Nilikuwa masikini sana nikakosa hata nafasi ya kuendelea na masomo,hii ilitokana na umasikini wa wazazi wangu pia.
Baada ya miaka kadhaa nilijiingiza kwenye kilimo cha viazi pale njombe,Hakika Mungu huwa hamtupi mjawake nilipata mafanikio makubwa sana,maisha yangu yalibadirika sana.
Baada ya mwaka mmoja niliamua kujiingiza kwenye biashara ya mbao,sasa hapa ndipo shida ilipoanzia.
Nilipo fanikiwa zaidi niliambiwa natumia uchawi.Nilipokuwa sina kitu nilichekwa sana,nilipoendelea kufanikiwa zaidi na zaidi wakasema Mimi Freemasons ila sasa maneno yanayowatoka nikuwa ni muuzaji wa dawa za kulevya.
Kumbuka nimeanza kilimo 1997_2003 baada ya hapo nikajiingiza kwenye biashara ya mbao.
Swali langu kwenu Watanzania kipi mwanadam akifanye ili muone mafanikio anayoyapata ni ya halali?
Hakika watanzania wana hila mbaya na asilimia kubwa kuiona pepo itakuwa ni ngumu.
Jamani tufanye kazi kwa bidii,tuache mijadala isiyokuwa na tija mitandaoni.Kila siku kujadiri watu na Mali zao huu ni upunguani kwa kutupwa.
Asanteni sana