Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Karibuni wadau wote wa michezo kutabiri matokeo ya huu mchezo wa marudiano kati ya hizi timu mbili kubwa kabisa Barani Afrika; Raja Casablanca ya Morocco vs Simba ya Tanzania.
Ikumbukwe timu zote mbili tayari zimeshafuzu hatua inayofuata ya robo fainali, Kombe la Klabu Bingwa Afrika. Na katika mechi zao za mwisho kucheza, Simba akiwa nyumbani, aliifunga Horoya goli 7-0! Huku Raja Casablanca akiwa ugenini Uganda, alipata sare ya 1-1 na wenyeji Vipers.
Kwa nini nimechukua nafasi hii nyeti kabisa kuwakaribisha wadau wenzangu wa michezo, kubashiri huu mchezo? Ni kutokana na kiwango bora kabisa walichokionesha Raja Casablanca tangu mwanzo kwenye hii hatua ya makundi, kiasi cha kutopoteza mchezo wao hata mmoja mpaka sasa. (Na ndiyo wamebiwa na hii mechi ya mwisho dhidi ya Simba)
Lakini sababu ya pili imetokana na kiwango walichokionesha Simba siku za hivi karibuni dhidi ya wapinzani wake kwenye haya mashindano! Mfano Simba ilimfunga Vipers nyumbani na ugenini, halafu ikamfunga tena Horoya goli 7-0 pale kwa Mkapa! Imgine Tripple C alipiga hat trick! Putin akapiga 2! Baleke naye akapiga 2!! What a performance!
Nisiwapotezee muda! Binafsi utabiri wangu unaenda kwa simba! Naamini kwenye hiyo mechi yao ya marudio kule Morocco, watampiga Mwarabu goli 3-0 katika uwanja wake wa nyumbani. Yaani kama walifanya Yanga vile kwa ile Club Africains ya Tunisia. Na wafungaji wa hayo magoli kama kawaida; watakuwa ni Chama, Baleke na Kibu D.
Vipi na wewe kuhusu utabiri wako? Na ifahamike pia unapobashiri, kuna kupatia! Lakini pia kuna kuchanika kwa mkeka. Hivyo asitokee mtu baadaye wa kuja kumkamata mwenzake uchawi hapa! Nadhani wazee wa mikeka wamenielewa vizuri.
Nani ni nani kati ya Raja Casablanca vs Simba wiki kadhaa kutoka sasa?
Karibuni wadau wenzangu wote wa mpira wa miguu.