Wengi hawajaielewa kauli ya Dkt. Ally Bashiru kuhusu CCM kutumia faida ya kuwa na dola kuendelea kubaki madarakani

Wengi hawajaielewa kauli ya Dkt. Ally Bashiru kuhusu CCM kutumia faida ya kuwa na dola kuendelea kubaki madarakani

Naona unajitahidi sana kumsafisha Katibu wako lakini nikueleze tu kuwa huo utetezi hauna nafasi kwa sasa hivi na hayo maneno aliyoyatamka tunajua ndiyo yamejaa ndani ya moyo wake.

Hiyo tafsiri unayosema haikueleweka labda ni wewe hukuielewa lakini yeye alinyooka kusema moja kwa moja kilichokuwa ndani ya moyo wake na kama kungekuwa na tafsiri nyingine ya hayo aliyoyatoa basi angeweza kuyatolea ufafanuzi wakati akiyatamka.

Kwa hiyo ndugu tulia tu ujumbe tumeshaupata na tu au fanyia kazi ndani ya tafakuri zetu kichwani na wala hutaweza kuleta maana ingine tofauti na alichokitamka zaidi utakuwa unapoteza muda hapa kutaka tuamini tofauti na aliyeyatoa hayo maneno.
 
Mleta mada Dr Bashiru tumemwelewa vizuri sana usitake kuhamisha magoli matumizi ya dola (polisi, mahakama, takukuru, uhamiaji na vyombo vingine vya dola) kukandamiza wapinzani hasa CHADEMA yapo wazi kabisa sasa unapotaka kuja kuhamisha magoli hapa baada ya kuona kauli yenu mliropoka bila kupima effect yake mnakuja kumsafisha ningekutukana pumbafu kabisa ila tu sheria za jfoo haziruhu kufanya hivo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dola maana yake ni vyombo vya ulinzi, police, jwtz, jkt na vyengine kuiweka ccm madarakani, kwa maana hio vyombo hivi Siku ya uchaguzi vinatumika kuhujumu wapinzani,kuwafukuza mawakala kwenye vituo vya uchaguzi, kusimamia kura fake visanduku vya kura uingizwa kwenye vituo.

2015 malori yamekamatwa na wananchi yamejaa kura fake, na dola kusimamia.

Dola huvamia office za wapinzani wakati wa uchaguzi kuwakamata na kuwapokonya kama computer za office na facilities nyengine.

Hio ndio dola



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mamtu unajua hayana akili? Who's gonna buy this garbage? Yani watu wa propaganda Lumumba wana fail sana..haya mambo wakawambie watu huko vijijini wenye uelewa mdogo kama wao...huyu bashiru ni kichaa sana..so anataka mapambano ya RAIA na vyombo vya dola?

Au PHD yake Kichwani hamsaidii Ku analyze mambo? Haki isipotendeka na CCM wakafikili vyombo ya dola vitawalinda siku zote then they are too naive to understand what's going to happen in the near future...

It's either hivyo vyombo vitawatoa madarakani wao au wananchi wenyewe watawatoa, ikibidi kwa nguvu na kumwaga damu! Historia huwa haikosei.
 
Hiyo kauli ina two faces of the coin, lakini wewe naona inclination yako ni kwenye only one of the coin without considering the opposite site of the same coin
 
Nigrastratatract,
Je alipotoa mifano halisi ya UNIP, KANU and the likes ulimuelewa? Unajua jinsi walivyokuwa na nini kiliwaangusha? Au ulikuwa Mtoto hujui? Huyo Katibu maana yake haijafichika ni kutumia jeshi la wananchi, jeshi la polisi, tume ya uchaguzi kupora uchaguzi na kilamtu including wewe unajua ila kwakuwa ibilisi kautawala moyo wako unajibaraguza.

Waliomtangulia pia walitumia dola ila hawwkuwa na ujasiri wa kutamka yanayotamkwa na viongozi wa awamu hii, si kutamkwa tuu Hata kufanya mambo ya aibu bila aibu!

Mfano halisi ametukumbusha kila wakati wa uchaguzi mkuu ndege za jeshi huwa zinatestiwa! Nadhani ratiba yao ya matengenezo inaendana sawa na uchaguzi!
 
Kasimba G, Mtu yeyote ambaye Roho yake haitawaliwi na shetani, anajua jinsi CCM inavyotumia vibaya vyombo vya dola kwa manufaa yake. Kinachofanyika ni uhuni na ujambazi katula siasa na utawala.

Je, ni halali watu kuongozwa na chama cha kihuni au kijambazi? CCM inafanya siasa za kihuni.

CCM lazima itoke kwenye primitivity, iingie kwenye siasa za kistaarabu. Siasa za wanadamu ambao kiujumla wanaoongozwa na Mungu.
 
Nigrastratatract,
Pole sana !! nenda ukasome na uelewe. Hivyo vyombo ulivyovitaja havipaswi na kujihusisha na chama chochote cha siasa. Kasome Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 toleo la 2000. Soma vilevile naSherial ya TISS ya mwaka 1996
 
Hapo kwa kweli GT hawapo.....,
Dr.Bashiru yuko sahihi na aliyeleta post amemwelewa vizuri.Ww usiyeelewa nenda tuition tena.
 
Back
Top Bottom