Miaka michache nyuma kuna siku nilikuwa namsikiliza Guru, rapper wa Gangstarr alikuwa anahojiwa.
Mtangazaji baada ya kumuhoji akamuuliza. Nimesikia una beef na Fifty Cent, tueleze kuhusu hiyo beef.
Guru akawa kama kashangaa, akasema beef gani? Mimi na Fifty tuko poa tu, hatuna beef. Namuheshimu sana Fifty, anafanya kazi nzuri etc.
Guru anavyokandya kwenye nyimbo zake nilikuwa nafikiri angemtukana Fifty.
Na angemtukana ingezia bonge la beef.
Lakini alijionesha kwamba yeye ni OG anayejua "Code of The Street".
Kwanza si kila beef lazima itangazwe na ikuzwe. Kuna vibeef vingine wadau wanakaa chini na kuvimaliza mtaani tu.
Pili hata kama wewe ni OG kiasi gani au matawi kivipi, inakubidi kujua kuishi na watu strategically ili usijiharibie kazi.
Tangu siku hiyo nikamuangalia Guru kuwa si OG tu, bali nibsavvy businesman pia.
Tatizo kibongobongo mtu akishafika level fulani anaona kashamaliza kila kitu.