Weka utabiri wako hapa wa mechi ya marudiano wiki chache zijazo kati Raja Casablanca ya Morocco vs Simba ya Tanzania

Weka utabiri wako hapa wa mechi ya marudiano wiki chache zijazo kati Raja Casablanca ya Morocco vs Simba ya Tanzania

Mimi naona Simba ikienda kule kwa lengo la kutaka sare wanaweza kuipata, lakini kama wanaenda kwa ajili ya kusaka alama 3, RAJA watathibitisha kile walichokifanya kwa Mkapa au hata na kutoa nyongeza.
 
Simba haijawahi kufungwa hata nusu ya hizo goli na timu yoyote ile hapa duniani. Lakini naheshimu utabiri wako.
Tusaidie kidogo hapo hesabu. NUSU ya goli 13 ndio goli ngapi hizo?
6
6.5
au 7?
Kama ni 6.5 tusaidie kujua Hilo goli 0.5 linapatikana vipi.
 
6 na 7 ndiyo majibu sahihi.
Basi kama ni hivyo ni sawa. Ila kwa kuweka kumbukumbu sawa Simba wameshawahi kufungwa hizo goli 6 ila sio kwa bila ni 6-1 kwenye mechi za kirafiki.
1981 timu moja ikiitwa Dynamo kutoka USSR ilikuja kucheza na bingwa wa Tanzania (Simba) ubingwa alioupata mwaka 1980 halafu akapangiwa kucheza na bingwa wa Zanzibar (KMKM) katika Uwanja wa Amaan. Dynamo alitoa dozi sawa sawa na aliyoitoa kwa Simba. Bahati nzuri hii ya Amaan nilikuwepo kule upande wa jukwaa la Urusi.
 
Mbona unachanganya madesa!! Raja anacheza na Makolo! Utopolo atakuwa ana jambo lake dhidi ya timu kubwa kabisa Barani Afrika; Tp Mazembe kule DRC.
Mazembe hawa waliofungwq na kutoleqa vipers(wababe wa utopolo)club bingwa na kuja kucheza kombe la maluza na utopwinyo? Hauko siriaz mgosi
 
Simba itumie mchezo huo kuzifanyia mazoezi combinations nzuri tactics kuelekea mchezo wao wa robo fainali - hata kama Simba itapoteza thats fine lakini waangalie na kuufanyika mazoezi mfumo watakaocheza robo fainali maana watakuwa washajua uwezekano wa mpinzani mmoja kati ya 2.
 
Simba hana cha kupoteza, kwa hiyo haitawaheshimu Raja na watashambulia mwanzo mwisho na Raja hataamini macho yake: Raja 0 - 4 Simba!!
 
Naona siku zinazidi tu kukaribia......!!!
 
Wajumbe wenzangu, hayawi hayawi, sasa yamekuwa. Utabiri wenu ni muhimu!

Je, simba atatoboa kweli kuchezeshwa saa nne usiku (saa 7 usiku kwa masaa yetu), na katika yake mazingira hatarishi ya baridi kali?

Huu uzi utafikia hitimisho usiku wa leo, na hivyo kama hujatabiri, basi unakaribishwa kuwa mtabiri. Mshindi atatangazwa kesho panapo majaliwa.
 
Back
Top Bottom