Wazoefu na wabobezi: Nina akiba ya Tsh. Milioni 50 nianze na kipi maishani?

Tshs 50,000,000.00 = $20,000.00
1: project no. 1: Tafuta location nzuri nunua Bakery ndogo ($4,000+ Sausage maker, ($500.00) + Juice processing ( small business) $1,000.00+ machine ndogo ya kutengeneza ice cream $1,000.00+ machine ndogo ya kutengeneza chips $1,000+ majiko ya kutengeneza chips. Hizo zote ziweke location moja kwenye watu wengi gharama zake zote ni chini ya $10,000.00 pambana nazo zingine $10,000 weka Bank.

2: Fungua mgahawa mkubwa anza kulisha watu ,uwe na wapishi wazuri tumia nusu ya hiyo pesa. Zingine weka Bank

Sijui uko mkoa gani ningekupa projects nyingi zaidi au nitumiye kwenye Private message
 
Namba nne vijana wanapita nayo sana.

Nakushauri kimoja.

Tafuta mafundi nyumba au mafundi Rangi wale ambao wameenda shule na ambao hawajeenda shule yaani wale wataani.

Fungua ofisi na ifanye iwe kampuni ya ujenzi utatafuta Kazi lakini siku moja utapita.

Au nenda ZANZIBAR kale urojo utulize wenge Kwanza.
 
Nunua hisa za CRDB za 25m. 25m nyingine tia UTT Bond fund upate 200,000 each month kama faida ya kuendesha maisha mdomdo. Hisa zikitema toa kiasi wekeza tena UTT endeleza mchakato huo baada ya miaka 5 utakuja kunishukuru
 
AmKATRINA njoo tuunganishe nguvu me nna 25m UTT + 50m tayari tuna 75m yetu 😊
Baada ya hapo ntakupa mipango ambayo ndani ya 5 years wasipo tuita Freemasons basi unidai 50m yako
 
Kama uko Dar nenda nje ya mji sehemu za makazi mapya fungua banda la vinywaji mchanganyiko mixer pombe za kienyeji na duka genge kama mil 3 au nne hivi,,,,,,halafu wasikilize sana walevi utapata mawazo ya kila namna na hakuna atakaye fahamu kwamba una fedha,,,
N.B,
Usisahau kuweka supu za makwasukwasu
 
Mkuu naomba contact za wanaouza viwanja maeneo haya. Wale wa makampuni itapendeza.
 
Kila nikiandika nafuta,.
Njoo kwanza tule kitimoto hapa tubadilishane mawazo mawili matatu
Wewe si umetoka kupigwa pesa na sister wa ki-lutheran juzi tu hapo, leo hii unataka kumpa mtu ushauri wa kipesa tena?.
 
Una elimu gani kama una degree tuongee
 
Mume mtarajiwa niko hapa, unachelewesha watoto wetu kuanza shule wewe.
 


Usifanye chochote kwanza hiyo pesa hifadhi bank lakini iwe kwenye fixed acc ya mda mfupi au weka UTT bond fund ambayo utaweza kuitoa yote bila
Masharti yoyote na italidha thaman ya pesa yako

Lengo la kukwambia uhifadhi hiyo pesa kwanza ni kuwa ujipe mda wa kupunguza mihemuko na kimuhemuhe cha kuwa na hiyo pesa ili akili itulie urudi katika akili ya mwanzo iliokupa maarifa ya kukusanya hiyo milioni 5 ulioweka bank.. naamini kabla ya hiyi 5m uliokusanya mdogo mdogo usingehitaji ushauri wa jinsi ya kuitumia sababu kitendo cha kuikusanya mdogo mdogo maana yake kuna ki malengo flan na displine uliiweka.. do not loose that.. ulichonacho sasa ni mihemuko

maana naona unataka kuachana na akili iliokupa milioni tano unataka kuazima akili za wengine ili wakuambie jinsi ya kuitumia milioni 50

Tuliza akili kwanza rudi tafakari je kabla ya hiyo 45m malengo kwenye maisha yako yalikuwa nini. Maana pesa ambazo zinakuja kama sadaka usipotulize akili Zitaondoka bila kutarajia kama zilivyokuja

Simaanishi kuwa watu hawatatoa mawazo mazuri humu ila mawazo ya mtu mwingine yanaweza yasiwe na faida kwako sababu yanaweza yasiendane na mazingira na life sytle unayoishi.. mara nyingi tunaomba ushauri kwa vitu ambavyo tayari tuna experince navyo ili
Tujue tunaboreshaje.. lakini ni hatari kuja kuomba ushauri wa jinsi ya kutumia 50m kwa Mtu ambaye hajui hata ugali wako wa siku unaupataje.. au hasling zako za kila siku zinaendaje ni kama Unabet.

Kumbuka unazungumzia jambo nyeti ambalo litaboresha maisha yako au kukupa msongo wa mawazo

Bahat mbaya Wa TZ na Afrika kwa ujumla hatuna Elimu ya Fedha hatujui thamani ya pesa... hapa ndio watu weupe (wazungu, wahindi na kadhalika) ndio wanatupiga bao.. tunajua pesa ni kwa ajili ya kununulia vitu na huduma tu .. mfumo
Wetu wa maisha na malezi
Kuanzia ngazi ya serikali hadi familia unatufundisha kimatendo na kinadharia jinsi ya ku spend money not on how to manage money..

Kumbuka ""IF YOUR MONEY IS NOT MAKING YOU MONEY, THEN THERE IS A CHANCE YOUR MONEY IS LOOSING YOU MONEY.

Note: usikimbilie kujenga.. belive me kumiliki nyumba sio kipaumbele kama jamii yetu inavyotuaminisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…