Ndoa haina shida. Shida ni wanawake wa kisasa waliokosa mafunzo nyeti ya utumishi wa ndoa na kuitunza. Wanawake wa sasa ni material oriented na bila mali wanaona ndoa ni adhabu na mzigo kwao sababu wanazingatia maokoto.
Wanaume kwa muda mrefu wamechagua wao kwa hiyari yao kuwa ng'ombe wa kafara na matokeo yake ni kufa na kuteketea kama karatasi juu ya moto.
Watoto wa kiume hawaoni maisha nje ya mahusiano na mwanamke/ndoa/uchumba/mahusiano. Kijana wa wastani mpatie milioni 10 kama zawadi bila masharti yoyote ya namna ataitumia. Baada ya muda utagundua ameiwekeza kwenye mahusiano na mwanamke kwa namna ambayo hiyo pesa haitarudi hata mia. Mpe mtoto wa kike hata million 100, atatumia kidogo sana kwenye mahusiano na ataidai irudi kama sehemu ya uwekezaji wa kibiashara na sio upendo kama wa mwanaume.
Hii ni matokeo ya msisitIzo wa muda mrefu na upotoshaji ambao jamii imekuwa ikiubeba vichwani na kurithisha vijana na mabinti kuamini mwanaume pekee ndie anatakakiwa kurisk na kutoa vyake hadi senti ya mwisho hata kama hana. Asipofanya hivyo basi sio mwanaume kamili matokeo yake vijana wa kisasa wanaendesha maisha yao na huu upuuzi vichwani. Mtu hana hela anafosi kuazima gari aonekane yupo vema, anakutana na binti anabidi kupretend kuishi kwa madeni ili kumfurahisha mtu ambaye lolote likimkuta hatoweza endelea nae.
Mapenzi/ndoa/uchumba ni investment kama zinginezo tu,unachowekeza kinatakiwa kuzalishwa na kukua na kuletea mafanikio kwako kama kiongozi na sio kuburutwa na mtu kihisia.
Vijana wabadili priority. Hili pori /msitu wa miaka 20 hadi 50 unatakiwa kuendesha kwa mipango yako binafsi na kwa kujiamini,ndivyo ilivyokuwa miaka ya uanaume ambapo wanaume walikuwa na kidali cha maamuzi na sio wasasa kazi kulia lia na kuomba kuonewa huruma na wanawake ambao kwanza hawajajitunza,miili ni used,hawana bikra,adabu zero,hawatambui mamlaka ya kiume kwenye maisha yao,viburi, ujuaji, wafujaji wa pesa na mali za mwanaume wake,hawana huruma,nyumba za ibada wanakwenda kuzuga tu ila hawamtambui MUNGU kwa namna yoyote, hawa sio sampuli ya kukufanya ukose muelekeo.
Ule wakati unahisi kuchanganyikiwa,hofu,upweke,wasi wasi, na kukosa uelekeo wa maisha ndio tafsiri halisi ya kusimama mwenyewe,yaani ndio muda vijana wengi hukimbilia mapenzi kama sababu ya kuishi (purpose) na kuzika akili,mali,fikra,vipaji walivyopewa na MUNGU na kila kitu huko matokeo yake ni mwisho wao hutokea mara tu uzee ukiwafika.
Vijana wengi wanaamini wakishaoa then kilichobakia ni kuzeeka na kusubiria kuitwa babu na wajukuu kumbe muda huo mwanamke anapanga mawili ni aidha ufe umuachie kila kitu, hutaki then ufyate yeye ashike hatamu na rasilimali zote wakiwamo watoto. Matokeo yake mwanaume anakuwa kama ng'ombe tu,kuzunguka zunguka bila plan hatimae magonjwa ya utu uzima yanamuwahi sababu ya kukosa utulivu wa mwili na akili.
Rekebisheni hii life style vijana. Ukiwa umri huo wa miaka 15 ingia YouTube na kwenye website jifunze namna ya kufanys biashara na kuhifadhi pesa zako. Mwanamke akija muonyeshe hela zako ila akizitaka then yupo entitled kushare na wewe 10% ya pesa tena mnatumia nyote. Akija usimkubali akileta uvivu bali kaa nae kimkakati yaani awe investment kwako kama Msaidizi.
Akikushauri pokea ila usimuachie awe na final say. Ni heri kuanzisha jambo kwa fikra zako na likafeli kuliko kupokea ushauri wa mwanamke halafu jambo likafanikiwa,utafurahia mwanzoni na mtasheherekea subiria huko mbeleni kitakachokutokea hadi utatamani urudishe siku nyuma umwambie mama ,naomba ushauri wako kaa nao ni mzuri ila wacha tufanye hili langu,likifeli hasara ni yangu. Hayati Reginald Mengi na matajiri wa Marekani Jeff Bezos na Bill gates wamepitia hii kitu na wamejifunza kwa gharama kubwa sana.