Wekeza kwenye kilimo cha miti ya mbao PINE

ya mufindi

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2014
Posts
569
Reaction score
888
Ni uwekezaji mzuri, kama umeweka pesa Bank kwenye Fixed Account. Mfano huku mufindi ekari moja utainunua kwa Tsh. 900000 amoja na ardhi miti ikiwa na miaka 6. So, hekari moja ina miti 600 baada ya miaka minne ijayo kila mti utauuza wastani Tsh. 7000.

600*7000=4200000 kila hekari na unapanda tena.

Njoo uwekeze
0716101434

Picha hazitaki ku-upload
 
Kwa hesabu yako sidhani kama inalipa....

mapato baada ya miaka minne 4.2M ; mapato ukigawa kwa kila mwaka 1m..,
Gharama umeweka laki tisa tu ya kununua sidhani kama hakuna gharama nyingine..
 
Kwa hesabu yako sidhani kama inalipa....

mapato baada ya miaka minne 4.2M ; mapato ukigawa kwa kila mwaka 1m..,
Gharama umeweka laki tisa tu ya kununua sidhani kama hakuna gharama nyingine..
Kuna kazi ya kulisafisha shamba (ku pluni miti) kila mwaka, hapo bado majanga ya moto
 
Mufindi kubwa! Hayo mashamba yanapatikana maeneo gani? Mapanda, Ihanu, Ifwagi, Sawala, Luhunga, Mdabulo, Bumilayinga, Kibao, Itona.

Na vipi kuhusu historia ya moto kwenye hayo maeneo? Maana huo mti wa pine ukishika tu moto hugeuka kuwa petroli! Bora hata ya mlingoti.
 
mashamba yapo kilosa kata ya ihanu moto siku hizi hakuna
 
mashamba yapo kilosa kata ya ihanu moto siku hizi hakuna
 
Hizi hesabu za kwenye makaratasi ni nzuri sana...
Tafadhali tufahamishe kuna risk gani kubwa kwenye hii biashara maana watu wasiingie kwenye biashara wakiwa na positive thought tu.
mkuu risk kubwa ni moto tu japo kwa sasa sio janga kutokana na elimu na patrol ya vikosi vya sao hill japo mwaka jana binafsi niliunguliwa na ekari44
 
Hizi hesabu za kwenye makaratasi ni nzuri sana...

Tafadhali tufahamishe kuna risk gani kubwa kwenye hii biashara maana watu wasiingie kwenye biashara wakiwa na positive thought tu.
Kuchomewa moto
 
Kati ya pine, bodo bodo na mikaratusi ipi yenye soko zuri? Kwann wengi hawapandi mikaratusi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…