Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Horoya kwa namna wanavyocheza ilikuwa halali wapigwe nyingi, kwanza hawakumuheshimu mpinzani ambaye yuko nyumbani kwake, wameingia kwenye mchezo wakafunguka kuanzia dk ya kwanza ya mchezo, na hapo hapo wakashindwa kujielewa kwamba sio wazuri ni timu ya kawaida sana ambayo nafikiri bado wanajitafuta ili kurudi kwenye ule ubora waliokuwa nao misimu miwili iliyopita ambapo waliuza wachezaji wengi sana na kuacha wengi pia.
Sasa unapokutana na timu kama hii basi zitumie nafasi unazopata kiuhakika na ndicho walichofanya simba leo, kujisifu sana pia dhidi ya timu kama hii napo sio sahihi sana, unaweza ukajiona bora kumbe uliyekutana nae pia ni garasa.
Hongereni jiandaeni vizuri dhidi ya wanaokuja kwenu ambao sio tena horoya bali ni timu haswaaa.