Kifo cha Tupac kimekuwa na utata na kimeleta gumzo kubwa.
Kuna baadhi ya Watu wanasema, marehemu KADAFI alikuwa akiwafahamu wauaji wa Tupac, sababu yeye KADAFI alikuwa na Tupac, pamoja na Suge Knight mpaka dakika ya mwisho, alishuhudia lilipotokea tukio la kumwagiwa Risasi Marehemu Tupac.
Na marehemu KADAFI aliahidi kuwataja wauaji wa Tupac atakapoenda kwenye mahojiano na wanaUsalama, kitu ambacho baada ya kusikika KADAFI kuwa atawataja wauaji wa marehemu Tupac, ili kupoteza ushahidi ikabidi KADAFI nae auliwe.
Na cha ajabu zaidi KADAFI aliuawa kwa Risasi, miezi miwili tu baada ya kifo cha Tupac