WCB ndio imeshikilia Bongo Fleva kwa sasa, very creative label

WCB ndio imeshikilia Bongo Fleva kwa sasa, very creative label

WCB(Wasafi Classic Baby)nadhani nikisema hivyo kila mtu anaelewa.
WCB nadhani kwa sasa ndio label iliyoshikilia industry ya Bongo Fleva hawa watu wako very Creative na Wanafikra yakinifu. Tena isitoshe tu kusema ni label namba moja Tanzania bali hata Afrika inajizolea umaarufu kwa sasa.

Label Ina combination ya wasanii wenye majina makubwa Kama vile;
Diamond Platnumz (The C.E.O)
Rayvanny
Mbosso
Zuchu
Lava Lava

Zipo fununu pia zinasema Hanstone aliyeshirikishwa na Maua Sama kwenye ngoma ya Iokote naye yuko WCB anasubiri utambulisho tu.

Label hii Ina wasanii wachapakazi haswa ikiongozwa na Diamond Platnumz.

Wamejizolea mashabiki wengi sana East Afrika na Afrika kwa ujumla kiasi kwamba kila msanii anayepita hapati wakati mgumu sana kuizoea na kuendana na Game.
Mashabiki wa WCB wako very supportive sana na wana mapenzi ya kweli na label yao.

Ukiacha hivyo wasanii wao wana majina makubwa tayari hivyo hawatumii nguvu kubwa kupromote mziki wao.

Ukizungumzia trends na talk of the town bongo (Kiki za Mitandaoni)hawa jamaa ndo kwao kabisa hata wasipotoa nyimbo wanabaki kuongelewa na mashabiki muda wote kwa sababu ya drama zao za kimtandao.

Ni ngumu kwa label nyingine kushindana na hawa jamaa. Clouds Media na media nyingine zilijaribu kuua mziki wao kwa kuacha kupiga nyimbo zao Ila kwa nguvu ya mashabiki zao nyimbo zao zilikuwa zinapeta kitaani kama kawa watu walikuwa wana download na Ku stream Kama kawa.

Ukiangalia WCB iko full oriented sio Kama label nyingine Ina departments za kusimamia kila mahali
For instance
1.Social Media Department
2.Artists Managers
3.Directing Team
4.Music Department.

Lakini pia uanzishwaji wa kituo cha Wasafi Media umeongeza chachu na ufanisi kwa label kwa sababu kazi zao sasa zinapigwa bila masharti na kwa vyovyote vile mpenzi wa Wasafi Media asiye mpenzi wa WCB ataanza kuvutiwa nao tu.

Mwisho nimalizie kwa kutaja label nyingine ambazo binafsi naona bado zinatania katika uwekezaji
1.Kings Music(Alikiba)
2.Konde Music Worldwide (Harmonize)
3.African Princess(Nandy)

Hata hivyo hawa jamaa kwenye upande wa Ku shoot Video wako very serious ndo maana video zao zina quality na ni nzuri.

Wanajua kuimba nyimbo za miondoko yote Singeli,Mapenzi,Club Banger na wanatisha.Hakuna label itakuja kuifikia WCB kwa uwekezezaji walioufanya na kwa Hardworking spirit waliyonayo.

Kwanza jua Tanzania ina wanamuziki wengi sana, mno, wengiiii sana yaani

Tanzania kama dunia ya tatu bado wanamuziki wake wengi ni wadogo, wasafi media inamilikiwa na na mmiliki wa clouds (sema kwa ujinga wako haujui)

WCB sio muarobaini wa kuinua wanamuziki wengi kama clouds walivyofanya kwa miaka 20 iliyopita. Sasa hapo ndio tunasema akili ndio zinapoanzia

Wcb wanafanya vizuri sana, mno...lakini haiondoi ukweli kuwa uweze ku diss kuwa wengine wamewekeza kidogo.ndio uwezo wao halisia

Akina Rayvanny, lavalava wana mikoko gani ya maana unaijua? Wana nyumba gani za maana tusijue? Na kwa akili zako hauoni ni matangazo na kiki tu kuona wanazo nyingi?

Sijasikia diamond ana private jetty au nyumba ambayo DSM itashtuka!!! Haipo, tusingelala


So msifie diamond kwa mahaba yako, ila usidharau wengine

Uwekezaji mziki TZ ambao waliweza kutufukisha hapa ni clouds...ambao walifukuza wakongo wakavunja ngome za wahindi na kuleta taarabu na bongoflava.....hii ambao unaijua wewe!

Uwekezaji wa label TZ bado sana kwa label zote.

Unamfahamu Hamadai wewe? Kusah, ibrazoma? benson? Ndelah? Magic? Unamfahamu six one? Ukitaka kufaidi muziki na kujua nje ya box lako la wcb fuatilia hilo na weka strategy unawezaje kukusanya na kuwaweka sawa hawa wote

Diamond hata afanye nini hawezi mfikia Hamadai, six one, ndelah na wengine wengi...lakini ndie unamjua...ndio muziki ndio biashara sio? Lakini wewe kumjua na kumsifia diamond hakuwafanyi hawa wengine kuwa takataka

Nimeona unataja label nne tu, Tanzania we are rich of young and old artists...wengi mno, get time uwajue usipitwe na miziki yao mitamu

Ukiuliza kwa nini Ibrazoma hajulikani...utagundua kuna mengi ya kufanya kuliko kuwa na mahaba na wcb tu

Namalizia kwa kusema wcb ni label nzuri kwa jina ila bado haijafanikiwa kuwafanya members wake wafaidike nayo

Yaani inawezekana wewe unaipenda sana wcb kuliko rayvanny
 
Kiwango kikubwa sana cha copy and paste
120347875_188541896046343_7321852429850653732_n.jpg
 
Achana na hawa vijana chawa job less
Clouds wana nafasi kubwa mpka walipoufikisha mziki hapa.
Sasa hiyo kima inasema eti walitaka kuuwa mziki..!
Mbona wameshindwa kumfikisha Kiba walipo WCB licha ya kumpa support muda wote? Ifike mahala juhudi binafsi za mtu zikubalike.Na bado wanatumia nguvu kubwa sana kumshusha Mond Ila ndo hivyo wameshachelewa,juzi kimetoka hicho kijinyimbo Mediocre wamekipamba, wakamfanyia interview Kiba kumdhihaki Mond,bado unasema Wasafi ni mtoto wa Clouds 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom