Wengi hamjui, ujasiri wa Makonda ulianzia hapa!

Wengi hamjui, ujasiri wa Makonda ulianzia hapa!

Huu ujasiri usio kifani ndio muendelezo wake huu wa kusema atapiga makofi mtu
Kwa hiyo yote haya ni maelekezo
Ila kama kumtuma na kusema nani anaweza hizi kazi za udhalilishaji basi usiite ujasiri bali kazi zisizo na aibu wala Soni na hayaa

Siku njema
 
Ujasiri wa Makonda uliiashia kwenye mazishi ya JPM chato, baada ya pale Makonda anapokea maelekezo ya nini cha kufanya, na hata haya anayoyafanya yana baraka kutoka Kwa yule yule master planner wa hii michezo ya sarakasi za siasa hapa bongo.

Mapunziko ya Makonda na kuachwa kwake bila kuguswa yalikuwa maelekezo maana ni asset kwa kazi za CCM baadaye ndio maana aliachwa kiporo.

Waliomtuma safari hii wanaakili kuliko yeye, Wana akili pia kuliko bosi wake wa zamani na bahati mbaya walimleta mjini wenyewe kupitia yule Mzee aliyelala Tabora, na ni mabingwa wa michezo yote michafu lakini pia huwa ni watu low key sana kwenye game na michezo ya karata, Mara nyingi huchokozwa ila wakilipa visasi vyao ndio lawama huenda kwao maana adhabu zao ni Kali.
Hakuna lolote Chai tu hii. Makonda anafahamika vizuri na anafanya anachoweza fanya vizuri na Viongozi wake waliliona hili.
 
Mleta uzi anafanana na mtoto wa mstaafu wa Jiji pendwa na aliyetuachia majanga kwenye nishati muhimu
 
Baada ya kutoka Kolomije na kufika Dar es salaam Makonda alifikia Lumumba kwa utambulisho wa uCCM. Alilala katika moja ya ofisi za chama hicho siku kadhaa kabla ya Mzee Samwel Sitta kumchukua nyumbani kwake kama rafiki na Msaidizi wake.

Ni Sitta alifanikisha Makonda awe Katibu wa Chipukizi na Hamasa akisaidiwa na Jokate aka kidoti. Ni katika kipindi hicho Jaji Joseph Sinde Warioba akimaliza kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu Katiba Mpya.

Jaji Warioba alikabidhi ripoti hiyo Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kwa mbwembwe zote. Hata hivyo ripoti hiyo haikumpendeza kabisa JK baada ya kuonekana asilimia 75 walitaka mfumo wa Serikali tatu na Warioba alilisisitiza kila alilopata nafasi ya kuzungumza iwe ni kwenye tv, redio, magazeti na midahalo. Katika korido za Ikulu JK alisikika akisema kwa ghadhabu, "huyu Mzee ni mchawi, Serikali tatu ilikuwa kwenye hadidu za rejea?" Alikasirika sana.

Hukumu ya hasira yake iliyoratibiwa na wavaa mawani ilikuwa ni kumdhalilisha Warioba hadharani Kwa gharama zote. Hapa ndipo yule kachero wa operesheni aliyefia ajalini Bagamoyo alipojipa kandarasi ya kumdhalilisha Jaji Warioba ili mfalme aliyenuna afurahi. Ni hapa ndipo alipoulizwa Makonda kama anaweza kufanya kazi hiyo? Naye akasema, "Naam". Kwa kazi hii Makonda aliahidiwa kupewa 10m lakini alipewa 7m tu.

Kazi Gani? Naam, Makonda alipewa jukumu la kumtia dole Mzee Warioba na wengine wa UVCCM hao hao kuhakikisha wanapiga picha vizuri akifanyiwa udhalilishaji huo mbele ya wajukuu zake. Lakini Mungu ni Mwema Makonda aliishia kumvuta Mzee Warioba bila mafanikio. Ni jambo analijutia Hadi Leo Kwa nini hakumdhalilisha Warioba kama Mpango kazi ulivyosukwa. Huu ni ujasiri usio kifani. Kwa mfuatiliaji nenda Ubungo Blue Pearl ukaulize ni nani alilipia ukumbi wa mkutano kwa ajili ya mdahalo ule wa Katiba? Wale vijana wa UVCCM walitokea wapi ghafla na mabango? Utapata jawabu la hiki nilichoamua leo kuweka wazi.

Next time nitawaambia ujasiri wa Makonda ulivyowagharimu Charles Kitwanga na Charles Mwijage. Jumapili njema na maombolezo mema ya mpendwa wetu Edward Lowassa.
Kweli watanzania wengi wamechoka akili. Acha uongo!! Chuki zako binafsi zipeleke huko ndugu. Huu Uzi uondolewe.
 
Back
Top Bottom