mwana wa Tanzania, 1. Wengine tunaelewa "incumbency advantage" ni nini, kabla hata ya kumsikia Bashiru.
2.Incumbency advantage inaweza kuwa legit. Maana chanya mtu aliyekuwa madarakani anafanya kazi yake vizuri, wananchi wanaona, mpinzani anakuwa hana cha kukosoa, kwenye uchaguzi watu wanamchagua aliye madarakani kwa sababu wameona kafanya vizuri, hata kama mpinzani angeweza kufanya vizuri zaidi. Kiswahili hapa wanasema "Zimwi likujualo, halikuli likakwisha".
Pia aliye madarakani anachagua wanaoongoza Tume ya Uchaguzi, anatoa ruzuku, anateua majaji, mawaziri etc.
Watu washawajua incumbents mazuri na mabaya yao, wanaweza kusema tumewakubali hawa tunaowajua, hao tusiowajua ni fumbo hatutaki kucheza kamari na uongozi wa nchi.
3. Incumbency advantage kwa maana hasi, ndipo hapo incumbents wanatumia vyombo vya dola kudhibiti wapinzani, wanapanga njama na tume ya uchaguzi, wanaiba kura etc.
Tanzania tuna incumbency advantages za aina zote mbili.
Viongozi wanahitaji kuwa waangalifu wakitoa kauli tata, kwa sababu, kuna watu wengi wanachukua maana mbaya kabisa ya kauli. Na mimi hata siwezi kuwalaumu.
Ni wajibu wa viongozi kuwa makini katika kauli, si wajibu wa wananchi kutafuta tafsiri nzuri kabisa ya maneno ya viongozi.
Bashiru kwa kutoa kauli tata kwenye nchi ambayo ishawahi kuwa na wizi wa kura tangu enzi za chama kimoja, nchi ambayo rais anazuia watu wasifanye mikutano ya kisiasa inayoruhusiwa kikatiba, ameji exposed kutafsiriwa kwamba anaongelea incumbency advantage hasi ya wizi wa kura na kutumia vyombo vya dola vibaya.
Na kwa sababu CCM ni kweli hutumia advantage hii, I see this as a Freudian slip.
Somewhere in Bashiru's subconscious mind he wants to communicate to people that CCM is winning by misusing its incumbency to get an unfair advantage in elections.