WCB hawajasikika top 20

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
3,607
Reaction score
9,430
halla jf...

kama kawaida jumapili nipo nyumbani nimechill kuisindikiza weekend, kwa kawaida mara nyingi mm sio mdau wa clouds radio/tv, kwa hiyo top 20 huwa sisikilizi sana, badala yake huwa nasikiliza efm kuna kipindi kinachopiga bongo fleva za kitambo kinachoendeshwa na rdj kwachee, kipindi hicho kinaitwa muda wetu... any way hii sio ishu.

leo nikiwa nimetulia nikakumbuka kuna yanayosema chini chini kwamba wcb na clouds media kwa sasa hawapikiki chungu kimoja na nyimbo zao zimepigwa pini pale mawingu. nika-tune clouds fm kusikiliza top twenty kilichoendeshwa na mwanadada mamy baby. what a surprise sijaisikia nyimbo yoyote kutoka chamani wcb. nimeshangaa sana, kwa nn ? hawa jamaa wakiongozwa na boss wao naseeb wanatoa sana hits mara kwa mara kiasi kwamba ni ngumu kushindwa kuingia kwenye chat za media kali kama clouds.....

kuna harufu kubwa ya moshi inayofukuta chini, kati ya wcb na clouds, yamesemwa mengi sana, lakini mwisho wa siku muziki bila media amna kitu, japo kuna nguvu kubwa sana ya mitandao.

boss joe anatakiwa awe smart sana na hii issue, daimond kwa mara nyingine management yake inamuangusha, kina salam, tale na fela uswahili mwingi, wanampoteza jamaa bila kujijua. daimond anajisahau anavimba kichwa.
bashite ana uhusika mkubwa sana kwenye hili, ndiye mlezi wa wcb, ugomvi wake na boss ruge usimsababishe awaingize hawa jamaa, hata ile project ya tv na radio nahisi kuna mkono wa mkolomije, lengo ni kuwakomoa clouds na kupambana nao, kuna msemo unaosema aliyetangulia katangulia tu.

God bless Tanzania yetu ya maziwa na asali.
 
WCB income yao kubwa iko kwenye youtube na internet
hawahitaji clouds ili wafanikiwe
wanahitaji clouds kwa local spotlight ...

but kama wataanzisha media zao ...labda watafanikiwa kwa hilo..

But Ruge ni very smart hagombani na mtu ikiwa huyo mtu yuko top
anagombana only akiona decline imeshaanza...anaharakisha the fall ...
lets wait and see...
 
Hamna wanahabari huru mbele ya bosi wake kwa hiyo kawaida,ndio ujue uhuru wa habari kwa waandishi unamipaka.,bosi hakisema hamna basi hamna,na bosi hata akikosea vipi hutakiwi kuriport (mf Zamaradi na Mr Ruge).Tatizo la clouds hawataki mtu ujitambue,msanii akiwa mkubwa hata matumizi yanakuwa makubwa wao ,kila siku wanataka wakunyonye kisa wanakupa promo,hebu mcheki Barnaba ana nini .Alafu ilo swala la msani kuwa na media Mondi si wa kwanza akina Youssou N'Dour wana radio na wao kila siku wanazungumzia fursa na hizi ndio fursa kijana kaona kaamua kuifuata.Kwa staili hii ya Clouds ikiendekezwa tutatengeneza WASANII MASIKINI WENYE MAJINA MAKUBWA mf Barnaba.Ukichunguza huu mgogoro ni watu tu wanaona maslai yao yanavurugwa na Diamonda anaonekana hana nidham sababu ya kutetea maslai yake.Nakuhusu kushuka hiyo ni kawaida ktk sanaa kwani akina R kelly,P.didy,Brandy,Monica wapo wapi lkn leo si unaona wapo vizuri kiuchumi kwa hiyo tatizo sio kushuka bali unashuka huku ukiwa na Investment zinazokubeba na dogo kaamua kuwekeza na mkae mkijua hamna msanii ambaye hatokuja kushushuka (hata upewe promo kila sek kushuka lazima
) .Bora ushuke huku ushawekeza ,kuliko kushuka alafu hauna kitu kisa ulikuwa unataka upate promo.(kumsaidia mtu si lazima huko mbele umnyonye hata huyo LIL WYNE nae kamkazia BIRDMAIN na kamwambia album mpya haachii mpaka wampe dola mil 56,japokuwa alimsaidia sana)
 
kuna watu ambao wanawatia wenzao upepo wakijinga humu then mimi nawachora tu ..nawachora wanahis suala la kumanage station radio na TV nikitu rahisi kama suala la kuubinya mkate aiseee ...

clouds FM walifanikiwa mnooo kwenye media kupitia burudani kwakuwa miaka ya nyuma hapakuwahi kuwa na radio ama chombo kinachowagusa vijana ktk suala la burudani vile ipaswavyo yaani vijana wa miaka hiyo walikuwa wanahitaji kuwa kama kina 50cent ki life style ki star na kila kitu ..but hawakuwa na sehemu pakuwakilisha hilo clouds wkaiona hiyo fursa wakaitumia vyema ..ndio maana ikawa nirahisi kwakiasi Fulani kufika hapo walipo ijpo kuwa sio rahisi kivile kama tunavyodhani ..

yote kwa yote hakuna kinacho. shindikana chini ya jua
 
kuna watu ambao wanawatia wenzao upepo wakijinga humu then mimi nawachora tu ..nawachora wanahis suala la kumanage station radio na TV nikitu rahisi kama suala la kuubinya mkate aiseee ...

clouds FM walifanikiwa mnooo kwenye media kupitia burudani kwakuwa miaka ya nyuma hapakuwahi kuwa na radio ama chombo kinachowagusa vijana ktk suala la burudani vile ipaswavyo yaani vijana wa miaka hiyo walikuwa wanahitaji kuwa kama kina 50cent ki life style ki star na kila kitu ..but hawakuwa na sehemu pakuwakilisha hilo clouds wkaiona hiyo fursa wakaitumia vyema ..ndio maana ikawa nirahisi kwakiasi Fulani kufika hapo walipo ijpo kuwa sio rahisi kivile kama tunavyodhani ..

yote kwa yote hakuna kinacho. shindikana chini ya jua
ngoja tuone
 
tusubiri tuone, hii ishu bado ni mbichi sana...
 
yote kwa yote ukweli utabaki kuwa media wana impact sana kwenye muziki wetu... angalia kwa mfano mbosso, ndio kwanza ametambulishwa kundini na ametoa nyimbo mbili, kwa bahati mbaya kakutana na ugomvi, huoni kwamba huu ugomvi utamdhoofisha sana kijana ? muda utasema
 
Diamond anapotea kwenye muziki kwa kasi sana, ukiangalia watu aliokuwa anashindana nao mfano Davido anazidi kumuacha mbali kwa mafanikio ya kimuziki.
Diamond yupo busy na beef lake na CMG, Mara huku anapelekwa mahakamani ana kesi na mchepuko wake(Hamisa). Kwa kifupi Diamond sasa hivi hana muda wa ku focus kwenye mziki wake.
 
Huyu dogo namuombea mafanikio atoboe mpaka basi ili adhihirishe uwepo wa Mungu mmiliki wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo,

Nataka auonyeshe umma kama inawezakana na hakuna alizaliwa nacho ila siri ni kujituma tu,

Nataka auonyeshe umma kwamba Mungu ni mmoja tu na anambariki mtu kadri atakavyo yeye

Nataka auonyeshe umma kwamba hakuna mmiliki wa maish ya watu

Kimziki simpendi Diamond ila ntakuwa mchawi nikianza kushangilia kwamba anapotea


Go boy go boy

Tuombeane kheri jaman
 
Ruge,Tale,Sallam na Fella wanajuana.

kesi ya nyani kapewa ngedere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…