Wazungu walituwahi akili mapema, Afrika ingekuwa inajiendeleza kupitia malipo kwa madini.

Wazungu walituwahi akili mapema, Afrika ingekuwa inajiendeleza kupitia malipo kwa madini.

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
3,577
Reaction score
5,664
Wakati wa ukoloni, Wazungu waliona thamani ya madini ya Afrika mapema sana. Walitambua kwamba dhahabu, almasi, shaba na madini mengine yalikuwa msingi wa nguvu za kiuchumi na kisiasa duniani.
Badala ya kuruhusu Waafrika kutumia rasilimali hizi kama njia ya kujenga miundombinu na kuendeleza uchumi wao, walihakikisha madini yanachukuliwa ghafi na kupelekwa Ulaya.
Hapo ndipo akili ya Waafrika ilicheleweshwa,,,, tulibaki tukitegemea fedha za kigeni na misaada, badala ya kutumia hazina zetu kama malipo ya moja kwa moja kwa maendeleo.

Kama Afrika ingechagua mfumo wa malipo kwa madini, tungekuwa na nafasi ya kujenga reli, barabara, shule na hospitali mapema.
Dhahabu ingeweza kuwa sarafu ya kimataifa ya Afrika, ikitoa nguvu ya kujadiliana na mataifa mengine. Badala ya kuomba mikopo yenye riba kubwa, tungeweza kusema: “Tunawalipa kwa dhahabu, tujengeeni barabara na viwanda.” Hii ingekuwa njia ya kujitegemea na kupunguza utegemezi wa dola.

Lakini Wazungu walituwahi akili. Walitengeneza mifumo ya benki za kikoloni, wakadhibiti biashara na thamani ya madini, na kuhakikisha Afrika inabaki kuwa mashimo tu. Matokeo yake ni mzunguko wa madeni, utegemezi wa misaada, na kuchelewa kwa viwanda.
Vizazi vingi vinakua bila kuona faida ya madini ya nchi zao, huku Ulaya ikijenga miji na miundombinu kwa nguvu ya rasilimali zetu.

Leo, mjadala wa de-dollarization na malipo kwa madini unarudi tena. Ikiwa Afrika ingeweka dhahabu na madini mengine kama msingi wa malipo ya kimataifa, tungeweza kuondoka kwenye mtego wa sarafu za kigeni na kujenga uchumi wa ndani.

Hii si ndoto mpya bali ni nafasi iliyopotezwa mapema kwa sababu akili zetu zilitanguliwa na Wazungu.
 
Changamoto kubwa ni baada ya uhuru, nchi nyingi za Afrika zimeshindwa kujenga taasisi imara, kuongeza thamani ya madini kupitia viwanda, na kusimamia rasilimali zake kwa ufanisi.
 
Back
Top Bottom