WCB, Diamond na Rayvanny watozwa Tsh milioni 9 kutokana na maudhui mabovu ya wimbo 'Mwanza'

WCB, Diamond na Rayvanny watozwa Tsh milioni 9 kutokana na maudhui mabovu ya wimbo 'Mwanza'

Wewe jamaa ni kichwani maji kabisa hivi unadhani watoto nyimbo wanajifunzia nyumbani? Watoto wanacheza mtaani na huko mtaani Kuna vilibrary na soloon ambazo zinapiga nyimbo muda wote, mtoto anajifunza vitu vingi mtaani kuliko nyumbani, ukisema usiupige nyumbani lakini mtoto akarudi anaimba nyege nyege nyege.
Hivi huwa unatumia Nini kufikiri?

Kama wewe
 
Shida Neno NYEGEEE bhasiii...Why wafupishee Nyegeziii....!??? Iokotee popotee inaimbwaa maana ni ngumu hata mtoto kujua ni matusii sasaa neno Nyegee leynyewee tayari ni Tusii.. Iokotee haina tusi direct ilaa tafsida tu

Nan kakwambia kuwa nyege ni tusi? Nyege ni hali ya kutama kufanya mapenzi. Nasio tendo ili liwe tusi ni lazima lihusishwe na kitendo. Matusi mengi unaojua wew ni vitenzi. Ila nyege sio kitenzi ni hali
 
Jaribu kuwa serious basi,akafanyie mziki nje ya nchi ? Angeweza tu kama mashairi yake pamoja na lugha ingekuwa inajulikana ,hivi unapoimba nyege,nyege ,nyegezi unakuwa unaimanisha nini?
Hivi ww jamaa unaposikiliza mziki wa Cuba, Spain, India, Korea, Congo n.k unafahamu nn kuhusu lugha hizo? Otherwise hujui nn maana ya muziki.
 
Nan kakwambia kuwa nyege ni tusi? Nyege ni hali ya kutama kufanya mapenzi. Nasio tendo ili liwe tusi ni lazima lihusishwe na kitendo. Matusi mengi unaojua wew ni vitenzi. Ila nyege sio kitenzi ni hali


Uko sawa kabisa, nyege ni hali, tena hali ya udhaifu ya juu sana kwa kiumbe hai! Hali inayositiriwa kwa heshima zote sirini tangu Enzi za mababu zetu!

Lakini hivi tumejiuliza kama tuko tayari kumuona mtoto wa miaka 8 (hata kama sio wako wa kuzaa) wakilitamka hilo neno? Neno ambalo kwa jamii yetu limekua likitumika faragha na wahusika ama likitumika mbele ya watu wazima tu? Halafu hizi nyimbo watoto wengine wanajifunzia mashuleni na kwa ndugu, wakubwa zao, wasaidizi wa ndani na hata simu zetu tunapowapa wacheze games! Of coz ni ngumu sana kuzuia mabadiriko katika maadili nyakati hizi lakini sio lazima tuyasaidie hayo mabadiriko yaje haraka zaidi tena bila kuzingatia faida na hasara kwanza!

Radio na television ni kitu cha hatari sana kwa ubongo wa binaadam hasa kama anafanya matumizi ya kila wakati. Unapokua unasikiliza nyimbo zenye maudhui ya mapenzi ama ngono kila muda na kutazama video ama picha zenye maudhui hayo hayo, sio ajabu wewe ukawa ni mtu unaependa sana kufanya mapenzi ama ngono kila wakati unapohisi inafaa! ( Mind Programing! !)

Hebu fikiria kwa haraka nusu ya vijana wote wanaoendesha bodaboda ni wapenzi wa Nyimbo za wasafi ambazo nyingi zinazungumzia mambo ya chumbani! Vijana hawa maybe 300+ wawe muda wote wanawaza ngono na mapenzi na kuvifanya, nguvu kazi itaenda wapi zaidi?

Kitu kingine mjue wengine sio kwamba tunawaingilia mambo yenu ila mnaharibu pale mnapozileta faragha zetu sote (hata tusio wapenzi wa hizo nyimbo) hadharani tena mpaka kwa watoto wetu bila utashi wetu! Hivi hamuwezi kuzungumzia mapenzi kwa mafumbo zaidi? Mbona siku hizi mnalazimisha sana maneno ya sirini kusemwa hadharani? Mnachotafuta kugundua ni nini? Kwamba ninyi mnajua sana kuliko wengine? Aisee, inauma!! Ila ndio dunia!

**Sorry kwa nukuu Chief!
 
Back
Top Bottom