Wengi tungeswekwa magerezani awamu ya tano wakati Serikali inataka IP adress za accounts zinazoikosoa, tunashukuru JamiiForums mlitusimamia

kama ni kwenda kuomba kwa mitandao husika inawezekana wale ndio wana-configure hizo dns server.
 
Mkuu punguza ujuaji, mimi hapa nimeandika kwa lugha nyepesi tu kila mtu aweze kuelewa.

Ip adress ni kweli zinabadilika kila unapowasha na kuzima simu lakini kama zinarekodiwa (ip logging) katika tovuti na mitandao ya simu huwezi kuruka.

Kwa taarifa yako tu ni kwamba hata ip ambazo ulizitumia mwaka jana kama tovuti inazi log, zinaweza kuwa traced zilikuwa zinatumika kwenye namba ipi kama nayo mitandao ya simu inatunza kumbu kumbu.
 
Mkuu nikuelimishe tu kwamba kama tovuti inarekodi ip adress unaweza kudakwa kirahisi tu, unaweza kuanza kutumia hizo proxy lakini kama tovuti inarekodi ipp adress wanaweza kucheki hata ip adress zako zilizotumika kusajili account yako mwaka 2018 na wakaenda kuzi match wajue ip adress ni ilikuwa inatumika kwenye kifaa kipi na hapo wataangalia namba ya laini iliyokuwa kwenye kifaa aidha simu ama modem, n,k, hadi hapo ushadakwa.

Kigogo hakukamatwa kwasababu alikuwa anatumia twitter, twitter hawawezi kubabaishwa na nchi kama Tanzania eti watoe ip adress za mtu flani tena kwa sababu za kukandamiza uhuru wake maoni yani hapo twiiter hawawezi kukuelewa watakwambia peleka ujinga wako kwengine, Twitter hadi watoe ip adress labda iwe ni kwenye mambo ya ugaidi, ujambazi, n.k.
 
kama ni kwenda kuomba kwa mitandao husika inawezekana wale ndio wana-configure hizo dns server.

Sikuelewi unaposema wanaconfig DSN server ,kazi ya DNS server ni only kutranslate tu IP badala ya kwenye web kuandika 204.30,104.46 unamap na text jamiiforum.com ,kuconfig Static IP kwenye simu wanaconfig kwenye profile ya namba ya mteja na pia hizo static ip za kwenye computer ni for their LAN(locallly) and their DSN ikitoka nje kwenda globla iP inabidi ifanyiwe NATTING.
 

Sawa lengo la kutumia proxy/vpn ni kumpoteza third party ila source anaipata ip yako.....Na ndiyo maana tcra walivyotoa order kwa MNOs wablock Twitter/Facebook/Instagram kipindi cha jiwe lakini ukiswitch ON VPN ulikuwa una access vizuri because ilikuwa inampoteza Third party(MNO) na ndiyo lengo ila source(VPN /Proxy owner anajua ulivyokuja na local ip yako).
 
Tatizo ni kwamba hio order ya kutaka ip adress ilikuwa ni kama surprise, watu walikuwa washatumia jamiiforums almost kwa miaka na hapa hata wangeanza kujificha kwenye vpn au proxy ingekuwa useless kama kungekuwa na logs za ip adress walizokuwa wanatumia kabla ya kuanza kujificha endapo jamiiforums wangetoa ushirikiano.

Yote kwa yote tunashukuru mambo haya yalipita na tuombee iwe never and never again,

Vibe la kuchangia humu ndani lingekuwa limepungua sana, imagine kwamba tu unajua unachoandika hakina uhuru mda wowote uliemsema akipata hasira anakutumia difenda,
 
Kasheshe
 
Maxmeello angeunga Mkono Juhudi watu Wazito wazito waliomo humu wangeteketea sana
Mtu mwenye jicho pevu la mbali hawezi kufanya jambo kama hilo bila kufanya tathmini ya kina. Ilikuwa wazi kwa kila mwenye jicho la mwewe kwamba asingalifika popote
 
Kigog alitumia iphone. Plus vpn. Yan hapo ni kofuli la moto. Tena zile vpn za kulipia pesa nzuri.
 
Aisee
 

Before ungoje jamii forum iku protect, you need to protect yourself.
 
Well presented
 

Jamaa alikuwa na kihere here adi sio poa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…