Wazungu wana uchawi wa "small scale"?

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Eti katunguri ka kibantu
 
Huyo jamaa anayetangatanga nje alikuwa ni msukule ama?
 
Huyo jamaa anayetangatanga nje alikuwa ni msukule ama?
Itakuwa hivyo..ila tambua hawa jamaa hawatumii sana black magic kama ilivyo huku afrika. Wao wanawasiliana moja kwa moja na ibilisi na wana dhehebu lao wanajiita wajenzi huru au freemason na wana kampeni ya kushawishi kila mwanadamu amwasi Mungu na kujiunga nao na kuna kipindi wataanza kutumia nguvu, yaani chagua kujiunga nao ili uishi au kufa.
 
Ona unavyoruka ruka[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

"Thibitisha Kama Mtume Paulo alieneza ukristo"

Wewe SI unawaulizaga wengine wathibitishe Kama Mungu yupo, na wewe leo hii TUTHIBITISHIE KAMA MTUME PAULO ALIENEZA UKRISTO
Kuthibitisha ni nini?

Lazima tukubaliqne kwamba uelewa wako na uelewa wangu wa uthibitisho ni ule ule.

Kwa sababu, bila kukubaliana, kirahisi sana naweza kukuambia kwamba, Mtume Paulo alieneza Ukristo.

Na uthibitisho ni Biblia imesema hivyo.

Hapo, hata kama hukubaliani nami, ukikataa nafasi ya ku define uthibitisho ni nini, utafanya mjadala mzima usiwe na maana.

Nitathibitishaje wakati wewe na mimi hatujakubaliana uthibitisho ni nini?

Tutafanya vipi "litmus test" wakati hatujakubaliana bado nyekundu ni ipi na ya bluu ni ipi?
 
ooh hapo nimekupata sasa.
Kwa maana hiyo huu uchawi wetu sijui wa sumbawanga au sijui simiyu unaosifika kwao hao ni cha mtoto sana si ndio?
 
Mambo ya kipuuzi sio uchawi na kila race inafanya, onesha/ Thibitisha/Tukumbushe uchawi waliowahi kuufanya.
Kama wanaweza kufanya mambo ya kipuuzi hao wazungu na kufanya maasi,sasa wanashindwa vp na kufanya uchawi? Ungesema uchawi ni katika mambo ya kipuuzi na wazungu hawana mambo ya kipuuzi hapo ndio ningekuelewa, ila kama kila jamii ina mambo ya kipuuzi basi tambua na uchawi pia upo kwenye kila jamii.

Kabla ya kuniambia nikuthibitishie kwanza wewe una uhakika kiasi gani wenye kukufanya useme wazungu hawafanyi uchawi? Au ulikuwa unataka uone vibanda vya waganga na uwepo wa akina Manyanyau huko kwa wazungu ndio ujue kuwa wazungu nao washirikina?

Imani za kishirikina kwa wazungu zipo japo si sana ila zipo na hivyo uchawi pia hufanyika huko.
 
mtu anayedai uthibitisho dhidi ya jambo fulani nia yake apate kueleweshwa kutoka kwa mtu anayedai kitu hicho kipo

kulingana na namna ambavyo utathibitisha ndivyo nitakapopata concept ya kuuelewa
Hapana,huwezi kukurupuka na kuanza kudai uthibitisho wa kitu ambacho hujakielewa lazima kwanza ukifahamu hicho kitu.

Inawezekana hicho kitu unakijua kabisa kuwa kipo huhitaji uthibitisho au hukijui kabisa kinafananaje hivyo huwezi kukimbilia uthibitishiwe hicho kitu hata haukielewi,ndio maana nikakuuliza unaelewa vp uchawi kwanza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…