Wazungumzaji wa lingala na kiswahili cha kikongo tupeane phrases za Lingala

Wazungumzaji wa lingala na kiswahili cha kikongo tupeane phrases za Lingala

chotera

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
6,560
Reaction score
15,864
Hapa wadau

Ni iwe ulijifunza, uliishi Congo na unaweza kuongea lingala basi unaweza kushare hata mistari miwili mitatu ukaeleza ina maana gani ili watu wanifunze lingala,

Mfano ule wimbo wa donat mwanzo pale alipoimba “Bana Congo tosimbanamaboko, Congo elonga" alimaanisha “wakongomani wote tushikane mkono au tuungane Kongo isonge mbele

Maneno kama "Bolingo Nangai" ni kusema "mpenzi wangu" au "posa na bolingo" inamaana ya "kiu ya mapenzi," naomba wadau tuendelee kutiririka.
 
B
Hapa wadau
Ni iwe ulijifunza, uliishi Congo na unaweza kuongea lingala basi unaweza kushare hata mistari miwili mitatu ukaeleza ina maana gani ili watu wanifunze lingala,
Mfano ule wimbo wa donat mwanza pale alipoimba “ Bana Congo tosimbanamaboko, congo elonga alimaanisha “ wakongomani wote tushikane mkono au tuungane Kongo isonge mbele “
Maneno kama Bolingo Nangai ni kusema mpenzi wangu au posa na bolingo inamaana ya kiu ya mapenzi, naomba wadau tuendelee kutiririka.
Bolingo nangai ni mapenzi yangu...
 
Hiyo hapo
Screenshot_20220723-223032_Google.jpg


Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Haa...napenda kikongo mimi,lugha yao iko romantic sana. Hebu mmoja anipe verse yoyote ya jb mpiana kwa tafsiri ya kiswahili hasa kutoka ule wimbo wa feux d'amour

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
Ingia youtube tafuta translation yake Kuna mwana ameutafsiri wimbo wote kwa kiswahili Safi kabisa
 
Mfano Fally kwenye wimbo wa Associe alitamka maneno kama Bolingo esalaka pasi, hapa alimaanisha mapenzi huleta maumivu sana
Pia alisema ,Mais nayebi Bolingo eza Mabe na malamu (Mimi najuwa mapenzi Yana ubaya na wema)

Gatho beevans naye kwenye azalaki anasema nakangi motema nkasi mpasi esili te, alimaanisha sawa ameumizwa Moyo lakini maisha lazima yaende
 
Back
Top Bottom