Jumla ya wanachuo ambao hawatapiga kura ni 60,000 Tanzania yote,unafikiri hao wanatosha wataweza kumuweka mzinzi madarakani?
WEWE HUNA TOFAUTI NA HUYU MPUUZI HAPA CHINI ANAYEDHANI KUWA KUPIGA KURA NI SIASA NA SIO HATI YA KIKATIBA. HALAFU ANAJIITA PROFESSOR, SIJUI PROFESSOR WA KATIKATI YA VIDOLA KUNAKOOTA FUNGUS AU VIPI. KWELI HII NCHI ITAENDELEA KAMA WATU WANA MAWAZO YA KIJINGA NAMNA HII KISA KULINDA ULAJI? PROFESSOR UMEKOSEA, ALIYEKUPA HUO UPROFESSOR AKISOMA HII ATAKUFA MANAKE HAKUJUA KAMA UNAWEZA KUWA MJINGA KIASI HIKI
KURA NI HAKI YA KIKATIBA, SIO SIASA!!!
Prof: Maghembe: Vyuo vikuu havitafunguliwa hadi Novemba
Na Richard Makore
5th October 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe
Serikali imesema haitabadili uamuzi wake wa kufungua vyuo vya elimu mwezi Novemba mwaka huu kama ilivyopanga licha ya kuwepo shinikizo la wanafunzi wanaotaka vifunguliwe ili kuwawezesha kwenda kupiga kura kwa kuwa wengi wao walijiandiskisha vyuoni.
Uamuzi huo wa serikali ulitangazwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, na kuongeza kuwa vyuo vya elimu ya juu sio taasisi zinazoendesha siasa, bali ni maeneo yanayotumika kufundisha watalaamu wa kada mbalimbali
Profesa Maghembe alihoji ni kwa nini wanafunzi hao washinikize vyuo vifunguliwe kwa madai ya kutaka wakapige kura wakati wao hawahusiani na siasa zozote zinazoendelea hapa nchini na badala yake wao ni wanafunzi wanaohitaji kufundishwa ili wawe watalaamu wa baadaye.
Chuo kikuu sio sehemu ya kwenda kufanya siasa, bali ni sehemu ya kufundisha watalaam mbalimbali na kwa kweli nashangaa hawa wanafunzi kushinikiza vyuo vifunguliwe, alliliambia NIPASHE.
Alifafanua kwamba vyuo vyote vinapanga siku ya kuanza mwaka wa masomo kulingana na programu zao kwa mwaka mzima kwa kutegemea raslimali walizonazo.
Alisema mwaka huu muda wa kufungua umesogezwa mbele kutokana na kubadilika kwa mfumo wa udahili wa wanafunzi.
Profesa Maghembe alisema mabadiliko ya mfumo huo wa udahili kulilenga kurahisha kazi hiyo pamoja na kuziba mianya ya wanafunzi kudahiliwa zaidi ya chuo kimoja na hivyo kuwanyima wanafunzi nafasi wenzao wanaotaka kujiunga na vyuo.
Alifafanua kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ilitoa muda kwa watu waliotaka kuhamisha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura na kama wanafunzi hao hawakufanya hivyo serikali haina namna ya kuwasaidia ili waweze kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 31.
Wakati Profesa Maghembe akitoa msimamo huo wa serikali, juzi Nec nayo ilipigilia msumari wa mwisho baada ya kusema kuwa haitaweka utaratibu mwingine ili kuwawezesha wanafunzi wapatao 60,000 wa vyuo vikuu waliopo likizo kuweza kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
Kauli hiyo ya Nec ilitolewa juzi na Mkurugenzi wake, Rajabu Kiravu alipozungumza na Nipashe wakati akijibu hoja ya wanafunzi hao waliotaka kuwekewa utaratibu utakaowawezesha kupiga kura wakiwa likizo.
Wanafunzi hao na wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini ambao ni wapenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walitoa malalamiko hayo jana kwenye kongamano ambalo lilijadili masuala ya Uchaguzi Mkuu.
Kadhalika, wanafunzi hao waliitaka serikali kufungua vyuo vya elimu ya juu ili kuwapa fursa wanafunzi kupiga kura kwenye maeneo waliyojiandikishia na kwamba kama itashindwa kufanya hivyo watakuwa wanawanyima haki yao ya msingi kwa mujibu wa ibara ya 21 ya katiba.
CHANZO: NIPASHE