Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, Meditation ipo tofaut sana na wengi mnavyo dhani..na pengine hata mimi nilivyo kuwa najua mwanzo..maana ya meditation siyo kuondoa stress wala mawazo..hayo yanakuwa ni matokeo tu chanya ya meditation..lakini siyo lengo la meditation.Unapiga meditation huku mwenye nyumba anangonga hodi kudai kodi yake, huku unadaiwa pesa ya luku, hatari sana
Aiseee! Haya maisha niliyapitia mwaka Jana baada ya kufilisika aaaah! Sema mke wangu pekee ndio alikuwa mshauri mkuu vinginevyo ningekuwa historia.Hasa wanaume tunashindwa kusema ukweli kwamba tuna depression kwasababu tunaogopa kuonekana dhaifu kama wanawake, pia namna ambavyo jamii inamchukulia mwanaume inamuona kama kiumbe ambaye anatakiwa awe ngangali muda wote ila kiuhalisia depression haichagui mwanaume wala mwanamke.
Wengi sana tunapitia kwenye lindi la mawazo, stress na depression za kila namna kuanzia kudaiwa madeni, kufilisika, kukosa ajira, misuko suko ya ndoa, magoniwa, n.k.
Hivi ni vitu ambavyo ni ngumu sana kugawana na asiehusika lakini tunaweza kugawana comfort katika kufarijiana, kushauriana, kupeana moyo, n.k.
Kuongea huwa inasaidia kwa kiasi chake lakini sasa inafika kipindi unaona ni bora ukae kimya tu kulingana na uzoefu ulioupata katika maisha yako uliokufanya ujue maana halisi ya "kuwa uyaone" na "ukubwa dawa".
Unakuta una mtu wa karibu kabisa unaemwamini, anapoona una shida anaku hype kabisa "its okay unaweza kuongea na mimi, kuwa huru"
Baada ya muda unakuta mambo yako binafsi yameshasambaa mtaani, anaweza kuwa ni mzazi wako kabisa ama mwanafamilia lakini nae kwa lengo zuri la kupata ushauri wa zaidi akawaambia watu anaowaamini, matokeo yake hakuna siri tena, mtaani huko unaanza kujijua ushatangazwa "msimuone ana gari yule, pale alipo ana mawazo ya kurejesha deni", "msimuone ana mke mzuri vile, kagundulika ana kisukari shughuli hawezi", "msimuone vile anakwenda bar sana, kachapiwa mke yule", n.k. USHATANGAZWA!! hata kupita mitaa ya kati unaona noma.
Wengine unawaambia shida zako ila ndio wanafurahia mpaka wanaweza kukununulia chakula upate nguvu ya kuendelea kuwasimulia taabu zako, kwao ni kama kucheki tamthilia, kushuka kwako ama kuganda pale pale ndio furaha yao kubwa sana.
Mkuu, inawezekana kabisa ukawa unajizungumzia wewe na kujiona kama unachekwa kwa unayopitia, pole sana lakini usijisikie vibaya, dunia ndivyo ilivyo.Kuongea huwa inasaidia kwa kiasi chake lakini sasa inafika kipindi unaona ni bora ukae kimya tu kulingana na uzoefu ulioupata katika maisha yako uliokufanya ujue maana halisi ya "kuwa uyaone" na "ukubwa dawa".
Hii Safi sana.Hilo nilijifunza kipindi flani nilikuwa desperate and depressed sana.. Unawaambia watu ambao ulikuwa ride and die kwao ila tatizo lako wanachukulia simple sana na sometimes wanakukata bila huruma wala excuse.
Ikanisaidia kuwajua watu na nikawaweka kwenye category zao wanazostahili na wengine out kabsaa
Kisha nikaamua nirudi kwenye system yangu ya siku zote
"life langu ni jukumu langu la kwanza, nisitegemee mtu flani atafanya kitu flani ili nisogeee NO NO NOOOO,
Huwa naangalia solution tu na kama nikimuhitaji mtu, sifanyi attachment kuwa lazma anipe au anipush kwa sababu naheshimu time na rasilimali zao maana hawakuzipata freely au kirahisi,
Walipambana hivyo, wanaweza kuzitumia kwa mtu ambaye wanamtaka"
Toka hapo naona migogoro ya nafsi au kuona kama nimeonewa mtu akisema HAPANA kumepungua sana..
[emoji848] alaaa kumbee.Mkuu, Meditation ipo tofaut sana na wengi mnavyo dhani..na pengine hata mimi nilivyo kuwa najua mwanzo..maana ya meditation siyo kuondoa stress wala mawazo..hayo yanakuwa ni matokeo tu chanya ya meditation..lakini siyo lengo la meditation.
Kwanza unatakiwa kujua jinsi mind inavyo fanya kazi,hyo ni concept ya mwanzo kabisa..(Concious mind vs Subconscious mind)
Maana ya Meditation ni kuacha kila kitu kiflow kama kilivyo without reacting, judging or attachment to it,iwe ni kizuri ama kibaya..wewe unatakiwa ubaki constant..mwanzo ni ngumu sana because subconscious mind itaanza kurelease takataka zote (chuki,hasira,hofu,wivu, cravings) nk ulizo hifadhi tangu ukiwa mdogo mpka sasa then wewe unatakiwa tu ku witness kinacho endelea bila kuhukumu..with time utaanza ku gain power za ajabu,maana zile takataka za kwenye subconscious mind zinavyo toka,wewe unakuwa msafi.
Mshana Jr tutafute muda tuwaelekeze watu meditation..hii imekuwa the best knowledge in my life...kuliko degree ya aina yoyote
[emoji1787]kwa kweli ,bora ukalilie kanisan ,utoe sumu ,then maisha yanaendeleaHakikisha hawajui matatizo yako ili kuweza kukuepusha na matangazo
Hii Elimu ( Emotional Intelligence) tulipaswa tufundishwe tangu primary mpaka chuo kikuu.. Watu wengi linawachanganya neno Meditation,lakini maana yake kwa ufupi ni Consciousness ama Ufahamu kwa kiswahili...[emoji848] alaaa kumbee.
🙏🙏🙏Hii Safi sana.
L
Kusema kwamba hakuna ndugu waliofika msibani hakuna aliefika ntashangaa sana, au labda ulimaanisha waliofika ni wachache ama waliohudhuria ni wa huko huko kijijini ?Mie nilipata experience na funzo kubwa kutoka kwa mzee wangu (sasa marehemu).Mzee alikua na pesa...kipindi hicho..boss mzito sana serikalini..yaani kama kuna sherehe ya ubatizo home wanaokuja unakuta mkuu wa wilaya, katibu tawala, viongozi wa dini na watu kama hao.Mzee alisaidia watu wengi sana kwenye ujana wake, wale ndugu wa vijijini wanakuja home, wanasoma, wanaenda mbele kwa mafanikio.
Mzee alikua na marafiki si mchezo,..yaani heka heka..
Balaaa lilianza baada ya kuacha kazi ( kuna mambo yalitokea ingawa sijui)...maisha yake yakayumba sana, kaenda kwenye biashara ikagoma..kachukua mkopo bank...CRDB..kashindwa kulipa..nyumba ikapigwa mnada.....
Kaingia DSM kapiga maisha..etc...hali haikuwa nzuri sana....Cha ajabu sikuwahi kuona tena marafiki zake, ile kampani yake, ndugu aliwasaidia ambao tayari walikuwa vizuri....wote kimya, hata kwa upande wa mama wote kimya..
Mzee kapata maradhi kajifika..kaenda kuzikwa kijijini...hakuna rafiki, au ndugu wa pande zingine ambao yeye ndo aliwalea....waliotokea msibani....Nikawa nashangaa sana, mzee alikuwa na kampani bwana, kasaidia watu wengi- leo wako wapi???
Nilikuwa mdogo kipindi hicho..haya mambo yameanza niko darasa la tano, mzee kafariki niko chuo mwaka wa pili...
Nilijifunza kwa kweli...mpaka leo sina kabisa kiherehere na watu..ninajuana na watu wengi..lkn siamini sana katika urafiki wa kupitiliza.......nilijifunza
Mapitio ya mzee na yaliyomkumba yalinifundisha sana