Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amempa onyo kali Juma Lokole akitaka aache kumzungumzia vibaya baba mtoto wake, Whozu, akidai tabia hiyo imeanza muda mrefu.
"Heshima ni kitu cha bure sana kwenye maisha ya kila binadamu. Kuna jambo linanikwaza sana, na nimekuwa nikiliona mara kwa mara kwako Juma Lokole.
"Nimekuwa nikilifumbia macho kwa muda mrefu, lakini nimefika mahali ambapo siwezi tena kuendelea kukaa kimya.
"Juma, tayari nimeshajua humkubali baba wa mtoto wangu. Sio hivyo tu, umekuwa ukitoa maneno ya kumdhihaki kila iitwayo leo. Sipendi kabisa jambo hilo.
"Wewe unamuona wa nini? Mwenzio ndiye aliyeniheshimisha na kunifanya leo hii niwe mama. Sasa basi, kama huwezi kumzungumzia kwa wema, basi si lazima umzungumzie kabisa.
"Sipendezewi hata kidogo ninapopita kwenye ukurasa wako na kukuta fedheha juu yake. Ifike mahali tuheshimiane, hata kama ni kwa kujifanya, kwa ajili ya vizazi vyetu.
"Nimekuwekea maoni kwenye chapisho lako, lakini naona uliamua kuyafuta. I'm serious this time.
"Kama nimekuvumilia kipindi cha nyuma nilipokuwa Wema Sepetu, sasa hivi uvumilivu umenishinda kama Mama Ollie. Acha tabia yako hiyo! Siipendi kabisa!.
"Utasema kuna kitu amekufanyia, au unatumwa? Sio vizuri. Sitaki kabisa kumwona baba wa mtoto wangu akidhalilishwa.
"Sitaki! Vinaumiza, vinakwaza, vinakera!. If you can't say something positive, you'd rather not say anything at all. I hope you understand me," - Wema Sepetu.