Tatizo lenyewe ni lipi sasa. Taifa lenyewe linategemea 1 man show kusinamia kila kitu badala ya katiba.
Tunapenda shortcuts.
Matatizo ya jamii tunataka kuweka lawama kwa mtu mmoja tu, rais.
Ndiyo, naelewa kanunibya "Noblesse Oblige", aliyepewa talanta nyingi atadaiwa zaidi. Naelewa hili.
Lakini, kama nchi imeoza, huyo kiongozi mahiri tutampata wapi?
Ngazi ya kupandia kufika kwenye uongozi wa juu kabisa kitaifa kama urais, inakupitisha bungeni na kwenye uwaziri, ambako bila siasa za majitaka, bila rushwa, bila udini, ulaghai, ukabila, uchawa, huwezi kutoboa.
Sasa tunategemeaje rais aongoze kwa usafi na integrity ikiwa ngazi ya kumfikisha hapo kwenye urais imejaa uchafu?
Tunapenda sana shirtcuts, majawabu rahisi, ya muda mfupi, bika kufanya kazi ngumu ya kuangalia tumejikwaa wapi, si tumeangukia wapi tu.
Soma post namba 15 na 41 nimeelezea.