Wema Sepetu na maadili ya runinga zetu

Wema Sepetu na maadili ya runinga zetu

Kwani vijana ndiyo wanaruhusiwa kuangalia watu wanaoenda uchi wa nyama, umetukosea sana sisi vijana

Kama mnajifanya kukasirika iweje mtembee uchi wake kwa waume? Utamkuta binti amevaa sketi fupi mapaja yote yapo nje au amevaa suruali hadi ngozi yake ya ndani inaoneka au matiti yameachwa wazi, kijana wa kuime anavalia suruali mapajani kiuno chote unakutakimefunikwa na chupi sasa tukiwasema mnakasirika nini?
 
kipindi kinaitwa WEMA SEPETU - UNDER MY SHOES. Wema pamoja na mambo mengine anaonekana akiwa uchi anapiga picha. hata kama uchi wenyewe umefichwa kwa majani, na wakati anatembea maziwa nje picha zinafichwafichwa kwa computer lakini haizuii content kwamba wema anatembea uchi. Baadae anaonekana akiwa amevaa majani nusu uchi. Mpaka sasa sielewi ni elimu gani alikuwa anatoa ama ni makusudi gani alikuwa nayo kwa jamii. Lakini pia EATV wanataka vijana wetu wawe wanatembea uchi? ama watupe c-h-u-p-i na waanze kuvaa majani? Tanzania tumekosa maadili kiasi hiki hadi tunaachia vichaa watuonyeshe njia ya kwenda kweli? MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI TANGANYIKA!
Mimi nilivyoelewa alikua anafanya photoshoot ya gazeti(jina sikumbuki) sasa kwenye kipindi kile walikkua wanaonyesha process nzima ilivyokwenda. Ndio nguo na haziku-cover maeneo yote but ndio generation ya kibongo ilivyo hivi sasa.
 
Wewe mtu mzima uanendaje kuangalia hicho kipindi waachie vijana hafu sikuhizi kila mtu anaking'amuzi kwahiyo siyo lazima hiyo channeli iwepo unaweza kuifuta
Siku nyingine usilete katika jukwaa la siasa, peleka jukwaa la burudani.

Ni Tanzania na baadhi ya nchi za kiafrika ndio hatuna misingi mizuri ya maadili. Kwa hiyo kumbe wewe unashabikia vijana kuangaliana uchi zao? hivi kuonesha tupu ni ujana ama ujinga? unaposema sio lazima kuangalia ni sawa lakini hata free will zinamipaka. Ndio maana ukienda europe huwezi kuta magazeti ya ngono mahala pa wazi ama picha za utupu hovyohovyo! kweli unashabikia vijana wetu kuwa wapenda ngono?
 
Mimi nilivyoelewa alikua anafanya photoshoot ya gazeti(jina sikumbuki) sasa kwenye kipindi kile walikkua wanaonyesha process nzima ilivyokwenda. Ndio nguo na haziku-cover maeneo yote but ndio generation ya kibongo ilivyo hivi sasa.

would you like your daughter to behave the same way?
 
Mbona Channel zipo nyingi mfano Efatha, ATN, Tv Tumaini, Tv imani na zingine nyingi ambazo zinatangaza neno la Mungu tu. Kupo na watu wanapenda kuona hayo mambo tena na wewe ni mmoja wao ndio maana umeangalia mwanzo mwisho. EATV ipo kibiashara na wanafuata maadili ya habari ndio maana walificha baadhi ya viungo. Kama uliangalia bahati mbaya basi usirudie tena.

Uharibifu wa jamii huanzia kichwani! usije kukemea mapepo ukianza kuona kitoto chako cha kike kinatembea uke wake uko nje! biashara bila maadili ni upuuzi! mbona nchi za kiarabu wanatuzidi maendeleo na biashara na hawaachi tupu zao nje! kuangalia pia ni kujifunza!
 
Msanii si ndio kioo cha jamii KUNA vipindi vingine havina tija kwa jamii,,, haya bwn si ndo msanii huyo mwache afanye sanaa zake kumbe hata kukaa uch ni sanaa lol .leo kama hujashangaa kumuona wema akiwa vile bhasi ipo siku hautashangaa kumuona mwanao nae kavaa vile.. kashamulikwa na kioo chake
 
huyu wema hivi anatoa hela kabisa kutuonyesha sisi huo mwili wake na blabla ambazo mwanzo mwisho hana wazo jipya huwezi angalia hivi vipindi halafu ukapata jipya la maisha

Hatoi hela, wadhamini ndo eti wanatoa hela.
 
Ni Tanzania na baadhi ya nchi za kiafrika ndio hatuna misingi mizuri ya maadili. Kwa hiyo kumbe wewe unashabikia vijana kuangaliana uchi zao? hivi kuonesha tupu ni ujana ama ujinga? unaposema sio lazima kuangalia ni sawa lakini hata free will zinamipaka. Ndio maana ukienda europe huwezi kuta magazeti ya ngono mahala pa wazi ama picha za utupu hovyohovyo! kweli unashabikia vijana wetu kuwa wapenda ngono?

Ulaya walishaendelea, hakuna wamachinga wanaotandaza vitu barabarani, Kama ni kujilinda mbona wanaonesha channeli za ngono hukohuko Ulaya na kwasasa wanalalamika vijana wadogo teenagers wanaangalia pono kupitia kwenye mitandao? Unalalmika nini wakati nguo mnazileta wenyewe kuwauzia vijana au hata hili unataka kuilaumu serikali? Au unataka serikali ikupangie mavazi ya kuvaa? Sisi tunadumisha mila zetu tulikuwa tunavaa magome ya miti kufunika nyeti sasa leo mnajifanya hamzitaki hizo mila. Nenda kwa wazizabe kule porini uone wanavyoishi, nenda Botwana kwa waswana uwaone. Nadhani umenielewa. Mpingauonevu
 
majina yao tuwawajibishe kunako general election 2015

tanzania hatuna hiyo power kwa uwizi wao uliokithiri wa kura. ingekuwa nguvu ya kura inaweza kuwawajibisha naamini leo JK asingekuwa raisi wetu na viongozi wengi wa CCM wasingekuwa wawakilishi wetu. tatizo wizi wa kura unauuwa aina hii ya uwajibishaji.
 
Ulaya walishaendelea, hakuna wamachinga wanaotandaza vitu barabarani, Kama ni kujilinda mbona wanaonesha channeli za ngono hukohuko Ulaya na kwasasa wanalalamika vijana wadogo teenagers wanaangalia pono kupitia kwenye mitandao? Unalalmika nini wakati nguo mnazileta wenyewe kuwauzia vijana au hata hili unataka kuilaumu serikali? Au unataka serikali ikupangie mavazi ya kuvaa? Sisi tunadumisha mila zetu tulikuwa tunavaa magome ya miti kufunika nyeti sasa leo mnajifanya hamzitaki hizo mila. Nenda kwa wazizabe kule porini uone wanavyoishi, nenda Botwana kwa waswana uwaone. Nadhani umenielewa. Mpingauonevu

Nimekuwa ulaya japo kwa miezi mitatu. Majarida ya ngono yanafichwa mbali. Hata kama hakuna wamachinga bado huwezi kukuta gazeti la ngono ama movie za ngono eneo la wazi supermarket bali maduka yake yanakuwa underground ama eneo lolote isiyoonekana kirahisi. Picha za ngono ndio zinaoneshwa lakini ni usiku mkubwa wakati inajulikana watoto wamelala na hawana ulimbukeni wa kuwa na TV kila chumba kama sisi tunavyofanya. Asili yetu ni kuwa tulikuja tuko uchi kama wanyama. Utashi wa akili Mungu aliotupa ndio unatuambia hapana tusitembee uchi kama mbuzi bali tufiche tupu zetu. Ikiwa huna akili ya kuficha tupu wewe unakuwa kama mnyama tu na ndio maana wahadzabe tunawashangaa maana tunawaona kama wanyama tu! kama ni uongo vaa majani nawewe kesho ukiingia ofisini kama hatujaenda kukupima kichwa!
 
Alikua anapiga picha gazeti la mshkaji wangu linaitwa vibe...lakini hakutakiwa kuonyesha kwenye kipindi chake...it should be edited
 
mkuu ulichelewa kuja mjini au makusudi?wema ni maarufu toka mwaka 2006 unawezaje kusema mwaka huu 2014 ndio anautafuta huo umaarufu labda useme anataka kuulinda umaarufu wake

kazi yake ni muigizaji na ana kampuni yake ya kuzalisha filamu inaitwa endless fame ameshafanya filamu kadhaa kama superstar na nyingine nyingi pia ameigiza filamu kama lerato, the point of no return na nyingine kibao
Mkuu kweli na wewe umeingia kingi hapa kwenye red?? hiyo ni kazi ya kuizugia public tu bana, kazi yake halisi waulize TISS mbona wanamsitiri tu!
 
kile kipindi hata hakieleweki
sijui hata kimewekwa kwa madhumuni yapi!
hakielimishi wala nn,ujinga tu!!
 
kipindi kinaitwa WEMA SEPETU - UNDER MY SHOES. Wema pamoja na mambo mengine anaonekana akiwa uchi anapiga picha. hata kama uchi wenyewe umefichwa kwa majani, na wakati anatembea maziwa nje picha zinafichwafichwa kwa computer lakini haizuii content kwamba wema anatembea uchi. Baadae anaonekana akiwa amevaa majani nusu uchi. Mpaka sasa sielewi ni elimu gani alikuwa anatoa ama ni makusudi gani alikuwa nayo kwa jamii. Lakini pia EATV wanataka vijana wetu wawe wanatembea uchi? ama watupe c-h-u-p-i na waanze kuvaa majani? Tanzania tumekosa maadili kiasi hiki hadi tunaachia vichaa watuonyeshe njia ya kwenda kweli? MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI TANGANYIKA!

Mkuu weka picha tuone kamani kweli!
 
nawashangaa wale wakaka wanaomtengeneza na kushika shika yale maziwa. wema hajambakizia mumewe jambo jipya hata moja kwenye mwili wake maana wengi wamekwishauona.
 
Back
Top Bottom