WCB walipwa bilioni 2 na Universal music, TRA walamba mil 35

WCB walipwa bilioni 2 na Universal music, TRA walamba mil 35

Walitakiwa kulipa kodi ya milioni 250, kuna wajanja wa tra hapo wameifuta kodi ya ongezeko La thamani na kuwakata ya corporate tax, inayotokana na faida...malipi ya VAT Hanna hapo?
 
18% * 2,200,000,000 = 396,000,000 tsh. Jamaa kasema kalipa 35,000,000 ambayo ni sawa na
35,000,000/2,200,000,000 * 100 = 1.59%

Sasa mbona ushuru kalipa asilimia 1.59 tu ? Au ushuru ni asilimia ngapi kwani?

Msinirushie mawe hata sijabisha, nataka kufahamu tu
Labda atakuwa analipa kodi kwa instalments
 
Watu kwa kukurupuka tu hamjambo! Afu kitu kama hukijui ni bora ukae kimya ufiche ujinga wako! kweli nimeamin sio kila jukwaa JF kuna great thinkers !
 
Kama unafanya biashara yenye turnover ya 20+ Million lazima uandae vitabu vya mahesabu na vikaguliwe na auditors. Hao wasafi wanafanya biashara mbalimbali, ni kampuni.. Na kama wamelipwa 2 Billion hapo lazima 18% iende TRA ambayo ni Millioni 360.. Sasa million 35 ndio tunashangaa hapo muamala umefanyikaje
Nakubaliana na wewe! ila ni vigumu kumwambia msanii aandae vitabu vinavyoonyesha shoo zake
kuna mawili either tra wakapoteza mapato kutokana na kutokuwa na uwazi katika makusanyo yatokanayo na muziki au wakampunja msanii
Ndio dhana iliyopo hapo
 
Hizo tarakimu ni Fix tupu.
Huwezi ukalipwa Bilioni 2, halafu kodi ikawa ni milioni 35. Yaani sawa na Asilimia 1.75%. Sio kwa utawala huu wa Magufuli.
Kiwango cha chini kabisa ambacho Diamond angepaswa kulipa kama Kodi ni shilingi milioni 360, ambayo ni sawa na 18%.

Kinyume chake ni kwamba, Diamond amekwepa Kodi, au kiasi halisi alicholipwa sio Bilioni 2 bali ni shilingi milioni 194.
Capital gain tax ni 25%... ndio kodi stahili
 
Wasafi wanapenda namba ila hawajui hesabu...
Ninachojua mwanatandale kila akitoa nyimbo lazima aje na busta za kiki.
 
AMEFANYA VIZURI ILI KUONGEZA KIPATO
SEMA INABIDI NYIMBO ZINGINE AONGEZE KIINGEREZA NA KIFARANSA KWA VILE KISWAHILI TU HAITOSHI
Mbona akina Lwambo Luanzo Makiadi, Kofi, Oliver Mtukuzi, etc wameimba kwa lugha zao za asili walitesa na wanatesa dunia nzima?
 
Dah....safi sana kwa uzalendo Dogo.... ongezea zaidi ...Na bata kula bongo hii hii[emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
kodi inategemea mkataba umesainiwa wapi, nikupe mfano tu kama walisaini Las Vegas serikali ya Bongo haina chake. Kwa hiyo usijifanye smart kwa vitu usivyovijua.
don't be ridiculous.

Ingekuwa hivyo watu wote duniani wangekuwa wanaenda Las Vegas kusaini mikataba yao ili ku vitiate sheria za mikataba ya nchini kwao. I mean, that right there is just a wild, dreadful illusion.
 
Shangaa wewe... VAT ni 18%, Income Tax 30%.. Sasa 2 billion kulipa 35 M yaani sawa na 2% ya alichoingiza sijui ni TRA ya wapi wamefanya huo upumbavu
Labda deal yote ina worth 2b. Lakini initial payment kodi yake ndio 35m. Ukisikia mtu kaingia mkataba na kampuni kama adidas wa $5m haina maana analipwa zote mara moja.
 
don't be ridiculous.

Ingekuwa hivyo watu wote duniani wangekuwa wanaenda Las Vegas kusaini mikataba yao ili ku vitiate sheria za mikataba ya nchini kwao. I mean, that right there is just a wild, dreadful illusion.


Bro Las Vegas nimetoa mfano Tu. Inawezekana ikawa mahali kwingine tofauti na kama utaki sikulazimishi lakini ukweli Ni kwamba kodi inalipwa pale kazi zinapofanyika.

Na Ni hivi watu wengi wanataka mikataba isainiwe kwenye nchi zao ili watu wao wafaidike. Mfano Ni Usain Bolt ameamua mikataba ya wadhanini na advertisements zote zifanyike Jamaica kwa sasa ili kodi zilipwe nyumbani kwao.
 
Back
Top Bottom