Habarini za wakati huu ndugu zangu wapendwa wa Jf.
Ni hivi,
Kuna maeneo ya familia yameuzwa mahali na kila mwanafamilia amepata gawio la Mil.45.
Na kwa kuwa nilikuwa na akiba ya kama Mil.5 benki basi nikajumuisha na ile Mil.45 ikawa kama Mil.50.
Najua humu kuna watu wa kada mbalimbali
Wafanyabiashara,
Washauri wa kazi,
Wajenzi,
Wauza bidhaa mbalimbali,
Madalali,
Wasomi n.k
Sasa nimeleta hoja hii mezani kwenu ili mnishauri nianze na kipi katika hiyo pesa.
Kumbuka hapo
1. Sijajenga
2. Sina kiwanja
3. Sina biashara yoyote
4. Sijaolewa (wanasemaga mume ni asset)
5. Kazi yangu ni ya 'kijungujiko'
6. Umri wangu ni miaka 30 na dini yangu ni Mkristo Mkatoliki.
Please wale wa kusema niweke mkeka utoe Odd hapana.
Nahitaji kufanyia mambo ya maana tu.
Naombeni msaada kabla sijajua cha kufanya.
Asanteni
Usifanye chochote kwanza hiyo pesa hifadhi bank lakini iwe kwenye fixed acc ya mda mfupi au weka UTT bond fund ambayo utaweza kuitoa yote bila
Masharti yoyote na italidha thaman ya pesa yako
Lengo la kukwambia uhifadhi hiyo pesa kwanza ni kuwa ujipe mda wa kupunguza mihemuko na kimuhemuhe cha kuwa na hiyo pesa ili akili itulie urudi katika akili ya mwanzo iliokupa maarifa ya kukusanya hiyo milioni 5 ulioweka bank.. naamini kabla ya hiyi 5m uliokusanya mdogo mdogo usingehitaji ushauri wa jinsi ya kuitumia sababu kitendo cha kuikusanya mdogo mdogo maana yake kuna ki malengo flan na displine uliiweka.. do not loose that.. ulichonacho sasa ni mihemuko
maana naona unataka kuachana na akili iliokupa milioni tano unataka kuazima akili za wengine ili wakuambie jinsi ya kuitumia milioni 50
Tuliza akili kwanza rudi tafakari je kabla ya hiyo 45m malengo kwenye maisha yako yalikuwa nini. Maana pesa ambazo zinakuja kama sadaka usipotulize akili Zitaondoka bila kutarajia kama zilivyokuja
Simaanishi kuwa watu hawatatoa mawazo mazuri humu ila mawazo ya mtu mwingine yanaweza yasiwe na faida kwako sababu yanaweza yasiendane na mazingira na life sytle unayoishi.. mara nyingi tunaomba ushauri kwa vitu ambavyo tayari tuna experince navyo ili
Tujue tunaboreshaje.. lakini ni hatari kuja kuomba ushauri wa jinsi ya kutumia 50m kwa Mtu ambaye hajui hata ugali wako wa siku unaupataje.. au hasling zako za kila siku zinaendaje ni kama Unabet.
Kumbuka unazungumzia jambo nyeti ambalo litaboresha maisha yako au kukupa msongo wa mawazo
Bahat mbaya Wa TZ na Afrika kwa ujumla hatuna Elimu ya Fedha hatujui thamani ya pesa... hapa ndio watu weupe (wazungu, wahindi na kadhalika) ndio wanatupiga bao.. tunajua pesa ni kwa ajili ya kununulia vitu na huduma tu .. mfumo
Wetu wa maisha na malezi
Kuanzia ngazi ya serikali hadi familia unatufundisha kimatendo na kinadharia jinsi ya ku spend money not on how to manage money..
Kumbuka ""IF YOUR MONEY IS NOT MAKING YOU MONEY, THEN THERE IS A CHANCE YOUR MONEY IS LOOSING YOU MONEY.
Note: usikimbilie kujenga.. belive me kumiliki nyumba sio kipaumbele kama jamii yetu inavyotuaminisha