Elections 2010 Wengi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutopiga kura 2010

Elections 2010 Wengi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutopiga kura 2010

hizo ni akili finyu za makamaba and the lot in ccm, kwangu mimi nawaona hawa vijana kuwa potentially hazardous against ccm huko mitaani, vijijini na na kwingineko waliko sasa hadi tarehe 31 oktoba 2010 kuliok kama wangeruhusiwa kuwa vyuoni mwao.

kutokana na miscalculationa za ccm, chadema and the opposition ita benefit kwa kupata wasemaji na wawakilishi in different parts of the country. Nina uhakika mkubwa kuwa hata sasa wanachangia kwa kiwango kikubwa kuhamasisha watu kujazana katika mikutano ya kampeni ya dr slaa, watatumika kuwahamasisha watu kujitokeza kupiga kura na kulinda kura za wagombea wa chadema huko waliko.

ndio maana nathubutu kutamka kwa ccm imeishiwa fikra. Hivyo na na sisi wengine tuache kuwaiga ccm kulalama tu, lets seize the opportunity kwa kuwahamasisha hao vijana kulipa visasi vya kupokwa haki zao za kupiga kura kwa kuwahamasisha watanzania popote walipo washiriki kikamilifu kuleta mabadiliko mwaka 2010 kwa kujitokeza kupiga kura kwa wingi sana na kuwachagua wagombea wa chadema kwa wingi.

kwa kufanya hivyo watakuwa wametio mchango mkubwa kwa taifa hili unaozidi kura zao moja moja.

Safi sana mkuu, hata mimi naona ni mabalozi wazuri sana katika kuiwakilisha Chadema huko sehemu mbalimbali. vijana hao ndo haswaa wanaoonja machungu ya kuwa na mafisadi kwa kubaguliwa katika maisha yao vyuoni kama kulala watu wawili kwenye kitanda kimoja, kupewa mikopo isiyostahili na kwa manyanyaso, kusoma wakiwa wamesimama madarasani. nk
 
Kama wamemzuia kila mwanafunzi kupiga kura moja kwa ujuha wao (CCM na Serikali yao), ni faida kwa CHADEMA kama kila mwanafunzi huko aliko akimhamasisha Mama, Baba yake na ndugu zake wawili kupiga kura kwa DK. Slaa na kuikataa CCM.

Nimeafiki ule usemi wa Safari moja huanzisha nyingine!
 
Hao vijana kwa shida ambazo CCM imewabaandika nazo bila ya huruma wengi wao watajigharimia ili kuhakikisha CCM na hususani JK ni iBye-Bye
 
hizo ni akili finyu za makamaba and the lot in ccm, kwangu mimi nawaona hawa vijana kuwa potentially hazardous against ccm huko mitaani, vijijini na na kwingineko waliko sasa hadi tarehe 31 oktoba 2010 kuliok kama wangeruhusiwa kuwa vyuoni mwao.

kutokana na miscalculationa za ccm, chadema and the opposition ita benefit kwa kupata wasemaji na wawakilishi in different parts of the country. Nina uhakika mkubwa kuwa hata sasa wanachangia kwa kiwango kikubwa kuhamasisha watu kujazana katika mikutano ya kampeni ya dr slaa, watatumika kuwahamasisha watu kujitokeza kupiga kura na kulinda kura za wagombea wa chadema huko waliko.

ndio maana nathubutu kutamka kwa ccm imeishiwa fikra. Hivyo na na sisi wengine tuache kuwaiga ccm kulalama tu, lets seize the opportunity kwa kuwahamasisha hao vijana kulipa visasi vya kupokwa haki zao za kupiga kura kwa kuwahamasisha watanzania popote walipo washiriki kikamilifu kuleta mabadiliko mwaka 2010 kwa kujitokeza kupiga kura kwa wingi sana na kuwachagua wagombea wa chadema kwa wingi.

kwa kufanya hivyo watakuwa wametio mchango mkubwa kwa taifa hili unaozidi kura zao moja moja.

Well said and noted thanks Jatropha
 
Wakachague wabunge wakuwaongoza huko kwao na kwaletea maendeleo katika majimbo yao why ubungo ubungo baada ya mwaka wanarudi makwao?
 
Uko uko waliko watakuwa wajumbe wazuri wa kueneza ujumbe wa ukombozi wa Tanzania
 
Kosa la CCM wamewaweka huko mtaani muda mrefu na sasa wamechacha na wana uchungu. Ukichukulia kuwa Dr. Slaa kisha wahakikishia elimu bure?? Ila uongo, nafikiri kijana wetu wa Ubungo atapungukiwa kura kwa kuwakosa wanafuzi.
 
The last minutes . KIkwete kashika kichwa anawaza.jpg
 
Jumla ya wanachuo ambao hawatapiga kura ni 60,000 Tanzania yote,unafikiri hao wanatosha wataweza kumuweka mzinzi madarakani?
 
hizo ni akili finyu za makamaba and the lot in ccm, kwangu mimi nawaona hawa vijana kuwa potentially hazardous against ccm huko mitaani, vijijini na na kwingineko waliko sasa hadi tarehe 31 oktoba 2010 kuliok kama wangeruhusiwa kuwa vyuoni mwao.

kutokana na miscalculationa za ccm, chadema and the opposition ita benefit kwa kupata wasemaji na wawakilishi in different parts of the country. Nina uhakika mkubwa kuwa hata sasa wanachangia kwa kiwango kikubwa kuhamasisha watu kujazana katika mikutano ya kampeni ya dr slaa, watatumika kuwahamasisha watu kujitokeza kupiga kura na kulinda kura za wagombea wa chadema huko waliko.

ndio maana nathubutu kutamka kwa ccm imeishiwa fikra. Hivyo na na sisi wengine tuache kuwaiga ccm kulalama tu, lets seize the opportunity kwa kuwahamasisha hao vijana kulipa visasi vya kupokwa haki zao za kupiga kura kwa kuwahamasisha watanzania popote walipo washiriki kikamilifu kuleta mabadiliko mwaka 2010 kwa kujitokeza kupiga kura kwa wingi sana na kuwachagua wagombea wa chadema kwa wingi.

kwa kufanya hivyo watakuwa wametio mchango mkubwa kwa taifa hili unaozidi kura zao moja moja.

Nakupa tano mkuu, hizo ndiyo analysis tunazozihitaji hapa.Kifuatacho naamini mnyika anasoma hizi, afanye jitihada za kupatia vijana hawa hizi taarifa ili waendelee kuhamasisha bila kuchoka.Saa ya ukombozi ni sasa
 
Kwani hii imekaaje?

Kama Chuo kinafunguliwa tarehe 01/11/2010 si inamaana Wanafunzi wanatakiwa kurudi siku kadhaa kabla ya Jumatatu? Inabidi warudi wapate sehemu ya kulala, na kufahamu ratiba na kila kitu kinavyokwenda. Siku ya Jumatatu ni Masomo yanaanza na si kuwa ndiyo Wanafunzi wanafika Chuoni. Au kwa sababu mie sijasoma UDSM, sijui utaratibu ulivyo, hebu mnijuvye.......
 
hii issue ingekuwa organized mapema, hawa wanafunzi wote wangepatiwa nauli ya kwenda kwenye vyuo vyao na kurudi baada ya kura, cha muhimu ingeandaliwa nauli na chakula, malazi wakati wa kupigania haki na mambo ya maana sio muhimu sana, hasa kulala nje kwa siku moja tu,
watu walitembea kwa miguu umbali mrefu na walilala maporini kuunga mkono azimio la Arusha, sembuse hii ya sasa ya kuleta mabadiliko?
 
Kama wamemzuia kila mwanafunzi kupiga kura moja kwa ujuha wao (CCM na Serikali yao), ni faida kwa CHADEMA kama kila mwanafunzi huko aliko akimhamasisha Mama, Baba yake na ndugu zake wawili kupiga kura kwa DK. Slaa na kuikataa CCM.

Nimeafiki ule usemi wa Safari moja huanzisha nyingine!

Ni kweli huku vijijini vijana hawajalala wako wanamnadi Dr kwa nguvu zao zote.
 
mnyika na chadema wangewashawishi wanafunzi waliopo dar waunde kamati ya ku organize harambee ili nauli ipatikane ya wao kuja dar siku mbili kabla ya kupiga kura na zitafutwe familia zitakazoweza kujitolea ku accomodate mwanafunzi mmoja au wawili for two night, we have to be smart than ccm, hii inawezekana na muda wa kuwawezesha kuja kupiga kura unatosha tunahitaji muhamasishaji wa kuchukua jukumu miongoni mwa wanafunzi waliopo dar es salaam kuitisha harambee ya kupata nauli zao na kuwaomba wasamalia wa dar es salaam wajitokeze kujitolea accomodation ya siku mbili tu! Iundwe kamati ya wanafunzi wenyewe waliopo dar es salaam watuombe michango na kutoa matangazo kwa wanafunzi wanaotaka kurejea dar kupiga kura wawasiliane na hiyo kamati ili iweze kuratibu safari yao na kutafutia maradhi, ingekuwa ni kura za ccm hilo lingekuwa limetafutiwa ufumbuzi mapema! Its time for chadema to outsmart ccm on their conspiracy! Inawezekana hiyo kwani wana jf wako tayali kujitoa kuchukua mwanafunzi mmoja au wawili ambazo ni kura za dr. Slaa na mnyika, lets do it guys
 
wanchuo popote mlipo pigeni kampeni ya nguvu machunngu yenu yamalizikie hapo mtaa kwa mtaa,ENENDENI MKAITANGAZE CHADEMA ISIKIKE KOTE HUKO sengerema,kanyigo,bukombe,ngara,rombo,marangu,songea,tarime,maruku,upareni,kikatiti,kibosho,singida
 
Ndugu zangu si dhani kama wizi ni kuchukuatu kile kisichokua chako bila idhini ya mwenye nacho, hata kumzuia anestahili kukipata kutokukipata pia umeiba.

Nasema haya nikihusianisha na suala la viuo vikuu kufunguliwa baada ya octoba 31 (siku ya kupiga kura). Kma tunavyojua wengi kama sio wote wa wanfunzi wa vyuo vikuu wanasifa za kupiga kura, na ni dhahiri kua ni mpango wa ccm kutokufungua vyuo vikuu kabla ya 31 oktoba ili wanafunzi hawa wasipige kura kwani kama wakipiga kura nyingi hazitakwenda CCM. Mfano kwa pale ubungo, nyingi zitakwenda kwa Mnyika (ubunge) na Dr Slaa uraisi.

Ushauri: Wanaharakati, vyama vya siasa, taasisi za haiki za binadam na sisi tulio na uchungu na nchi kwa nini tusiungane kutafta suluhu ya hawa vijana kupiga kura??

Kwa slaa sina shaka, lakini kwa upinzani alio nao mnyika kutoka kwa mgombea wa cuf Mtatiro hapo ubungo, hizo kura za vyuo mnyika asingepata maana wengi wangempigia mtatiro maana wanamfahamu vizuri kiutendaji kushinda mnyika. Maana kwa hivi sasa tu ushindani ni mkali sana na huyo kijana mi namkubali sana, hivyo mnyika bado ana kazi ya ziada.
 
Jumla ya wanachuo ambao hawatapiga kura ni 60,000 Tanzania yote,unafikiri hao wanatosha wataweza kumuweka mzinzi madarakani?

WEWE HUNA TOFAUTI NA HUYU MPUUZI HAPA CHINI ANAYEDHANI KUWA KUPIGA KURA NI SIASA NA SIO HATI YA KIKATIBA. HALAFU ANAJIITA PROFESSOR, SIJUI PROFESSOR WA KATIKATI YA VIDOLA KUNAKOOTA FUNGUS AU VIPI. KWELI HII NCHI ITAENDELEA KAMA WATU WANA MAWAZO YA KIJINGA NAMNA HII KISA KULINDA ULAJI? PROFESSOR UMEKOSEA, ALIYEKUPA HUO UPROFESSOR AKISOMA HII ATAKUFA MANAKE HAKUJUA KAMA UNAWEZA KUWA MJINGA KIASI HIKI

KURA NI HAKI YA KIKATIBA, SIO SIASA!!!

Prof: Maghembe: Vyuo vikuu havitafunguliwa hadi Novemba

Na Richard Makore

5th October 2010

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

Maghembe%20J(7).jpg

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe

Serikali imesema haitabadili uamuzi wake wa kufungua vyuo vya elimu mwezi Novemba mwaka huu kama ilivyopanga licha ya kuwepo shinikizo la wanafunzi wanaotaka vifunguliwe ili kuwawezesha kwenda kupiga kura kwa kuwa wengi wao walijiandiskisha vyuoni.
Uamuzi huo wa serikali ulitangazwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, na kuongeza kuwa vyuo vya elimu ya juu sio taasisi zinazoendesha siasa, bali ni maeneo yanayotumika kufundisha watalaamu wa kada mbalimbali
Profesa Maghembe alihoji ni kwa nini wanafunzi hao washinikize vyuo vifunguliwe kwa madai ya kutaka wakapige kura wakati wao hawahusiani na siasa zozote zinazoendelea hapa nchini na badala yake wao ni wanafunzi wanaohitaji kufundishwa ili wawe watalaamu wa baadaye.
“Chuo kikuu sio sehemu ya kwenda kufanya siasa, bali ni sehemu ya kufundisha watalaam mbalimbali na kwa kweli nashangaa hawa wanafunzi kushinikiza vyuo vifunguliwe,” alliliambia NIPASHE.
Alifafanua kwamba vyuo vyote vinapanga siku ya kuanza mwaka wa masomo kulingana na programu zao kwa mwaka mzima kwa kutegemea raslimali walizonazo.
Alisema mwaka huu muda wa kufungua umesogezwa mbele kutokana na kubadilika kwa mfumo wa udahili wa wanafunzi.
Profesa Maghembe alisema mabadiliko ya mfumo huo wa udahili kulilenga kurahisha kazi hiyo pamoja na kuziba mianya ya wanafunzi kudahiliwa zaidi ya chuo kimoja na hivyo kuwanyima wanafunzi nafasi wenzao wanaotaka kujiunga na vyuo.
Alifafanua kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ilitoa muda kwa watu waliotaka kuhamisha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura na kama wanafunzi hao hawakufanya hivyo serikali haina namna ya kuwasaidia ili waweze kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 31.
Wakati Profesa Maghembe akitoa msimamo huo wa serikali, juzi Nec nayo ilipigilia msumari wa mwisho baada ya kusema kuwa haitaweka utaratibu mwingine ili kuwawezesha wanafunzi wapatao 60,000 wa vyuo vikuu waliopo likizo kuweza kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
Kauli hiyo ya Nec ilitolewa juzi na Mkurugenzi wake, Rajabu Kiravu alipozungumza na Nipashe wakati akijibu hoja ya wanafunzi hao waliotaka kuwekewa utaratibu utakaowawezesha kupiga kura wakiwa likizo.
Wanafunzi hao na wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini ambao ni wapenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walitoa malalamiko hayo jana kwenye kongamano ambalo lilijadili masuala ya Uchaguzi Mkuu.
Kadhalika, wanafunzi hao waliitaka serikali kufungua vyuo vya elimu ya juu ili kuwapa fursa wanafunzi kupiga kura kwenye maeneo waliyojiandikishia na kwamba kama itashindwa kufanya hivyo watakuwa wanawanyima haki yao ya msingi kwa mujibu wa ibara ya 21 ya katiba.

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom