Wazoefu na wabobezi: Nina akiba ya Tsh. Milioni 50 nianze na kipi maishani?

Wazoefu na wabobezi: Nina akiba ya Tsh. Milioni 50 nianze na kipi maishani?

Sijajua elimu yako ni level gani ila mimi nakushauri weka UTT Mil 45 jipe miezi sita ya kuamua ufanye kama hutapata cha kufanya iache huko huko we utaendelea kula gawio lako la kila mwezi 400k + huku ukiendelea na harakati nyingine.

Nakuonya kuwa makini matapeli wapo wengi na wapo tayari kuwekeza muda wao kutekeleza azma yao. Nenda taratibu na makini.
 
Habarini za wakati huu ndugu zangu wapendwa wa Jf.

Ni hivi,
Kuna maeneo ya familia yameuzwa mahali na kila mwanafamilia amepata gawio la Mil.45.
Na kwa kuwa nilikuwa na akiba ya kama Mil.5 benki basi nikajumuisha na ile Mil.45 ikawa kama Mil.50.

Najua humu kuna watu wa kada mbalimbali
Wafanyabiashara,
Washauri wa kazi,
Wajenzi,
Wauza bidhaa mbalimbali,
Madalali,
Wasomi n.k

Sasa nimeleta hoja hii mezani kwenu ili mnishauri nianze na kipi katika hiyo pesa.
Kumbuka hapo
1. Sijajenga
2. Sina kiwanja
3. Sina biashara yoyote
4. Sijaolewa (wanasemaga mume ni asset)
5. Kazi yangu ni ya 'kijungujiko'
6. Umri wangu ni miaka 30 na dini yangu ni Mkristo Mkatoliki.

Please wale wa kusema niweke mkeka utoe Odd hapana.
Nahitaji kufanyia mambo ya maana tu.

Naombeni msaada kabla sijajua cha kufanya.
Asanteni
Ujitahidi sana kuwa makini na mwenye utulivuwa kutosha. Maana utazungukwa na madalali wa kila aina, ili tu waambulie chochote kitu kwenye huo mgao wako.
 
Na namba umeweka huoni aibu mdau...
Dunia Ni ya wachache na SI ya kila mtu Waoga,Wenye Aibu,Na watu Dhaifu Hawajawahi kuwa na Nafasi Duniani.

Kina chotofautisha Mtu na Mtu Mtaani Si vyeti,SI Umri Ni Akili,Uzoefu,sahihi Na maamuzi

Hakuna akili,Uzoefu Na Usahihi usio na Gharama,Na Hakuna mwenye Akili,Uzoefu Na Njia Sahihi anaesindikiza watu kwenye utajiri.
 
PELEKA 10M FIXED NMB BANK KWA MIEZI 3 FAIDA IPO APO KABLA SIJAKUELEZA IZO 40M...EN SIKIA UMRI WAKO USITEGEMEE SANA KUOLEWA SABABU YA PESA ULIONAYO FAMILIA ITASEMA UMEPATA PESA UMEKIMBILIA WANAUME CC PIA TUPO TU....CHA UMUHIMU USITAKE KUJENGA MJINI NENDA KIBAHA KWA MFIPA CHUO CHA MWALIMU NYERERE KULE KUNA VIWANJA 2.5M SEHEMU NZR SANA UNAPATA KIWANJA CHENYE MADINI YA KUJENGEA TAFUTA RAMANI YA CHUMBA NA SEBULE NA JIKO NDANI KABISA NAAMINI KWA 23.5 UTAKUA NA KAMJENGO KAKALI SANA KWA UWEZO WAKO XO HAPO UTAINGIA TOWN KUTAFUTA MCHONGO WA 5M NI KUBWA SANA KWA BIASHARA NDOGO NDOGO KAMA UWAKALA IVYO CC WENYE 30YEARS PLAN YETU NI HIYAPO.... AmKATRINA
 
Ushauri na matumizi huendana zaidi na rika
Sasa kwa rika langu nakushauri kwa kuwa uko single tafuta kiwanja Cha kawaida Cha ml 3-4
Jenga nyumba ndogo ila nzuri hasa 2 bedroom na jiko angalau iwe 30 hadi na decorations
Kiasi kinachobaki boresha biashara au ongeza biashara nyingine e.g vifaa vya simu na miamala
 
Tumsifu YESU KRISTO

Kama ni kweli naomba nikushauli kwa njia za BWANA wetu YESU KRISTO

1, Anza na sadaka mtumish kwenye hiyo hela yako chukua sh laki tano nunua sabuni za unga zitenganishe kama ifuatavyo zingine peleka hospital kwa wagonjwa zingine peleka gerezan kwa wafungwa
2, nunua taulo na nepi hizi zote peleka hospital Kuna wahitaji wengi sana
3,nunua sulual na mashati ya mtumba hivi vyote peleka gerezan Kuna wafungwa hawana nguo kabisa
4, nunua rozary na biblia hata mbili tu hizi nazo peleka kwa wafungwa hakika BWANA YESU KRISTO atakubaliki sana
5, chukua laki tano watafute masikin watano ambao wana biashara za chini sana kama wauza karanga na wauza mandazi jaribu kuwainua kwa kuwapa laki moja moja tu, hakika MUNGU hataacha kukubariki
6, kama uko dar es salaam jitaid uingie mafungo nenda st Joseph hata walau kwa mda wa siku tatu tu, ongea na MUNGU kwa mda huo huku ukimwekea mipango yako yote

Ukishamaliza hivyo BWANA YESU KRISTO hataacha kukuonesha nini cha kufanya na nina kuhahikishia utasonga mbele milele utafanikiwa kuanzia ndoa na biashara

Anza na BWANA Dada yangu, MUNGU MWENYEZI AKUBARIKI SANA , ukitaka namna ya kwenda kuwaona wafungwa na wagonjwa na kupeleka vitu vyao waweza niona ni dm tu usijal kabisa kuwa huru

ROHO wa MUNGU awe na wewe acha kutegemea ushauri wa wanadamu utaanguka dada yangu Anza na MUNGU kwanza

Asante
 
SIKIA NDUGU NAKUPA MUONGOZO TU KIDOGO UTAKUSAIDIA,

Cha Kwanza Wale Matajiri unawaona si kwasababu Wanatafuta Sana au wanaakili Sana kuliko wengine ila Ni watu wenye Uwezo wa kuitunza,kuizungusha,Na kuilinda hela kwa mda Mrefu Kama Huwezi kulinda hela na Kuizungusha hela yako,Utabaki TU kuwa Daraja la Pesa Kwenda kwa wengine,

Pili Kama Huna Roho Ngumu Una Huruma Sana,Huna maamuzi Magumu Biashara Huwezi Nenda kidimbwi hela yako ukale kitimoto.
maana Hatua na Huruma,Biashara na Huruma havikai Sehemu Moja.

Tatu Kama Huna mke/mme/Familia(Watoto Miaka 5+) ukimbilia kujenga Ni Uoga Wa maisha Na Hayatokuwa maamuzi Sahihi Kwako.

Nne Hakuna Hela ndogo kwenye mtaji,Na Hakuna Hela kubwa kwenye mtaji.
Maamuzi Sahihi ndio kitu muhimu yanaweza kukuongezea ulichonacho au kukipoteza ulichonacho.

Mwisho Hela Hakaagi kwa mtu asie na Akili,Sio Akili Za GPA😂
Akili za mtaani.
Habarini za wakati huu ndugu zangu wapendwa wa Jf.

Ni hivi,
Kuna maeneo ya familia yameuzwa mahali na kila mwanafamilia amepata gawio la Mil.45.
Na kwa kuwa nilikuwa na akiba ya kama Mil.5 benki basi nikajumuisha na ile Mil.45 ikawa kama Mil.50.

Najua humu kuna watu wa kada mbalimbali
Wafanyabiashara,
Washauri wa kazi,
Wajenzi,
Wauza bidhaa mbalimbali,
Madalali,
Wasomi n.k

Sasa nimeleta hoja hii mezani kwenu ili mnishauri nianze na kipi katika hiyo pesa.
Kumbuka hapo
1. Sijajenga
2. Sina kiwanja
3. Sina biashara yoyote
4. Sijaolewa (wanasemaga mume ni asset)
5. Kazi yangu ni ya 'kijungujiko'
6. Umri wangu ni miaka 30 na dini yangu ni Mkristo Mkatoliki.

Please wale wa kusema niweke mkeka utoe Odd hapana.
Nahitaji kufanyia mambo ya maana tu.

Naombeni msaada kabla sijajua cha kufanya.
Asanteni
 
Wakati unaendelea kutafakari cha kufanya, kwa sasa wekeza UTT wakupe 500k kila mwezi
UOGA NDIO UNAOFANYA WATU WENGI WAFE NA MAISHA YA KAWAIDA,

MIMI SJAWAHI KUWA MUUMINI WA MFUKO WA UTT NA FIXED ACCOUNT ZA BANK KUWANUFAISHA WAO,

MALA 100 NI HERI ALIENUNUA HISA ZA CRDB ANAUHAKIKA WA KUNAFAIKA VYEMA KWA ALICHOWEKEZA KWA MIAKA IJAYO KULIKO FIXED NA UTT.

IMAGINE 50M UPEWE 500K PER MONTH AISEE😂😂😂

LABDA IWE NI KUTUNZA HAPO SAWA LAKN SIO KUWEKEZA
 
BRO NADHANI HATA MALAIKA WA KHERI WAKIONA HUU UJUMBE WAKO WATACHEKA SANA,

CHA KWANZA SINA NJAA ACCOUNT INASOMA VYEMA,

CHA PILI ME NA MIAKA 23 SI MKUBWA KIUMRI KIHIVYO NA UMRI WA WASTANI,ILA NI MKUBWA KI EXPERIENCE NILIAZANGA BIASHARA NA MIAKA 9

TATU KUNA VITU NILIVIFAHAMU MIAKA 2 ILIOPITA NA NIKIWA 21 ALAFU NA MATAJIRI HAWATUAMBIAGI PIA ILA KUMPA MAARIFA BURE SIWEZI ALAFU SIO LAZIMA HAWEZI AACHE😂😂😂
Kuwa makini kuna mtu hapo juu kaweka namba ya simu nina mashaka nae.
 
Sasa nimeleta hoja hii mezani kwenu ili mnishauri nianze na kipi katika hiyo pesa.
Kumbuka hapo
1. Sijajenga
2. Sina kiwanja
3. Sina biashara yoyote
4. Sijaolewa (wanasemaga mume ni asset)
5. Kazi yangu ni ya 'kijungujiko'
50ml ni pesa ndogo sana ukiwa na WENGE, ila ukituliza kichwa ni hela inatosha kukuondolea UMASIKINI.

Kwanza, Relax na utulie(hili utulivu ni gumu sana), ila jitahidi utulie sana maana Pesa huwa haitaki kelele na haikai mahali ambapo hapana utulivu. UTULIVU ninamaanisha nafsi yako isianze kuwaza mambo meeeengi ikiamini hio pesa itayamaliza yote, HAPA UTAFELI.

Pili, Hela ya urithi huwa haikai(NI WACHACHE SANA HUTOBOA KWA HELA ZA URITHI, labda MALI ila sio HELA), hii ni kwasababu ya hio point ya juu niliyoeleza, so usiingie kwenye hilo KUNDI. Maana utaona hela hio inaweza maliza kila tatizo lako ila ITAISHA UNAIONA.

USHAURI, Ili uweze kutuliza kichwa lazima uwe na jambo ambalo utaona hio 50ml haitoshi, hili litafanya uione thamani halisi ya hio Pesa (actual value) na sio hii ya kufikirika.

BIASHARA itakayokufaa sana kwa hyo hela yako ni nyumba ya kupangisha(chumba sebule) AU boresha hiohio biashara unayoifanya ili ilete pesa zaidi na hakikisha biashara utayochagua unaijua vizuri maana WAPIGAJI nao wanaitaka hio Pesa. UTAPATA WASHAURI WENGI SANA KWA SASA, na wote biashara zao watasema zinalipa.

Nasisitiza tena. PESA haitaki kelele, hivyo be disciplined. Wish you all the best.
 
Ukipata mwanaume anayejielewa hapo mnasogea kidogo ;awe na tabia kama zako ,awe mwaminifu.

Ogopa matapeli wapo sana humu ,wanaweza kuja inbox.
 
Back
Top Bottom