwa, SGR, Makao makuu nk. Huyu kaleta nini kipya? Kukodisha Bandari kwa DP world na kuwandoa wamasai mbugani ndiyo investment kubwa?
Mungu yupi?Tofauti na yule, huyu mcha Mungu
Siku hizi sisikii neno la wewe ni Sukuma gang 😆😁😁😂wote Sasahivi tunaimba wimbo mmoja, Samia shikilia hapo hapo mpaka 2025😂😂😁.Na. M. M. Mwanakijiji
Rais Samia alitaka kupendwa. Rais Samia alitaka kukubalika. Rais Samia alitaka kuoenakana yeye siyo kama yule. Baada ya kuapishwa kufuatia maombolezo ya kifo cha Bw. Yule mara moja watu walianza kusema sasa "wanashusha pumzi". Wapo watu walisherehekea na wakajua kuwa sasa angalau wanaweza kuhema. Hali ya kuwa roho juu kisa bwana yule asiyelala na mwenye kukesha na mafaili hadi chumbani ikashuka. Watu wakaanza kutembea na kuchekeana bila kuogopana.
Upinzani ulishukuru zaidi kwana Bw. Yule aliwabana kweli kweli. Lakini upinzani dhidi yake ulikuwa wazi kabisa na kamili; mgogoro wake na upinzani na dhana ya demokrasia watu waliijua kabla hajaingia madarakani. Hakuwahi kuwa na ahadi za kidemokrasia hata kama aliziimba kidogo. Watu walijua kuwa yeye alichotaka ni "kazi" watu wakakutane kwenye kampeni. Hakutaka kuendekeza siasa za kushindana; walipojaribu kujitutumua vyombo vya dola vya nchi hii vikaingia kumfanya Bw. Yule atawale bila kuzingwazingwa.
Wale wajomba zetu walipojaribu kusema hakuwapepesea macho; na aliwaonesha kweli yeye hawajali kivile pale alipokataa kabisa kwenda kubeba tenga lake kulipeleka huko waliko kuwaomba. Kama aliwaomba aliwataka wao waje kwake ndio awaombe. Tena waje na matenga yao kwanza! Alikataa sana ile hali ya "kujidhalilisha". Sasa Rais Samia alipoingia madarakani siyo tu alitaka kupendwa na watendaji serikali ambao walikuwa roho juu hata kwenda Dubai ilikuwa Mbinde bali alitaka kupendwa na wajomba zetu huko nchi za Magharibi. Rais Samia katika kupendwa huko akaamua kujitenga kimaono na kiutendaji na Bw. Yule.
Bw. Yule alikuwa anafokafoka; mama hakasema yeye hafoki. Huku kijijini Mama akaanza kujulikana kwa "Mama Nahaya Mkayaangilie". Mama hakutaka watu waondoke wamenuna; alijua kuwabembeleza na hata akiwatimua kazi hakutaka wajue ni yeye amechukizwa. Mama akakwepa kabisa kutimua watendaji wabovu papo kwa papo japo anafanya hivyo kimya kimya. Niliandika mahali kuwa Rais Samia ni Simba Mwendapole.
Sasa haya ya juzi ndio yamefunua kuwa jani halitui mbali ya mti na kuwa atapikaye hutapika mbele yake. Mama alijaribu kuwapendeza wapinzani, amejaribu kuwatetea watu wabovu na kwa namna alibariki ulaji wa "urefu wa kamba zao" kumbe wajanja wakala na kamba zenyewe! Mama ambaye alisifiwa kuwa yeye hafokei watu juzi kwenye sherehe za Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mama akajikuta amegeuka kama Bw. Yule.
Yaani, kama hotuba ile ingetolewa kwa sauti ya Bw. Yule kuna watu wangebeba mashada ya maua na kumwambia mama kumbe umerudi! Sasa alivyojitenga vyote vile, na juhudi zote za 4R zimekuwa sasa ni juhudi za 4K - Kugeukana, Kukimbizana, Kutoleana Macho na Kupigana Mikwara! Alijaribu kujitenga na habari za Bw. Yule; lakini sasa karudi tena karudi na naona na tenga analipiga mkwara. Tunakoelekea jina la Bw. Yule litaanza kuimbwa mbele zake kama alama za kumuunga mkono.
Hana uchamungu wowoteTofauti na yule, huyu mcha Mungu
Mungu yupi huyo??Tofauti na yule, huyu mcha Mungu
Mcha Mungu anaongea maneno kama hayo...!?Tofauti na yule, huyu mcha Mungu
Ninyanyue tu sampuli ya kipande hiki kuwasilisha andiko zima na kusema: Sikubaliani/Nakubaliana.Kutoleana Macho na Kupigana Mikwara! Alijaribu kujitenga na habari za Bw. Yule; lakini sasa karudi tena karudi na naona na tenga analipiga mkwara. Tunakoelekea jina la Bw. Yule litaanza kuimbwa mbele zake kama alama za kumuunga mkono.
Hana ucha Mungu wowoteTofauti na yule, huyu mcha Mungu
Naam! Mwanzo alitaka ushauri wa JK, lakini baadaye akawatosa watu wa JK na kuanza kufuata ushauri wa ChawaNinyanyue tu sampuli ya kipande hiki kuwasilisha andiko zima na kusema: Sikubaliani/Nakubaliana.
Samia hata siku moja hawezi; hata kwa kuigiza kama anavyojaribu sasa kuwa kama Magufuli kwa njia yoyote ile.
Hili ni kosa moja la mada nzima.
Samia, toka aingie madarakani, hajui afanye nini. Hana msimamo madhubuti anao uamini yeye kama yeye; matokeo yake ndiko huko kuyumbayumba unako kuona, hasa kupitia katika utenguzi na uteuzi wa karibu kila wiki
Samia, hakuna chochote kinacho mpa msukumo kuwaongoza waTanzania, mbali ya kudondokewa na tunda la mwembe chini ya mti wa mchongoma. Kitu pekee kinacho mpendezesha ni kuwa na hayo madaraka makubwa ambayo hakuyategemea. Kwa bahati mbaya sana, kadakwa na genge, hasa huko huko ndani ya CCM, linalo tumia nafasi yake hiyo sasa kufanya uchafu wanaotaka.
Samia sasa kaja kugundua kuwa nafasi yake ipo mashakani, kwa sababu kule kujipendesheza kwa wananchi uliko kuelezea kwa ukweli, kumeshindikana. Kwa hiyo nafasi kwake kwa kushinda uchaguzi kwa kura hakupo; kwa hiyo njia pekee iliyo baki ni kuhakikisha anarudi madarakani kwa nguvu.
Katunga sheria ya kuwapoteza na kuwaua watu ili uoga baina ya watu ienee. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sasa ni Tamisemi ndio watahakikisha watu wao ndio watakao hakikisha huko mitaani kura za bandia za Samia zinapatikana
Hata katika haya, hakuna mfanano wowote na Magufuli
Yapo mengi, ya kumtofautisha Samia na Magufuli lakini ngoja niachie hapa.
Huyu wako hata ungemfunga mgongoni kwako uwe unampa maelekezo unayodhani ni mazuri kwenu, bado nyote mtaanguka tu; kwa sababu akili zenu haziko 'tuned' kuwa viongozi.Nilikuwa wa kwanza kusema Mama arudishe siasa za kuwashughulikia Wapinzani bila kuingiza mambo hayo kwenye uchumi.
Mifano Iko Mingi sana kuanzia Uganda,Rwanda,Egypt,China nk.
Bwana wako yule alikuwa haelewi yeye akaleta chuki zake Hadi kwenye Uchumi,Hali ikawa mbaya wawekezaji wakakimbia, account zikaanza kufungwa ,watu kubambikiwa Kodi Kwa sababu pesa imepungua na Biashara kukaba kiasi kwamba vilio vya vyuma kukaza vilitamalaki.
Rais awashughulikie Wanasiasa uchwara na vibaraka wote ila silete siasa za ujamaa hapa.
Mwisho kama unaembeba habebeki unategemea uendelee kumbeba? Una mdamp tuu unasonga mbele mwenyewe.
Duh,Kujikosha kuwa yeye ni mama alikula matapishi matakatifu ya Bw. Yule lakini bahati mbaya yakawa magumu yakashindwa KUMENG'ENYEKA si kwa maji wala umeme simu zenyewe zikashindwa kupigika Mama shingoni akakabika mratibu mkuu akaona isiwe tabu akajitoa pembeni akakaa. Kijana aliyekuwa nje akarejea akiwa kibri mabega juu akagonga koromeo la mama mwisho matapishi matapikwa yakatapikwa kwa mara ya pili. Mwishowe akaona ajilie ngogwe alizokuwa kazianika Juanita kwa ajili ya mbegu msimu ujao kazimeza ngogwe zikamvuruga tumbo kiasi . Mkeka ukasukwa upya tunasubiri.
mafirauni ni mafirauni tu hawabebeki...sasa ngoja wapelekwe kama walivyozoeaNa. M. M. Mwanakijiji