Wema aanika sababu za kummwaga Diamond

Wema aanika sababu za kummwaga Diamond

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Miss Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye', amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz'.

Akizungumza na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati, Wema alianza kwa kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu ya yeye kumtema Diamond huku kisa wakiwa hawakijui na wengine wamehamishia sababu kwa nyota wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari', jambo ambalo si kweli.

Wema alimwaga ‘ubuyu' kwamba, yeye ameamua kumpa likizo ndefu Diamond ili kila mmoja aweze kufanya mambo yake ya maana kwa uhuru mkubwa hasa baada ya jamaa huyo kunukuliwa na magazeti pendwa akisema hana mpango wa kuoa jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kumwacha njia panda.

SAFARI YAKE CHINA NAYO TATIZO:
Kuhusu suala la kusema amempa likizo ndefu ili kila mtu afanye mambo yake, Wema alirejea safari yake ya China hivi karibuni ambapo Diamond hakutaka asafiri ila akalazimisha. Hapo aliona anatakiwa kuwa huru zaidi.

MWISHO WA LIKIZO:
Wema alipotakiwa kutaja mwisho wa likizo hiyo endapo ni ya siku 28 kama ilivyo kwa sheria ya kazi ya Tanzania, aligoma kusema chochote huku akisisitiza amempa likizo Diamond.

AMZUNGUMZIA ZARI:
Staa huyo asiyekaukiwa na matukio, alikwenda mbele zaidi kwa kumzungumzia Zari ambapo alisema kuna wanaodai mwanamuziki huyo tajiri yuko kimapenzi na Diamond, lakini yeye haoni ukweli wowote kwani anajua wawili hao wana ‘projekti' ambayo ni mawazo ya muda mrefu.

BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA:
"Kwanza naomba watu wajue kuwa, projekti ya Diamond na Zari ninaijua na bahati nzuri Zari ni shoga‘ngu tangu kitambo hivyo yote yanayofanyika mimi nayatambua hatua kwa hatua pamoja na kwamba sijaongea na Diamond siku nyingi," alisema Wema.

DIAMOND AULIZWA KAMA ANAITAMBUA LIKIZO NDEFU:
Baada ya mazungumzo na Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond kwa lengo la kutaka kumfahamisha kama anafahamu kwamba amepewa likizo ndefu. "Dah! Nashindwa niseme nini hapo! Lakini ujue maisha kila mfa maji siku zote haishi kutapatapa, kiukweli mimi hapo naona Wema anatoa majibu ya kisiasa tu.

Nashindwa kujibu kila linalosemwa na watu ila kuna kipindi mtu hutakiwi kujibu kila kitu. Kuna mambo mengine yanatakiwa uyaache yapite tu.
"Mimi nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee," alisema Diamond huku akichekacheka kwa ishara ya furaha akijiandaa kuachia ngoma kali mpya iitwayo ‘Nitampata Wapi' leo.

KWENYE WHATSAPP:
Wakati Diamond akisema hayo, baadaye kwenye maelezo yake mafupi (profile) ya WhatsApp aliweka picha ya Zari huku akiambatanisha na maneno yaliyosomeka:

"Unapokosa usisikitike, Mwenyezi Mungu kakuandalia kizuri zaidi."

Wema na Diamond wamekuwa na kasumba ya kuachana na kurudiana hivyo kuna kila dalili wawili hao wakarudiana tena.

Chanzo: GPL
 
Attachments

  • 1416463023368.jpg
    1416463023368.jpg
    69.4 KB · Views: 6,546
Mama ubaya unavyojitahid kukanusha zari hatoki na ndomo ,kumbe roho inauma eeh? Maana unajua zari humpati kwa lolote, Ila hata mimi naona hakuna kitu kati ya ndomo na zari ni upambe tu kama mama ubaya alivyosema, halafu kumbe nyie mnapendana maana kila mtu anatoa maelezo nusu nusu mara mmepeana likizo mara huyu nae mfamaji aishi kutapa tapa, mbwa nyie mnatufanya sie matukunyunyu
 
Heeeeeee wema lini ushakua na ushoga na zari hheloooooi ashakua shoga yako au ndo unataka uwe mbeba pochi niniii
Hilo paja wema sio la kuacha nje tena uwe unalifunika tu halivutiii
Diamond baba bado mdogo na una akili sana huwezi oa gume gume la mjini wa kuolewa sio wema aolewe na club tu na pombe
Dai umejibu vizuriii
 
Ebu nisaidie kushangaa, huo ushoga umeanza lini? Namuonaga anavyojishaua kupost kwenye insta ya zari manina kumbe zari ndo kiboko yake nfyuu, eti shoga ake, na aunty ezekiel cheus dawa kamwachia nani?
 
Unanichosha bhna, we una quote maneno yote hayo, halafu thread na comment hata havihusiani..

Kuhusu ban kuisha waulize ma mods, maana wao ndo wanakumbu kumbu nzuri..

Hhhhhhaaaa binam hujanywa chai nini heeeeeeeeeee, ,akawaulize mods wana kumbukumbu nzuri jibu zuriii
 
Yani sanaaa ya bongo kizunguzungu ukiona kuna tukio tu basi nyimbo mpya inakuja hii sio nzuri kwenye kukuza sanaa kutengemea tukio ndio kitu kifanyike
 
Ebu nisaidie kushangaa, huo ushoga umeanza lini? Namuonaga anavyojishaua kupost kwenye insta ya zari manina kumbe zari ndo kiboko yake nfyuu, eti shoga ake, na aunty ezekiel cheus dawa kamwachia nani?

Atajipendekezaaaa mnooo alitafutwa sinta tu heeee ye aendeleee na rafiki zake wacheza vigodoro ndo hadhi yakeeeee
Tukikutwa na Mrembo by Nature tunalooo naomba leo asije humu tumchambe kabisa madam wa ke
 
Last edited by a moderator:
warumi

Nakuambia Dai mjanja hataki kumuoa wema, angekua ashamuoa mbonaaa
 
Last edited by a moderator:
Hhhhhhaaaa binam hujanywa chai nini heeeeeeeeeee, ,akawaulize mods wana kumbukumbu nzuri jibu zuriii

Mi mambo ya ban ananiuliza ntajulia wapi? Anipishe mi aniambie wema kamuacha ndomo lini nitamtajia tarehe mwezi had siku mengine akaulize uko mtaa wa pili
 
Atajipendekezaaaa mnooo alitafutwa sinta tu heeee ye aendeleee na rafiki zake wacheza vigodoro ndo hadhi yakeeeee
Tukikutwa na Mrembo by Nature tunalooo naomba leo asije humu tumchambe kabisa madam wa ke

Mrembo by Nature aje tu kwa kweli labda atakuwa anaujua vizur ushoga wa wema na zari maana izi habar kwangu ni breaking news kama sio exclusive looh!! Sio kujipendekeza uku eti zari shoga angu, warumi alivyokuwa mbea si angeshajua, we ngoja sintah amsikie atakoma vichambo vyake
 
Last edited by a moderator:
Ila wanaume hawa daaaa lazima ukae yani zali anakula maisha na domo afu wema........... Afu ......
 
Mama ubaya unavyojitahid kukanusha zari hatoki na ndomo ,kumbe roho inauma eeh? Maana unajua zari humpati kwa lolote, Ila hata mimi naona hakuna kitu kati ya ndomo na zari ni upambe tu kama mama ubaya alivyosema, halafu kumbe nyie mnapendana maana kila mtu anatoa maelezo nusu nusu mara mmepeana likizo mara huyu nae mfamaji aishi kutapa tapa, mbwa nyie mnatufanya sie matukunyunyu

Wanapendana vip wakat wema hajiamini kabisa kwa domo yani hapo wema hana ngao kabisaaaaaaa natabir hata warudiane hakunaga ndoa hapo
 
Back
Top Bottom