WCB walipwa bilioni 2 na Universal music, TRA walamba mil 35

WCB walipwa bilioni 2 na Universal music, TRA walamba mil 35

kumbe ww ni bongo flavour


Hapana mi napiga guitar for fun tu. Na ukileta kifaa chochote cha muziki Bongo usifikiri utatumia peke yako, watu wengi wanatamani lakini hawana kwa kupata.
 
2 billion kodi 35 M (18,000$) Da ...hii ni asilimia ngapi???.huyu Nasibu aache majigambo ya kipuuzi
 
18% * 2,200,000,000 = 396,000,000 tsh. Jamaa kasema kalipa 35,000,000 ambayo ni sawa na
35,000,000/2,200,000,000 * 100 = 1.59%

Sasa mbona ushuru kalipa asilimia 1.59 tu ? Au ushuru ni asilimia ngapi kwani?

Msinirushie mawe hata sijabisha, nataka kufahamu tu
msiwe mnakurupa tu kujibu maswali mleta mada kaonganisha habari mbili tofauti

1 ni hiyo habari ya partnership kati ya wcb na universe

2 diamond amesema yy ndo msaa anaelipa kodi kubwa tra zaid ya 35mil

kwahyo hizo habari mbili tofauti

over
 
AMEFANYA VIZURI ILI KUONGEZA KIPATO
SEMA INABIDI NYIMBO ZINGINE AONGEZE KIINGEREZA NA KIFARANSA KWA VILE KISWAHILI TU HAITOSHI
 
Usipotoshe hapa diamond na WCB hawajasainiwa na Universal Music bali wameingia partnership tu, tena ni ya kusambaza music wao world wide.
Albam ya diamond(international albam) itakayotoka hivi karibuni itasambazwa na universal music
Duh kwaio jamaa anatoa album sio
 
Hongera zake Domo huo ndo mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine. Na wewe mwenye huu Uzi sio campany ni Company
 
Aiseee leo sichangii chochote kuhusu diamond nataka nimzungumzie ila vidole havitaki vimeshachoka
 
Hizo tarakimu ni Fix tupu.
Huwezi ukalipwa Bilioni 2, halafu kodi ikawa ni milioni 35. Yaani sawa na Asilimia 1.75%. Sio kwa utawala huu wa Magufuli.
Kiwango cha chini kabisa ambacho Diamond angepaswa kulipa kama Kodi ni shilingi milioni 360, ambayo ni sawa na 18%.

Kinyume chake ni kwamba, Diamond amekwepa Kodi, au kiasi halisi alicholipwa sio Bilioni 2 bali ni shilingi milioni 194.
 
Swala la kodi halikwepeki, siku ukiingia kwenye reli ya TRA huna ujanja lazima ulipe. Kuna siku niliingiza guitar jipya kutoka Sweden nikapigiwa mahesabu nikaambiwa nililipie laki nne mi mwenyewe nilichoka.
TRA wanaroho mbaya mkuu[emoji38],yaani Guitar tu hela yote hiyo?!
 
gari la million 10 unalipa kodi million 8 had tisa, iweje mkataba wa bilion 2 kod ilipwe 35m.
 
Yale yale
Mwenzao alisign na sony wakamdhihaki leo wao wameangukia kule kule
Hawajasaini mkataba wa kuwa chini ya Management!!!
Universal wamesaini kama Distributors wa kazi za WCB wasafi!!
Kuna tofauti kati ya Management na Distributors pekee mkuu tafadhali usikurupuke!!
 
Hawajasaini mkataba wa kuwa chini ya Management!!!
Universal wamesaini kama Distributors wa kazi za WCB wasafi!!
Kuna tofauti kati ya Management na Distributors pekee mkuu tafadhali usikurupuke!!
Of course
 
Back
Top Bottom