Wekeza kwenye kilimo cha miti ya mbao PINE

Kwa anataka pwani kwa ajili ya kulima miti ya mitiki, shamba lipo ,ekari moja 200000, zipo eka 30
 
mzee hesabu ni simple na faida ni zaidi ya hiyo sema siyo vizuri kuwataja watu wakubwa waliowekeza kwenye miti huku mufindi nikikupa mifano unaweza usiku huu ukafunga safari kuja kuwekeza mkuu
Ha ha ha ha ha atatoka usik kuja kuwekeza
 
Nimeambiwa kuwa pine huharibu rutuba ya ardhi. Je, ni kweli?
Pine ndiyo huleta rutuba sana kwenye shamba na ndio maana tukivuna msimu huo tunapanda mahindi,ulezi au maharage hustawi sana then tunarudishia miti mfano ukipita hapa sao hill utaona sehemu ilyovunwa miti kumepandwa mahindi alikwambia kakudanganya.
 
Mkuu umefafanua vizuri japo mie sio kishoka wala dalali nikikusimulia nimeanza kupanda miti yangu kwa mkono wangu tangu nikiwa darasa la sita mwaka2004 sasa kila mwaka nikawà napanda ekari moja nimeanza sekondari miti bado midogo kwanini nisiuze kwa bei ndogo nijisomeshe haya chuo nako mahitaji kibao kwanini nisiuze bei ndogo ili nijikwamue so kuuza kwa bei ndogo ni kwasababu ya ugumu wa maisha
lakin in all ufafanuzi wako mzuri karibu sana mufindi
 
Mkuu kumbe uko gharama za viwanja zina nafuu mno. Hongereni wenye nafasi hizo
Mkuu karibu hii ni fursa kwa wote nchi ni yetu sote watu wengi wa kandà ya ziwa wamewekeza huku ndo maana kitakwimu wilaya hii mufindi ni ya pili kimapato kwa taifa karibu.
 
Mwandiko wako vs chuo

Haviendani kabisa.

Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
 
Nimetoka kilolo kijiji cha masisiwe mti mmoja unafaa kuvunwa unauzwa sh 2,500 nilikua na ekar 4 zangu nilinunua 2010. Kwa bei hiyo nimetamani hata kuichoma moto. Kama una wanunuzi wa sh 10,000 njoo pm ekari 4 zipo vizuri unatoa mpaka mbao za 8
 
Kwangu pm haitaki hebu ni pm tuongee
 
Mti mmoja 7000?! Uzuri miti ya mbao siyo kama matunda, tutauza hate awamu ya 6
 
Mti mmoja 7000?! Uzuri miti ya mbao siyo kama matunda, tutauza hate awamu ya 6
Uzuri wake ndo huo unauza ukipenda ubaya unakuja ukiuguliwa,ada ya watoto shule,kujenga nk lazima uuze kwa hasara
 
Naomba Mungu anisaidie yasinikute yote hayo aisee......
mungu ndio wa kwanza nikikusimulia nilivounguliwa miti mara mbili,utakata tamaa ila ....mara ya mwisho nilitusua
 
nielekeze umenunua sehem gan miti yako
Mimi siyo mkongwe, kuna ndugu yangu yupo huko muda mrefu siwezi kumtaja hapa. Amenichukulia miti huko mwaka Jana, sijapata nafasi ya kufika huko, nategemea kufika mwakani.
 
Mimi siyo mkongwe, kuna ndugu yangu yupo huko muda mrefu siwezi kumtaja hapa. Amenichukulia miti huko mwaka Jana, sijapata nafasi ya kufika huko, nategemea kufika mwakani.
Bila shaka ni mapanda kikubwa imani nitakuelekeza jins ya kukinga majanga ya moto kwa gharama ndogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…