Wengi hawajaielewa kauli ya Dkt. Ally Bashiru kuhusu CCM kutumia faida ya kuwa na dola kuendelea kubaki madarakani

Wengi hawajaielewa kauli ya Dkt. Ally Bashiru kuhusu CCM kutumia faida ya kuwa na dola kuendelea kubaki madarakani

Unajua mchawi akiroga sana na akianza kuzeeka huwa anawatangazia waliomzunguka kuwa cku zote yaya ndie aliyekuwa anawaroga jamani nyie wachawi MUNGU anawaona shauri yenu
 
Nimesikiliza kwa umakini alichosema katibu mkuun CCM juu ya matumizi ya dola kuhakikisha chama kilicho shika dola, nimegundua kuna upotoshaji.

Alicho maanisha ni kutumia dola kwa maslahi ya chama dola ili kilinde maslahi umma.

Mfano kudhibiti rushwa, ufisadi, kuleta nidhamu kazini n.k . Na sio kukandamiza upinzani.
Nonsense
 
Chama kilichoshika dola huvitimia vyombo vya dola kutekeleza ilani yake
Chama kilichoshika dola kinapaswa kutenda kadri ya katiba. Kama kwa ufinyu wa akili yako ni huo basi duniani kusingekuwa na vyama vya upinzani. Kwa vile chama kilicho madarakani kinalindwa na dola. Acheni UHAYAWANI HUU WATANZANIA
 
Mleta mada pole sana kwa kuwa mwanafunzi wa Bashiru pia pole sana kwa kurithi ujinga wa Bashiru.
Ki msingi, hii mada haikuhusu wala sio saizi yako. Lakini kwakuwa ni mada ya wazi, basi kila mtu anaweza kuweka chochote. Ila mwisho utaeleza nani ilimhusu na nani alidandia tuu.
 
mwana wa Tanzania,
Wasio mwelewa Dr Bashiru katika hilo ama wanafanya maksudi ili kukidhi muktadha wa kisiasa, wana akili finyu katika kuchakata hoja, au wanajifanya hamnazo kwa vile ukweli huo ni mchungu na hauwanufaishi kisiasa.
 
Yaani umeweka maneno ya kiingereza ili tukuamini wakati mzee wa fegi au mzee wa sigara ashamaliza maneno au hauelewi vyombo vya dola ni nini?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Vyombo vya dola vinafufua hizo ndege au unataka tukufundishe siasa?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mfano uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na kile kilichotokea Zanzibar 2015 na katika majimbo mengi tu ya uchaguzi kama kule kwa kafulila,yote hayo ukiyapachika kwenye kauli ya Bashiru basi unaelewa kwa wepesi sana!
 
mwana wa Tanzania, Wewe na mkufunzi wako yatosha kuwapeleka darasani kwa Albert Einstein: If you can't explain it simply, you don't understand it well enough! Kazi kwenu. Pingeni hata hilo. Hamjambo?
 
Kwanza tafsiri tunaposema dola tuna maana gani? na tunaposema vyombo vya dola tuna maana gani?

Mimi kwa tafsiri isiyo rasmi nadhani vyombo vya dola ni taasisi za umma ambazo chama chochote kikiingia madarakani kitazikuta na hicho chama hakitakiwi kutumia vyombo hivyo kupata faida isiyo ya kisheria. Kwa mfano kuayatumia majeshi yetu yakandamize wapinzani wako wa kisiasa bila sababu.
 
Unapotoa maelezo ambayo wengi hawakuelewi sio makosa ya wale unaowaeleza bali ya yule anayelezea kutokueleweka..., huyu jamaa statements zake nyingi ni unneccessary and leave a lot to be desired...
 
Ukweli ambao haukuwa umetamkwa wazi, sasa umewekwa wazi na Dr. Bashiru bila kumung'unya maneno. Vyama vya upinzani vinapambana na CCM + Dola. Hiyo dola inatumikaje, the writings are on the wall for everybody to see.
 
Back
Top Bottom