Wema amenishangaza kwa kauli ya "yeye na uzungu wake"

Wema amenishangaza kwa kauli ya "yeye na uzungu wake"

Habarini Wadau,

Usiku huu katika taarifa ya habari ya TV1, habari ikielezea uhamasishaji wa wasanii kuupa kipaumbele miziki yenye mahadhi ya uswahili kama segere na singeli nimemsikia Wema Sepetu akihojiwa na kuzungumza haya:-

"Mimi pamoja na uzungu wangu lakini huwa napenda nyimbo zenye uswahili kama hizi"

Kwa aliyeelewa vizuri hiyo kauli ya Wema ilimaanisha nini? Wema ni Mzungu?

Nawasilisha.
hahahahahhaha. nasubiri majibu tujue huo uzungu. lolmfao
 
Ahahahahaaaa yeah right!

Huu ndo 'Uzungu' wake.

Hebu yasikieni hayo matusi ya 'Mzungu'.

'Mzungu' in action...

😀😀😀😀

hahaha nacheka sna aisee. eti uzungu wke ndo huo?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwanza sikutaka kuamini masikio yangu juu ya kile nilichokisikia. nikamuuliza mwenzangu,
"Eti Wema amesemaje?"
"Amesema yeye pamoja na uzungu wake wote bado anapenda mambo ya uswahili kama yale...."
Nikasema hapana kwa kuwa hii tv ni ya zamani itakuwa imeanza kutupa habari zisizo za kweli.
Sasa saa hizi nimeingia humu nimeikuta tena hii habari, kwanza nikatikisa kichwa kwa dharau halafu ghafla nikakumbuka huyu amewahi kutaka kugombea ubunge kupitia CCM na alipita kila mkoa kumnadi Mr Alcohol... "Sio ajabu hawa ndio tuliochagua kuwakabidhi nchi yetu eti wamesema wataifanya iwe ya viwanda hahahahahah."
hahahhaha. zero brain ni tatzo kbwa nchi ytu.
 
Watu wanaohusisha ustaarabu au tabia fulani fulani na Uzungu ni wazi hawajaishi na Wazungu kwa muda mrefu.

Kwa sababu, kwa mtu yeyote aliyeishi na Wazungu kwa muda mrefu basi lazima atakuwa anajua kuwa hata wao wapo wengi tu wenye tabia za ajabu ajabu kama uhasidi, upekepeke, umbeya, uasherati, na kadhalika.

Hebu ona hawa Wazungu wanavyosutana na kurushiana ngumi halafu nambie wana tofauti gani na watu wengine..

Wenyewe watakuambia hizo ni swaga...
Ngozi nyeusi kila kitu ni kizuri kwake ilimradi hicho kitu awe kakifanya mzungu.
 
Labda nitakuwa tofauti maana mimi nashangazwa na watu ambao bado wanashangazwa na huyu kiumbe kiukweli hajitambui
 
Watu wanaohusisha ustaarabu au tabia fulani fulani na Uzungu ni wazi hawajaishi na Wazungu kwa muda mrefu.

Kwa sababu, kwa mtu yeyote aliyeishi na Wazungu kwa muda mrefu basi lazima atakuwa anajua kuwa hata wao wapo wengi tu wenye tabia za ajabu ajabu kama uhasidi, upekepeke, umbeya, uasherati, na kadhalika.

Hebu ona hawa Wazungu wanavyosutana na kurushiana ngumi halafu nambie wana tofauti gani na watu wengine..

Hahah mkuu,nlivyoona hayo ma trucks tu nikajua watakuwa wale mnaowaita ma rednecks,wazungu waswazi.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Huo sio 'uzungu'?

Au yeye anazungumzia uzungu upi labda?

Mwisho wa siku ujinga bado ni adui mkubwa kwenye jamii yetu.
Mkuu yeye wala sio wakumlaumu sana mana hana alijuwalo,wakuwalaumu ni wale walomfanya awe supastaa na role model wa mabinti wa skuiz
 
Back
Top Bottom