Weka aya/ mstari kutoka kitabu cha dini yako unaoona umeandikwa kwa ustadi, weledi na hekima ya hali ya juu

1YOHANA 4:1 Wapenzi, msiamini kila Roho bali zijaribuni hizo Roho kama zimetokana na Mungu; kwasababu Manabii wengi wa uongo wametokea duniani
 
Hii verse chini napenda kusoma nikipata feelings za ukatili na unyama sababu inanitaka nisiache kitu niangamize watoto ,wanyama mpaka vichanga ni destroy completely kusiwepo hata chembe ya alama yao.View attachment 2657194
Sasa umeambiwa uwaangamize waamaleki...Waamaleki wako wapi?
 
Sasa umeambiwa uwaangamize waamaleki...Waamaleki wako wapi?
Kwani nimesema naangamiza watu ? kuna wakati mtu unapata feelings za ukatili ukiweka na hiyo aya unakuwa mzuka unapanda zaidi ya mvuta ganja akiwa anavuta.

Napenda kuuliza Waamaleki hawakuwa watu ? mpaka itoke amri kama hiyo pengine ni ya kikatili zaidi kuwahi kutokea kwani inajumulisha vichanga ,watoto ,wanawake mpaka wanyama
 
Yeremia 29:11
Kwa maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi,ni mawazo ya amani na si ya mabaya ,kuwapa ninyi tumaini hata siku zenu za mwisho.
 
QURAN 78 An-nabai
31.Hakika wachamungu wanastahiki kufuzu
32.Mabustani na mizabibu
33.Na wake waliolingana nao
34.Na bilauri zilizojaa
35.Hawatasikia humo upuuzi wala uongo
 
Thanks
 
Zaburi ya 20 yote..


Yoshua1:5

Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha
 
Mithali ngap sijui
Yote ni ubatili mtupu ni sawa na kutafuna upepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…