Wazungu Wanaogopa Ongezeko la Waafrika – Je, Wana Sababu?

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
1,435
Reaction score
3,120
Nimeangalia documentary moja nzito YouTube, ambayo inazungumzia hofu inayoongezeka Ulaya kuhusu ongezeko la watu kutoka Afrika, hususan kusini mwa Jangwa la Sahara.
Mwandishi mmoja mwenye IQ ya 160 anadai kuwa:

“Civilisation is a product of the genetic and cultural makeup of its founding people. If those people are replaced or diluted, the civilisation collapses.”

Nimeandika tafakari yangu kamili kuhusu hilo hapa:
➡️ “Afrika ni Tishio kwa Ustaarabu (civilization)” – Je, Huyu Mzungu Ana Sababu? : Wingi Wetu ni Baraka au Laana kwa Dunia?

Nauliza:
Je, hizi hofu ni za kweli au ni aina mpya ya ubaguzi wa kimataifa? Je, Afrika inaweza kuchukua nafasi kama chanzo cha ustaarabu?
 
Waendelee kuwa na hofu huku wao wana promote ujinga kwa vijana wao. Majitu yao hayazai, mashoga na masagaji.
 
Wana shida na rasilimali sio sisi... Tukiwa wengi watashindwa kutudanganyia mkate ili wachukue vya thamani
 
Unadhani ni rahisi?
Wakiacha kutoa misaada,wakizuia technology zao kuanzia net Hadi matibabu,madawa,viuatilifu..wakiweka vikwazo vya uchumi,miaka 50 tu,tutabaki Milion 200 Africa nzima..
 
Wakiacha kutoa misaada,wakizuia technology zao kuanzia net Hadi matibabu,madawa,viuatilifu..wakiweka vikwazo vya uchumi,miaka 50 tu,tutabaki Milion 200 Africa nzima..
Zamani kabla hawajaja tuliishije? mbona hatukuisha?.
 
Zamani kabla hawajaja tuliishije? mbona hatukuisha?.
Watu walikua wanakufa kwa kukosa chanjo,Kila ugonjwa ulikua hatari..wamama katika kujifungua walikua wanapoteza watoto au wao kupoteza maisha..mtoto akifanikiwa kuishi miaka 15 Basi Mungu mkubwa ataishi Hadi uzee ila vifo vya watoto ilikua kawaida..

Sijui Kama tungeisha wote au vipi ila bila wazungu maisha kwetu yangekua tofauti Sana.. primitives
 
Unadhani ni rahisi?
Kuna ugumu Gani kwani? Wakikata misaada yote na mikopo na tukapigwa blockade hamna hata nzi inayoingia au kutoka barani hapa nakuhakikishia itachukua wiki mbili tu mpaka mwezi tunarudi ujima; baada ya mwaka wakija kuchunguza tutakaobaki tutakuwa tunaishi kama Wahadzabe
 
Tatizo wengi wetu tumekulia mfumo huu wa Sasa na tunadhani huko nyuma napo ilikua hivi hivi; tunasahau wasatani wa maisha kwa typical muafrika ilikuwa miaka 35
 
Tatizo wengi wetu tumekulia mfumo huu wa Sasa na tunadhani huko nyuma napo ilikua hivi hivi; tunasahau wasatani wa maisha kwa typical muafrika ilikuwa miaka 35
Tunajisahau sana,.au watu hawataki kuangalia tulipo toka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…