Wazoefu wamikopo ya mabank nahitaji uzoefu wenu

Usiwekeze nyumba ndugu, mikopo ya benki sio rafiki.
Siwezi kushindwa Kulipa, vilevile endapo kama nitashindwa kulipa basi hiyo nyumba nitaiuza mwenyewe niwamalizie deni lao nibaki nachenji
 
Iyo hati ya nyumba itakua bank.nan ata kubari kuuziwa nyumba bila Hati ya nyumba...

Yani ukisha kopa iyo nyumba utaendelea kukaa.ila sio yako tena adi utakapo rudisha deni na upewe hati yake
Siwezi kushindwa Kulipa, vilevile endapo kama nitashindwa kulipa basi hiyo nyumba nitaiuza mwenyewe niwamalizie deni lao nibaki nachenji
 
Kopa bank zote sio Access Bank mkuu narudia sio Access Bank
Access wapoje mkuu? Ila nasikia juu juu kuwa hao jamaa wanajua sana kudai, wanaweza timba kwako hata mara nne kwa siku.
 
Wazoefu wamikopo yamabank nahitaji uzoefu wenu.

Nibank gani naweza pata mkopo wabiashara wakuanzia Milion 5 mpaka milioni 8 kwadhamana yanyumba?
NMB wanatoa mkopo ndani ya Siku 7 za kazi Bila shida yoyote.

1. Lazima uwe na biashara ambayo umeishaifanya kwa muda was miezi 6
2. Uwe na ripoti ya fedha ya miezi 6
3. Uwe na hati ya nyumba Kama dhamana.

Riba yao Ni 14% kwa mwaka sawa na 1.6% kwa mwezi.
Kila la kheri
 
N.m.b, t.p.b, crdb.je nyumba ina hati au leseni ya makazi?je unataka kuanzisha biashara au ulisha anza?kama unaanza usikope
Wazoefu wamikopo yamabank nahitaji uzoefu wenu.

Nibank gani naweza pata mkopo wabiashara wakuanzia Milion 5 mpaka milioni 8 kwadhamana yanyumba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…